Wafanyakazi wa Kujitolea Raia wa Ki-Hispania Waachiliwa Huru Baada ya Miezi 21 Uhamishoni

Tangazo la kuachiliwa huru kusikotarajiwa kwa wafanyakazi wawili wa Hispania wa misaada waliokuwa wakifanya kazi katika Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka, na kutekwa nyara Oktoba 13, 2011, lilitoka baada ya miezi 21 ya utumwa.

Wakati walipotekwa nyara, Montserrat Serra na Blanca Thiebaut walikuwa wafanyakazi katika hospitali ilikuwa imeanzishwa huko Dadaab, kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani [es], iliyoko karibu na mpaka wa Somalia nchini Kenya, na inayohifadhi watu wasiopungua nusu milioni ya Wasomali wanaokimbia ukame na vita katika nchi yao. Inaaminika kwamba akina dada hao wa kujitolea walipelekwa nchini Somalia baada ya kutekwa nyara na kubaki huko kwa muda huo wote.

Montserrat Serra (izquierda) y Blanca Thiebaut, las dos cooperantes españolas liberadas tras un secuestro de 21 meses en Somalia. Foto publicada en Twitter por José Campos.

Montserrat Serra (kushoto) y Blanca Thiebaut, wafanyakazi wawili wa Ki-Hispania wa misaada walioachiliwa huru baada ya miezi 21 ya kutekwa nyara nchini Somalia. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa twita na José Campos.

Haiko wazi vilevile ikiwa watekaji wao walikuwa wahalifu wa kawaida au wanachama wa kikundi cha Al Qaeda, ingawa waangalizi wengi wanalichukulia tukio hilo kama lililofanywa na magaidi. Madaktari Wasiokuwa na Mipaka waliitisha mkutano wa waandishi wa habari baada ya habari hiyo, lakini José Antonio Bastos, Rais wa DWB Hispania, alisema hawangetoa taarifa juu ya mchakato wa ukombozi “ili kutokusababisha matatizo kwa watu wengine wanaojitolea nchini Somalia pamoja na watoa habari.” Shirika hilo ndilo lililokuw likifanya maelewano yaliyosababisha kuachiwa huru wafanyakazi hao. Serikali ya Uhispania haikuingilia kati suala hilo. Kisicho wazi ni kama fidia ilipwa, kiasi kilichotakiwa kulipwa, au nani aliyechukua jukumu la kulipa malipo yaliyotakiwa.

Wengi walisheherekea kuachiliwa huru kwa wanawake hao wawili, kama vile Beli Alvarez[es], aliyetwiti:

@Beli_AlvarezMensaje de cariño y bienvenida a las dos cooperantes españolas de @MSF_espana Enhorabuena a esta ong por su labor tan grande en el mundo

@Beli_Alvarez: Ujumbe wa upendo wa kuwakaribisha wafanyakazi wawili wa misaada wa ki-Hispania kutoka @MSF_espana Hongera AZISE hii kwa kazi ya kubwa inayoifanya dunia kote

Hata hivyo, sio kila ujumbe ulikuwa ni wa pongezi. Raia wengi wa Mtandao  hawakujali kuwa serikali ya Kihispania ilikuwa imelipa fidia kwa ajili ya wafanyakazi hao na wakaonyesha kutoridhika kwao, wakati mwingine wakiwalaumu wafanyakazi hao kwa kutokuogopa hatari na kujitafutia matatizo yao wenyewe.

burbman89 alitoa maoni hii kwenye habari hiyo, ambayo yalionekana kwenye 20minutos.es [es]:

Vamos, que nos ha costado una pasta a todos los españoles que estas “buenas samaritanas” se vayan por ahí a darle alegría al cuerpo…. pero porque no se quedarán en casita!!!!

Jamani, imetugharimu sana sisi Wahispania kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya hawa “wasamaria wema” kwenda huko kuwafanya waponde raha …. kwa nini wao wasikae nyumbani!!!

Katika chombo hicho hicho cha habari, 1-2-3-4 [es] waliwalaumu wafanyakazi hao wa kujitolea kwa uwezekano wa mashambulizi ya Al Qaeda kwa siku za usoni:

Rueda de prensa de Médicos Sin Fronteras España para anunciar la liberación de las dos cooperantes. Imagen publicada en Twitter por MSF Prensa.

Madakatari Wasiokuwa na Mipaka nchini Uhispania wakiwa kwenye mkutano na vyombo vya habari kutangaza kuachiliwa huru kwa wafanyakazi wawili wa kujitolea.  Picha zimechapishwa kwenye Mtandao wa Twita na DWB Press.

(…) los islamistas comprarán armas con los millones de euros que les hemos regalado. Armas con las que los islamistas secuestrarán a mas occidentales y con las que asesinarán a un montón de africanos. Armas con las que cometerán atentados.

El daño causado por estas “cooperantes solidarias” es incalculable.

(…) Waislam watanunua silaha kwa mamilioni ya Euro tulizo wapa. Silaha ambazo Waislam watazitumia kuteka nyara zaidi raia wa Magharibi na kuwaua Waafrika wengi. Silaha ambazo kwazo hufanyia mashambulizi.

Madhara yanayosababishwa na hawa “wafanyakazi wa misaada” hayahesabiki.

