Erdogan Aapa “Kuifutilia Mbali” Twita Nchini Uturuki

Serikali ya Uturuki imeufunga mtandao wa Twita -sambamba na huduma ya Google iitwayo DNS, iliyokuwa inatumika kama njia ya mzunguko kufuatia kufungwa kwa mtandao wa twita. Inaonekana, hata hivyo, kuwa mpango wa serikali hiyo wa kudhibiti raia wa nchi hiyo kuwasiliana unakumbana na mipango kinzani, kwa kuwa twiti zinazotoka nchini Uturuki ndio kwanza zimeongezeka.

Kufungiwa kwa mtandao wa Twita, kulikoripotiwa kuathiri watu zaidi ya milioni 10 wanaotumia mtandao huo nchini Uturuki, hali iliyofuatia kuchapishwa kwa nyaraka zinazosemekana ‘kufunua’ ufisadi wa maswahiba wa karibu wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.

Taarifa za habari zinasema kuwa Erdogan ameahidi “kuufutilia mbali mtandao wa Twita” akiongeza kuwa kamwe hajali kile ambacho kingesemwa na jumuiya ya kimataifa.

Juan Cole anaelezea jaribio la Erdogan la kufungia huduma hiyo ya kijamii akiita “upuuzi”:

Jaribio la kipuuzi la Erdogan la kujaribu kudhibiti matumizi ya mtandao wa intaneti limekwama na kushindwa mara moja. Vijana wa Kituruki wana weledi kuhusiana na matumizi ya zana za kupata huduma hiyo ziitwazo Tor na VPN, na watumiaji wa Twita nchini Uturuki walijipanga haraka sana kiasi ambacho huenda kilimchanganya kichwa ndugu Erdogan.

Erik Meyersson anaongeza:

Watumiaji wa mtandao wa Twita nchini Uturuki walimgundua @torproject mwaka jana, haishangazi watu bado wanatwiti pamoja na kufungiwa kwa mtandao huo nchini Uturuki

Na mtafiti wa Uturuki Zeynep Tufekci anatabasamu muda wote amvao watumiaji wa mtandao wa twita nchini Uturuki wanapaza sauti zao pamoja na kufungiwa kwa mtandao huo:

Ingawa mtandao umefungiwa bado twiti milioni 1.2 zimeendelea kutumwa nchini Uturuki

Hata hivyo, anaongeza:

Kufungiwa kwa DNS, ikifuatiwa na kufungiwa kwa IPS, nani ajuaye nini kinafuata. Uturuki iko mbioni kuwa na weledi wa hali ya juu wa masuala ya kiteknoloji. Kinachofuta ni mradi wa Tor

Kutoka Uturuki, Engin Onder anaeleza namna watumiaji wa Twita walivyosambaza ujumbe wa namna ya “kuuzunguka” ufungiaji huo:

Mtandao wa twita umefungiwa leo nchini Uturuki, jamaa wanatengeneza huduma ya DSN ya google kwenye mabango ya chama tawala

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.