Soka pekee huigawa Tanzania

The Benjamin Mkapa National Stadium in Dar es Salaam, Tanzania. Photo by Omar Mohammed

Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa Dar es SalaamTanzania. Picha na Omar Mohammed

Dar es Salaam, Tanzania — Unapozungumzia upinzani wa soka, ni mara chache hapa Afrika utakutana unaoshinda ule wa kati ya simba na Yanga (known locally as Yanga). Zote zinatoka kwenye mji ambao unaaminika kuwa ndiyo kitovu cha biashara, Dar es Salaam, ndizo timu mbili kubwa na kongwe nchini Tanzania. Wameshinda idadi kubwa ya vikombe, wanajivunia idadi ya mashabiki wengi, na kwenye vikosi vyao utakuta wachezaji bora wenye vipaji wanavyowakilisha taifa.

Timu hizi mbili zinapokutana, Dar es Salaam inabadilishwa. Ni kama umeme wa aina Fulani unapita jijini. Ni hafifu, lakini nguvu yake inaonekana, na uchangamfu wa jiji la Dar ukiongezeka kwa kiasi fulani.
Tanzania imekuwa ikijivunia umoja wa watu wake ambao hauwezi kuingiliwa. Sisi ni Tanzania kwanza, kabla ya rangi, dini au ukabila. Lakini siku ya watani wa jadi wanapokutana Dar es Salaam hugawanyika katika pande mbili. Watu huvalia mavazi maarufu yenye rangi nyekundu na nyeupe kwa wapenzi wa Simba au kijani na njano kwa wapenzi wa Yanga. Kila kona za mitaa utaona bendera zikiwa na nembo za timu husika, ilimradi tu kuwachanganya wapizani. Magari nayo yanabandikwa vipeperushi vya moja ya timu kuonesha ushabiki wa dreva. Yenye picha kubwa ya mnyama Simba ni ya timu ya Simba na ile ya mwenge unaonekana ndani ya ramani ya Afrika ni Yanga. Na siku ya pambano lenyewe, hakuna kitu kinachoitwa kutokuwa na upande jijini Dar.

Ninachuruzika damu nyekundu

Mimi ni shabiki wa Simba. Siku zote nimekuwa na nitaendelea kuwa hivyo. Mahusiano yangu na Simba yapo imara. Baba yangu, Mohammed Hadi Tamimi, aliichezea timu hii mwishoni mwa miaka ya 60 hadi mwanzoni mwa miaka ya 70 wakati huo ikiitwa Sunderland. Nilipokuwa kijana mdogo, nilikuwa nikiamka mapema siku ya pambano na watani wetu, nakuchukua kisanduku changu cha Simba na mjomba wangu hunibeba kwenye mabega yake na tunaelekea uwanjani.

"One day, everyone will be Simba SC's supporter." Photo by Omar Mohammed

““ siku moja, kila mtu atakuwa mfuasi wa simba.” Picha na Omar Mohammed

Kumbukumbu zangu kwa hizo siku imejawa na maumivu ya moyo. Nakumbuka mechi nyingi tulizofungwa, na hali ya kukata tamaa iliyofuata. Mchezaji mmoja kwenye Simba ndio alikuwa ni tatizo. Said Sued “Scud” aliyeichezea Yanga miaka ya 90 na utaalamu wake ulikuwa ni kuifunga simba. Kwa kiasi alikuwa na uzito uliopitiliza kwa hiyo hakuwa akicheza mara mara, lakini inapotokea siku anacheza ilikuwa kama haizuiliki kwamba ataifungia timu yake, na mashambulizi hatari yaliyomfanya ajitengenezee jina la “Skadi”.
Kwa kadri ninavyozidi kukua, kujitoa kwangu kwa ajili ya simba kumepungua kwa kiasi fulani. Miaka kumi iliyopita nilipata kuhudhuria si zaidi ya mechi tatu za Simba na Yanga. Lakini siku za karibuni nimeanza kufuatilia maendeleo ya timu yangu ya kale na tena jumapili iliyopita baada ya kukosekana kwa muda mrefu, niliamua kwenda kutazama mechi hii ya watani wa jadi.