Katika safu yake, “hali haiko tena kama ilivyokuwa” [es], katika  jarida  la La Gaceta, Rafael Bardají anasema kwamba [es]

[los cooperantes] Ya no son elementos neutrales a los que se respeta, sino que son una pieza más en los conflictos. Y eso es algo que afecta no sólo a su seguridad personal sino a todo el Estado (…). Pagarles por lo que hacen y pagar por la liberación de sus miembros es amoral e insostenible.

[wafanyakazi wa kujitolea] wamebadilika na si wale tuliowajua kuwa hawana upande wowote na waliheshimiwa, lakini badala yake wamekuwa ni sehemu ya migogoro. Na hili ni jambo ambalo huathiri si tu usalama wao binafsi, bali hata wa Nchi nzima (…). Kuwalipa kwa  wanachokifanya na tena kulipa ili watoe wafanyakazi wao ni kinyume na maadili na ni kazi isiyoweza kuendelea kwa muda mrefu.

Katika hali hiyo hiyo, Ricardo Peytaví anatoa maoni yake katika safu yake ya Upotevu ambao sote huulipia [es] katika gazeti la mtandaoni la El Dia

Lo único que quiero es saber cuánto me cuesta todo esto en parte alícuota, habida cuenta de que este mes he pagado en impuestos más de un tercio de mis ingresos brutos. (…) cualquier ciudadano de este país se ha convertido en pieza fácil para todo facineroso que desee ganar dinero fácil.

Kitu pekee ambacho nataka kujua ni kiasi gani haya yote hunigharamu mimi kwa maana ya hisa, kutokana na kwamba mwezi huu mimi nimelipa zaidi ya theluthi moja ya mapato yangu katika kodi. (…) Raia yeyote wa nchi hii amekuwa mhanga rahisi kwa  kila chenye jinai ambacho kinachotaka kupata fedha kwa urahisi.

Hata hivyo, kuna raia wa mtandao na wanablogu wengi pia ambao wanafurahia matokeo mazuri ya utekaji nyara, na kupongeza kazi ya wafanyakazi wa kujitolea na hata shirika lenyewe katika jamii yenye mazingira magumu kama yale ya wakimbizi. Belen de la Banda alizungumza kuhusu hili katika blogu ya 3500 millones [es]:

Blanca, Montse y sus compañeros de profesión son los referentes morales que estamos necesitando en estos tiempos de incertidumbre y desconfianza. (…) nuestra sociedad debería buscar el modo de que sientan también nuestro abrazo, para agradecer el esfuerzo ímprobo y valioso de un trabajo que les ha llevado a esta situación extrema. Porque personas como ellas hacen que nuestro país y nuestro mundo sean mejores.

Blanca, Montse, na wenzao ni mifano ya kimaadili kwamba tunawahitaji katika nyakati hizi za kutokuwa na uhakika na kutoaminiana. (…) Jamii yetu yapaswa kutafuta njia ya kuhisi ukaribu wetu, kukubali juhudi kubwa sana na kazi muhimu ambayo imesababisha hali hii ya kupindukia. Kwa sababu watu kama wao huifanya nchi na dunia yetu kuwa bora.

Na 1358 aliacha maoni haya [es] kwenye habari ya iliyoonekana kwenye El Pais
[es]:

Las cooperantes, a su llegada a España tras su liberación. Imagen de la web de RTVE.

Kuwasili kwa wafanyakazi wa kujitolea Uhispania kufuatia kuachiliwa kwao. Picha kutoka kwa tovuti ya RTVE.

Me uno a aquellos que SE ALEGRAN por la vuelta a casa de estás dos Personas y como CONTRIBUYENTE me PARECE MUY BIEN si es que se ha tenido que pagar por su liberación. La vida, incluso de aquellos que nos caen mál no tiene précio y mucho mejor gastarse el dinero (si es que se ha hecho) en PERSONAS que no en juegos de indios y vaqueros para que cuatro VAGOS jueguen y se crean chonvaine en “misiones” de “paz” y “reconstrucción”.

Ninaungana na wale ambao WANA FURAHA kwa kurudi nyumbani ya watu hawa wawili na kama MLIPAKODI INAONEKANA VYEMA SANA kwangu mimi ikiwa kuachiliwa kwao kulipaswa kulipiwa. Maisha, hata maisha ya wale ambao sisi hatuwapendi, hayana bei na ni bora zaidi kutumia fedha (kama imefanyika) kwa WATU kuliko kwa michezo ya Wahindi ili WAZEMBE wanne wacheze na kujiamini wenyewe kuwa mashujaa katika “huduma” wa “amani” na “mageuzi.”

Pamoja na utata ambao umetokana na malipo ya kuwaokoa, habari njema ni kwamba Montserrat Serra na Blanca Thiebaut wako pamoja na familia zao, salama na wazima. Madaktari DWB pamoja na wanasaikolojia wamewahudumia tangu kuachiliwa kwao wameshauri kwamba wapewe muda wa kupata nafuu na kukabiliana na pilika pilika za maisha kwa mara nyingine tena, kumaanisha kwamba watu watasubiri kwa muda kabla hawajaweza kuzungumza kuhusu jinsi walivyoishi utumwani katika miezi hii 21. Walionekana tu wakishuka kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Madrid, wakionekana kukonda na kuonekana kuchoka, lakini wakitabasamu. Ni matumaini watapona haraka na kurudi kwa maisha yao ya kawaida hivi karibuni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.