Jieleze:Siku ya Blogu kwa Haki za Raia!

Human rights

Picha ya siku ya haki za binadamu. Na Catching.Light kwenye mtandao wa Flickr (CC-BY)

Tangu 2007, Siku ya Blogu imekuwa ikiwaalika wanablogu duniani kushiriki kwa mtiririko huu: Siku moja, Mada mmoja, maelfu ya sauti. Mada ya mwaka huu ni Haki za Binadamu – na tarehe ni Oktoba 16. Jitihada za pamoja, wanablogu, watangazaji wa mtandao na wengine walizungumzia masuala ya kidunia -na namna nzuri ya kuzungumzia haki za binadamu kuliko kutumia maneno yaliyozoeleka: “Yeyote ana haki ya uhuru wa maoni na kujieleza” (Tamko la Haki za Binadamu, Ibara ya 20).

Kwenye mtandao wa Global Voices mara kadhaa huwa tunajadili masuala ya haki za binadamu, hasa kwenye maeneo yenye uhusiano na ufuatiliwaji wa mtandaoni, upepelezi na uhuru wa maoni mtandaoni. Tunatarajia kuwa na siku moja kwa ajili ya kutafakari na kuzungumza kuhusiana na mada hiyo ambayo daima imekuwa na umuhimu wake.

Mpaka sasa, blogu 1,377 kutoka kwenye nchi 114 zimejiandikisha kuhusika na Siku ya Blogu 2013. Andikisha blogu yako leo, na jiunge na mazungumzo ya kidunia! Alamahabari (tags) za mwaka huu ni #BAD13, #HumanRights, #Oct16.

Kama kawaida, tutaorodhesha michango ya waandishi wa Global Voices duniani kote – kaa tayari!

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.