Ni ya kiwango tangu zamani zile 

Niliwasili, pamoja na baadhi ya rafiki zangu, katika uwanja mkubwa wenye uwezo wa kubeba watu 60,000 -Uwanja wa Taifa wa Benjamin William Mkapa yapata saa moja kabla ya saa kumi kamili mpira kuanza. Hali ya hewa ilishakuwa ya kuchangamsha, kukiwa na vikundi viwili vya mashabiki pinzani wakiimbiana. Wakati huo mechi ya timu za vijana ya timu hizo ilikuwa inaendelea. Nilivyochukua tu kiti changu nikaona hisia za wasiwasi zinaniingia.
Simba ilikuwa inakuja uwanjani wakiwa na hali nzuri kimchezo. Bado hawajafungwa na wanaongoza ligi, walikuwa wameshinda mechi tano kati ya nane walizocheza. Yanga, kwa upande mwingine walishaonja machungu ya kufungwa mechi moja msimu huu, lakini kushinda mechi nne na sare tatu, walikuwa nafasi ya nne, pointi tatu nyuma ya vinara wa ligi.

Simba players in a huddle before kick-off. Photo by Omar Mohammed

Wachezaji wa Simba wakipiga dua kabla ya kuanza mechi. Picha na Omar Mohammed

Lakini wakati mechi imeanza, ilikuwa ni yanga waliotoka getini katika hali ya unyonge. Walikaa na mpira kwa umakini na uangalifu na kutawala kipindi chote cha kwanza. Simba kama vile hawakuwa na uhakika na wanachokifanya, bila kujua wazi mbinu wanazotakiwa kutumia. Hawakuwa na nguvu kabisa, walihangaika mno kumiliki mpira, na badala yake kutegemea pasi ndefu mchezo ambao uliyopelekea kupoteza mipira, hii ikawaweka katika hali ya kucheza kwa kujilinda.
Shujaa wa kipindi cha kwanza bila shaka alikuwa namba 10 wa Yanga,
Mrisho Ngasa. Mchezaji huyu wa zamani wa Simba, alikuwa anaisababishia timu yake ya zamani kila aina ya usumbufu. Akicheza kati ya viungo na ushambuliaji, mwendo wake na mpira uliwachanganya kabisa nafasi ya ulinzi ya Simba langoni. Akiwa na mpira mwenendo wake uliwavuruga wabeki wanne wa nyuma wa Simba. Dakika ya 15 tu ya mchezo alizawadiwa kwa juhudi zake. Mpira uliorushwa kutoka kushoto ulimtoroka beki wa Simba na kutua kwenye njia ya Ngasa ambaye aliunyoosha nyavuni kuiandikia Yanga bao stahili la kuongoza.

Mrisho Ngasa, made life difficult for Simba's defense in the first half, celebrates opening the score for Yanga in the Dar Derby. Photo courtesy of Lenzi ya Michezo

Mrisho Ngasa, aliyeifanya kazi ya mabeki wa Simba kuwa ngumu katika kipindi cha kwanza, akishangilia bao lake la kwanza kwa Yanga katika mpambano wa Dar. Picha ya Lenzi ya Michezo.

