Uganda: Kukumbuka milipuko ya mabomu ya 2010

Makala haya yamechapishwa kwa kuchelewa kutokana na hitilafu za kiufundi. Awali yalikuwa yawe yamechapishwa tarehe 13 Julai 2012.

Ni miaka miwili sasa tangu jumla ya watu 80 kupoteza maisha katika mililipuko ya mabomu katika klubu ya mcheo wa Rugby huko Kyaddondo na katika baa ya Kijiji cha ki-Ethipoia nchini Uganda. Wahanga hawa walikuwa wamekwenda kutazama finali za kandanda za kombe la dunia zilizokuwa zinafanyika nchini Afrika kusini ambapo kwa mara ya kwanza bara la Afrika lilikuwa limeandaa michuano hiyo. Mashabiki hao walikuwa wamesubiri kwa hamu mechi hiyo ya fainali kati ya Uholanzi na Hispania.

Ilikuwa inaelekea usiku wa manane wakati milipuko hiyo ikitokea, shambulizi ambalo liliwaacha watu sabini wakiwa wamefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.

Mnara wa kumbukumbu ya mashambuzi hayo huko Kyaddondo

 

Waandishi wa vyombo vikuu vya habari viliwakumbuka wa-Ganda waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo. Wa-Ganda wengine kutoka seheme nyinginezo ulimwenguni  walituma jumbe zao kwenye mitandao ya facebook na twita  wakitumia alama habari ya #Twakumbuka Julai 11

@beewool alizungumza machache kwenye twita akisema:

@beewol‬ #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11 #Twakumbuka Julai 11‪‬ ‪‬ ‪‬ ‪‬ ‪‬ ‪

 

Aliongeza:

@beewol:  Mungu azirehemu roho za wapenda kandanda waliopoteza maisha mahali miaka miwili iliyopita na ziweke mahali pema peponi #Twakumbuka Julai 11

 

@pkahill alimkumbuka rafiki yake:

@pkahill: Hakuwa na betri na alikuwa akiwasubiri marafiki zake katika duka la Shoprite na akamwacha rafiki mmoja ndani na bomu ikalipuka

Aliongeza:

@ pkahill: Na twaziombea roho zote tulizozipoteza, nawatakia faraja wapendwa wao kwa matarajio kwamba jeraha la kuwapoteza ndugu zao litapona

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.