Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi

Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu [ru] katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa. Nafasi tano za Ugavana zilikuwa zikigombaniwa, kwa mara ya kwanza tangu Vladimir Putin kufutilia mbali chaguzi kama hizo miaka saba iliyopita.

Mbinu chafu na vitendo vya kupakana matope

Wakati kivumbi hicho cha uchaguzi kilipotulia, matokeo yalionyesha kuwa wanachama wa vuguvugu la upinzani hawakufanya vizuri katika maeneo machache ambayo walifanikiwa kusimamisha wagombea. Chama cha Umoja cha Urusi (URP), na wagombea wengine ambao walikuwa ni mashabiki wa Putin, walijizolea kura nyingi katika nafasi mbalimbali. Vyama pekee vya upinzani kufurahia angalia mafanikio kidogo walikuwa walewale: Wakomunisti, chama LDPR, na kile cha Just Urusi. Bado haijafahamika sawasawa ni kiasi gani mafanikio ya chama cha United Russia yametokana na wizi wa kura na tuhuma za vitendo visivyokubalika. Hata hivyo, kulikuwa na taarifa ya kuenea ya mbinu chafu.

Evgeniya Chirikova, Kiongozi wa Watetezi wa Msitu wa Khimki, ulioko sehemu ya Khimki, Urusi ( Aprili 19, 2011), Kwa hisani ya Daniel Beilinson, CC 2.0.

For example, journalist Dmitry Aleshkovsky blogged about the elections in a small district in the republic of Tatarstan in very 

Kwa mfano, mwandishi wa habari Dmitry Aleshkovsky aliblogu kuhusu uchaguzi huo katika wilaya ndogo katika jamhuri ya Tatarstan kwa kutumia lugha kali[ru]:

Я видел умирающих от холеры людей в тени развалин разрушенного землетрясением Порт-о-Пренса, я видел тысячи сожженных домов в грузинских селах Южной Осетии […]. И эти выборы вызывают во мне примерно такое же количество ужаса, как и всё описанное выше.

Nimeona raia wakipoteza maisha kwa magojwa kama kipindupindu katika kivuli cha nyumba zilizoharibika huko Port-au-Prince zilizobomolewa na tetemeko, nimeona maelfu ya nyumba jijini Georgia zilizochomwa katika vijiji vya Ossetia ya Kusini […]. Chaguzi hizi [Za Serikali za Mitaa] hufanya nijisikie vibaya vilevile kwa kiasi nilichokieleza hapo juu.

Aleshkovsky aliendelea kuelezea ukiukwaji wa taratibu mbalimbali za uchaguzi, kuanzia vitendo vya kuongeza kura za ziada katika masanduku ya kupigia kura mpaka kuondolewa kwa nguvu kwa waangalizi huru.

Kiwango ambacho udanganyifu ulifanywa na vibaraka wa serikali tarajiwa ulikuwepo, hata katika uchaguzi mdogo kama hizi tena kwa nafasi ndogo kama udiwani, kinashangaza sana. Sergey Ezhov, mwanachama wa Limonov, ambalo ni vuguvugu la siasa nchini Urusi aligombea nafasi ya halmashauri ya jiji katika mji mdogo wa Sarai. Alielezea  [ru] yale aliyokumbana nayo kupitia blogu yake:

Беспредел началася за несколько дней до даты голосования. Когда, видимо, жулики поняли, что я прохожу в депутаты. Спокойные и тихие Сараи завалили лживыми и прокационными листовками, по месту работы и учебы собирали избирателей и приказывали ни в коем случае не голосовать за Ежова. В это же время полиция начала препятствовать в агитации нам.

Uvunjifu wa sheria ulianza siku chache kabla ya kura. Wakati jamaa waligutuka kwamba naelekea kushinda uchaguzi. Mji mdogo wa Sarai ambao una sifa ya utulivu na amani ghafla ulifuka vipeperushi vya uongo na kupakana matope, wapiga kura walifuatwa kokote walikokuwa iwe ni makazini au mashuleni, na kuambiwa wasimpigie Ezhov kura kwa sababu yoyote. Wakati huo huo, polisi walianza kuvuruga kampeni yetu.