Mambo yaliendelea kuwa mazuri kwa Yanga katika dakika ya 35. Baada ya Simba kushindwa kuondoa mpira uliorushwa ndani ya sita ya lango la Simba na kumkuta Hamis Kiiza aliyeusukuma na kuipa timu yake uongozi wa 2-0. Na punde tu kabla ya mapumziko, Yanga wakafunga tena. Baada ya pasi ndefu iliyounganishwa na kiungo Kavumbangu aliyemzunguka mlinzi wa Simba kabla ya kumtengenezea Kiiza, aliyeukata mpira huo na kufunga goli lake la pili kwenye mchezo huo. 3-0, Yanga. Yalikuwa kama mauaji.
Simba hawakuwa na wazo ni kitu gani kimewaangusha. Mwamuzi alipopiga filimbi kuashiria ni mapumziko, wachezaji wakahisi kupumua. Wapenzi wao walikuwa wameduwaa. Wengine waliona kwamba walichokiona kinatosha wakaamua kuondoka. Waliofanya hivyo walikuwa wakose ujio mkubwa katika historia ya mechi ya watani wa jadi.
Mapema baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Simba wakafanya mabadiliko mawili. Viungo William Lucian na Said Ndemla wakaingia kumsaidia Haroun Chanongo aliyelemewa na Abdulhalim Humuod. Kuingia kwa washambuliaji wawili makinda kulibadilisha kabisa mchezo. Ghafla viungo wa Simba, wakachangamka, haraka haraka tofauti na kipindi cha kipindi kwanza, wakauchukua na kuutawala mchezo. Hasa Lucian na Ndemla, waliongezea nguvu safu ya ushamuliaji ya Simba na mapema iwezekanavyo ikawasaidia Simba kuanza kupunguza magoli.
Kisha, katika dakika ya 54, Yanga walishindwa kuizuia presha kutoka kwa washambuliaji wa Simba na kusababisha mshambuliaji wa Simba Bertram Mombeki kwenye nafasi ya kupiga mpira juu ya nyavu, hii kidogo ikaipa timu yake matumaini.
Dakika chache baadae,kona iliyochongwa na Ramadhan Singano iliunganishwa kwa nguvu na beki wa kati wa Uganda Joseph Owino na ghafla ikawa 3-2, sasa mpira ukawa kwenye mikono yetu.

Wapenzi wa Yanga wakaonekana kukosa pumzi na kuishiwa nguvu wakati wale wa Simba wakiamini kwamba kurudi kwao inawezekana ikawa kweli. Kelele ndani ya uwanja zilikuwa za juu, zikisisitiza ‘Twende Simba!’’
Lakini Yanga walikuwa bado hawajamaliza. Ngasa sasa akiwa mpole kipindi cha pili, aliliwania goli la wazi, lakini awamu hii shuti lake liliokolewa na kipa wa Simba Abel Dhaira. Ni wazi kabisa kwamba Ngassa aliijutia nafasi hiyo. Dakika tano kabla ya mpira kumalizika, Simba wakapata adhabu ndogo kutokea winga ya kulia, karibu na ndani ya lango la Yanga. Krosi hiyo yenye matokeo ilitengenezwa na Gilbert Kaze, aliyegonga kichwa safi na kuisawazishia simba kusababishia rangi nyeupe na nyekundu nusu ya uwanja kuzizima. Kurudi kwa simba kukawa kumekamilika.

Final Score in the Dar Derby. Photo by Omar Mohammed

Matokeo ya mwisho katika pambano hilo. Picha na Omar Mohammed

Ulikuwa ni mgeuko wa kushtua, mara ya kwanza katika historia ya timu hizi kukutana kwamba wameweza kumaliza kwa matokeo hayo. Mechi iliisha kwa bao 3-3.
Dakika chache baadae, baada ya mwamuzi kupiga kipenga kuashiria pambano kuisha, baadhi ya wachezaji wa simba walianguka uwanjani, wasiamini kilichotokea. Walioweza kusimama waliwadhihaki washindani wao, wakiwasema kwamba wamekuwa ni sehemu ya mechi hiyo kubwa isiyosahaulika na ambayo itadumu kwenye kumbukumbu za mashabiki wao.

Omar Mohammed ni mwandishi wa habari Mtanzania anayeishi Dar es Salaam. Anatwiti katika  @shurufu.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.