Je, Kutakuwa na Fungate kwa Marekani na Irani?

President Hassan Rouhani and President Barack Obama. Via Iran-emrooz.net

Marais wa Iran na Marekani: Hassan Rouhani na Barack Obama. Kupitia Iran-emrooz.net

Wiki moja tu baada ya tukio la kihistoria la kupigiana simu kati ya rais mpya wa Iran, Hassan Rouhani, na Barack Obama, bado kuna minong'ono miongoni mwa wa-Irani kuhusu “Kufa kwa Marekani” na kuchoma bendera za Marekani na Israeli baada ya swala ya Ijumaa mjini Tehran Oktoba 4, 2013.

Bado, baadhi ya wa-Iran wanatarajia kuwa simu hiyo ilikuwa ni hatua nzuri katika kuimarisha mahusiano ambayo yangeweza kufanya vikwazo vya Marekani viongozwe. Wengine hawakufurahia mazungumzo hayo na “Shetani Mkuu,” jina ambalo Marekani huitwa kila hotuba rasmi za Iran zinapotolewa.

Katika kuonyesha kuwa mada hii imo kwenye kichwa kwa Rais Rouhani, ameripotiwa kuyaomba mashirika mawili ya kura ya maoni “kutafiti” kile wa-Irani wanachofikiri kuhusu mahusiano ya Marekani na Irani. Wakati huo huo, watumiaji wa mtandaoni walitoa maoni yao kuhusu matukio hayo kati ya nchi hizo mbili.

Mwananchi mmoja wa Iran aliweka video yake kwenye mtandao wa YouTube, ikipendekeza kuwa Rouhani aongeze maswali ya ziada kwenye utafiti wake:

- “Watu wangapi wanahitaji utawala wa Jamhuri ya Kiislamu?”
– “Wanafikiri nini kuhusu uhuru wa kijamii na kisiasa?”
– “Wewe [Rais Rouhani] umesema hapakuwa na udanganyifu katika uchaguzi wa rais 2009 uliokuwa na malalamiko mengi, hebu tuwaulize wa-Iran wanafikiri nini kuhusu jambo hilo”

Zarebin anaandika [fa] katika blogu yake kuwa utafiti huo utahandisiwa kwa namna yoyote ambayo Kiongozi Mkuu atataka. Kama anataka kukarabati mahusiano na Marekani, hivyo utafiti utaonyesha hilo. “Tumetengwa namna gani. Kila kitu ni maoni ya Kiongozi huyo na utafiti ni kujaribu kuthibitisha hicho hicho.”

Tusema au Tusiseme

Firoozeh alitwiti:

Katika uhusiano wowote, uwe wa kidiplomasia au usio wa kidiplomasia, lazima twende kwa makini.

Akiungana na utawala wa Kiislamu, mwanablogu Khabrnegar1351 anaandika[fa] kuwa Iran imekuwa na nguvu kiasi cha Marekani “kuitazama Iran kama taifa lenye nguvu duniani” na “itakusudia kujenga mahusiano na Tehran kwa woga tu.”

Mwanablogu mwingine, Ahestan, anatukumbusha mafundisho ya mpinzani wa Marekani Ayatollah Khomeini, mwasisi wa taifa hilo la ki-Islamu anayesema [fa], “Mshindi halisi wa mazugumzo ya Obama-Rouhani ni Obama.” Mwnaablogu huyu anasema lengo kuu la simu hiyo lilikuwa kuwaonyesha mamilioni ya Waislamu wanaofuata mafundisho ya Imam huyo [Khomeini] kwamba Iran iko tayari kuzungumza na “Shetani Mkuu.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.