- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wamalagasi Wajadili Kivazi na Maoni ya Mlimbwende wa Kigeni Kuhusu Madagaska

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Mazingira, Safari, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Upiga Picha, Vichekesho

Picha ya Tangazo la Kivazi cha Kuogolea 2014 [1] iliyopigwa eneo la (kisiwa cha) Nosy Iranja, Madagaska:

Nosy Iranja ni kisiwa kinachofahamika kama Turtle kwa sababu viumbe waitwao Hawksbill Turtles walikuja ufukweni kutaga mayai yao. Kisiwa hicho pia kinafahamika kwa mchanga wa pekee unaounganisha visiwa hivyo viwili.

Nosy Iranja, Madagascar - Public Domain

Nosy Iranja, Madagaska – Kwa matumizi ya umma

Mlimbende mashuhuri wa ki-Rusi Irina Shayk na mke wa msakata kandanda Cristiano Ronaldo alisema kwamba ana uhusiano maalumu na Madagaska [2]:

Nilipokuwa mwanafunzi niliripoti kuhusu Madagaska, na tangu wakati huo imekuwa ni ndoto yangu kubwa kwenda kule [..] Watu (Malagasi) wanaishi na kutembea kila siku kwenye barabara, wakiishi maisha ya kawaida, na bado wanafuraha. Ni uzoefu unaokufanya uwe mnyenyekevu, na kuyatafakari mambo katika kina chake.

Rakotonirina Miaro anashangaa kwa nini ulimwengu nje ya Madagaska wanaonekana kuvutiwa mno na utajiri wa kisiwa hicho laini raia wa Kimalagarasi hawaonekani kujali [3] [mg]:

Ny olon-kafa maita ny hatsaran'ny Nosin-tsik fa ny tompony jay no tsy mahafatatra fa tsar i Gasikara! Tsara daholo ny mannequin naka sary é!

Wageni wanajua ni kwa jinsi gani kisiwa chetu kina uzuri wa asili lakini sisi, tunaoishi hapa, hatuonekani kuvutiwa na raslimali zetu wenyewe. Ndio, na picha za nguo za kuogelea hazikuwa mbaya kuzitazama hata hivyo