Ezhov alipoteza uchaguzi. Awali alidhani kuwa nafasi ndogo kama hiyo aliyogombea ingempa kinga ya kushambuliwa na serikali. Ni wazi, alikuwa amefikiri kimakosa. Kama ilivyokuja kuwa, baadhi ya mbinu hizo chafu zilitumika dhidi ya wagombea wengine wa chama cha United Russia kwa kutumia wanachama wa chama hichohicho cha United Russia. Hayo yalitokea Angara, kama alivyoripoti [ru] Sergey Schmidt, Profesa wa sayansi ya siasa wa chuo kimoja sehemu hiyo. Mgombea wa Umeya wa chama cha United Russia alijikuta na wakati mgumu – kampeni zake zikitingishwa na kashfa baada ya kashfa, gavana tena kwa waziwazi alimsaidia mpinzani wake, na kadhalika. Mwishowe alishinda, hata hivyo, kwa kiasi kikubwa kwa sababu wapiga kura walitaka “kumwuunga mkono na kumsaidia mtu aliyeonekana ni dhaifu,” Schmidt anasema. Inaonekana kwamba siasa za kupakana matope zilikuwa zimekithiri.
Mayai yote katika kapu moja, penye usalama zaidi

Picha kutoka tovuti ya tume ya uchaguzi ya upinzani kwa uratibu wa kura za baraza. Oktoba 19, 2012.

Ilivyoonekana, kiongozi wa upinzani naye pia alishindwa uchaguzi. Dhamira ya Evgenya Chirikova kuwa meya katika kitongoji cha Khimki jijini Moscow ndiyo ilionyesha ushindani ambapo wapinzani waliungana pamoja, wakipata michango ya fedha na watu wa kujitolea kufanya kampeni. Bado, Chirikova alishindwa, akiambulia 20% ya kura. Ingawa kulikuwa na matukio ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, tovuti ya yatokanayo na uchaguzi[ru] ilithibitisha rasmi matokeo rasmi ya kura. Chirikova alishindwa, ingawa yeye ni mmoja wa viongozi bora na maarufu wa upinzani, hasa huko Khimki, ambapo yu mwanachama hai wa jamii ya sehemu hiyo.

Kwa kifupi, upinzani ulifanya vibaya katika uchaguzi huo. Hili halina ubishi. Lakini pia hakuna ubishi kuwa wanapinzani waijiandaa kushinda uchaguzi huu. Chirikova kwa ukweli  alikuwa mgombea pekee mkubwa kuwakilisha upinzani. Uchaguzi wa mitaa ungeweza kuwa fursa kubwa ya kujaribu kufanya kampeni katika ngazi ya mitaa na labda kuzishusha harakati za upinzani kwa wananchi. Hata hivyo nafasi hiyo inaonekana kuwa imepeperushwa na upepo. Kwa mwezi mzima uliopita, uchaguzi wa wa Oktoba 14 haukuonekana katika duru za blogu (Isipokuwa Chirikova pekee kuthibitisha kanuni hiyo).

Hakika, kwa mwezi wote uliopita, raia wa mtandaoni wa Kirusi wamekuwa wakipumbazwa na chaguzi kadhaa – uchaguzi wa mtandaoni kwa Baraza  la Uratibu wa Upinzani, kuanzia leo na kuishia tarehe 21 Oktoba. Badala ya kushindana katika uchaguzi rasmi, baadhi ya wanaharakati wa sehemu hizo walichuana katika uchaguzi wa Uratibu Baraza, wakishiriki katika midahalo ya televisheni, mashindano ya insha, kupiga kampeni, kupoteza muda katika misuguano ya ndani ya chama – yote hayo kwa ajili ya kugombea nafasi katika taasisi ambayo haitakuwa na meno yoyote, hata kama itakuja kuwepo.

Labda, kama nguvu ya kuwahamasisha wapiga kura ambao ni watumiaji wa mtandao kwenda kuwa wapiga kura ingetumika kuhamasisha wapiga kura halisi, ingelifanikiwa katika kuongeza kidogo idadi ya waliojitokeza kupiga kura Oktoba 14 (hasa kwa kuzingatia jinsi ni vigumu kuwa wapiga kura hakika kwenye cvk2012.org [ru]). Kama ilivyo sasa, ni kama vile Uratibu Baraza ulisababisha uchaguzi mchovu. Ni matumaini ilipaswa kuwa hivvo.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.