Theluji Nchini Iran: Watu 500,000 Wakosa Umeme, Nishati ya Gesi Pamoja na Maji

Snow in Mazandaran. Source: Mehr. Photographer: Pejman Marzi.

Theluji huko Mazandaran. Chanzo: Mehr News Agency. Mpiga picha: Pejman Marzi.

Inataarifiwa kuwa watu 500,000 wameshindwa kutoka katika vijiji wanavyoishi huku wakikosa huduma ya umeme, nishati ya gesi pamoja na maji hali iliyotokana na kutanda kwa theluji mwisho wa wiki hii Kaskazini mwa nchi ya Iran katika majimbo ya, Gilan na Mazandaran.

Afisa mmoja alisema kuwa hili ni anguko kubwa la theluji ambalo halikuwahi kutokea kwa miaka 50 iliyopita. Hadi sasa, maelfu ya watu wameshaokolewa na kupelekwa kwenye makazi ya muda au kulazwa hospitalini.

ZA1-1RA alitwiti:

Sina shaka na familia yangu, wana hifadhi ya kutosha ya mchele kwa matumizi ya miezi kadhaa.

Farshad Faryabi alitwiti:

Waziri wa mambo ya nje wa Swiden, Carl Blidt, [aliyeko safarini nchini Iran] hataweza kurudi Swiden kutoka na hali tete ya theluji nchini Iran.

Soheila Sadegh alitwiti:

Theluji nzito yaharibu vibaya shule huko Gilan.

Maysam Bizar alitwiti:

Gharama ya maji ya chupa yalipanda mara nne zaidi ya bei ya kawaida katika kipindi cha tatizo la theluji. Kama hatuwezi kujihurumia, labda cha kufanya ni kutegemea maadui?

Mozdeh A alitwiti:

Kilicho na Baraka kwa wengine, kwetu ni laana.

Saham Borghani mwezi uliopita (tar 10 Januari) aliweka picha ya chain a barafu.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.