Wakati Papa Anajiuzulu, Warusi Wajiuzulu kwa Putin

Kama kila jamii inayatazama matukio kupitia lensi ya matokeo ya walichokichagua, basi kwa jamii ya Warusi Mtandaoni lensi ya uchaguzi wao ni siasa za ndani. Haikuja bila kutarajiwa, basi, kuwa habari za kujiuzulu kwa Papa Benedict XIV na kuachia wadhifa wake zimetafsiriwa kwa mtazamo huu na wanablogu wa ki-Rusi. Vilevile haikushangaza kuwa nyingi ya tafsiri hizi zilikuwa katika namna ya utani –zaidi ya yotem kata wa-Rusi washikao dini hawajawa na utetezi wowote. Pasipokutaka kujua matokeo ya kujiuzulu kwa Papa Benedict na atahri yake kwa imani ya Kikatoliki au tafsiri ya hatua hiyo kufuatia kashfa ya udhalilishaji iliyowakabili kwa watawa, RuNet walioweka habari hiyo kwenye safu za vichekesho.

Mwanablogu na mwandishi wa habari Ivan Davydov alilitazama suala hili kwa msimamo wa ustawi wa jamii [ru]:

В России из каждой третьей семьи папа ушел. И ничего, не шумит никто в прессе.

Nchini Urusi thelusi ya familia zimetelekezwa na baba zao [kwa ki-Rusi neno “papa” lina maana ya baba na Papa]. Hakuna, hakuna anayepiga kelele kwenye vyombo vya habari.

Shabiki wa siasa wa RuNet aitwaye Politrash alichambua [ru] kukua kwa mashinikizo Kaskazini mwa Caucasus:

Бенедикт XVI: “Руководство футбольного клуба “Анжи” сделало мне предложение, от которого я не мог отказаться”.

Benedict XVI: “Uongozi wa timu ya kandanda iitwayo “Anzhi” umenipa ofa ambayo nisingeweza kuikataa.

FC Anzhi ni timu iliyopo Makhachkala, Jamhuri ya Dagestan, na inamilikiwa na bilionea wa ki-Rusi Suleyman Kerimov, ambaye tangu mwaka 2011 amekuwa akitumia mapesa yake kuwanunua wachezaji wazuri kutoka kwenye timu za Ulaya kama FC Milan.

While Benedict XVI is retiring, President Putin still has some juice left. Pope Benedict in Poland, October 17, 2010. © Kancelaria Prezydenta RP. GNU Licence. Vladimir Putin in Tuva, August 13, 2007. © www.kremlin.ru

Wakati Papa Benedict XVI anajiuzulu, Rais Putin bado anang'ang'ania. Papa Benedict nchini Poland, Oktoba 17, 2010. © Kancelaria Prezydenta RP. Bima ya GNU. Vladimir Putin mjini Tuva, Agosti 13, 2007. © www.kremlin.ru CC 3.0

Wanablogu wengi, hata hivyo, walizungumzia zaidi kuhusu Vladimir Putin. Kuna ufanano wa moja kwa moja kwa ubabe na uongozi wa kibavu wa Putin na Papa. Wote wawili wanaendesha taasisi kwa “amri za kutoka juu”, ingawa mtawala mmoja wa Urusi  [ru] anayesemekana kuwa aliwahi kutofautiana na Papa? Makundi mangapi anayo?”

Ksenia Sobchak alihitimisha maoni ya jumla katika twiti hii [ru], akizungumzia namna katiba ilivyotumika kuhalalisha awamu ya tatu ya Putin:

Даже папа ушел.Сам.В теократическом гос-ве Ватикан принцип сменяемости власти работает лучше чем в стране “суверенной демократии”…

Hata Papa ameamua kuondoka. Kwa hiari. Katika nchi ya kidini ya Vatican kanuni za kuachiana madaraka zinafanya kazi vizuri kuliko kwenye nchi ya “demokrasia ya kujitegemea” …

Anwani feki ya twita ya Rossneft rais wa gor Sechin ilionyesha [ru] kuwa Papa huenda alikuwa na mambo mengine ya ndani yaliyomfanya ajiuzulu:

Папа Римский Бенедикт XVI весело троллит Путина

Papa wa Rome Benedict XVI anataka kumkasirisha Putin aone atafanyaje

Anuani feki ya Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi ilijibu [ru] wito huo wa Papa kwa Putin, ikiwa na nukuu ya mwandishi wa habari wa Putin:

“Не дождетесь!” – кратко прокомментировал Дмитрий Песков последние новости из Ватикана.

“Haiwezekani hata kidogo!” – Dmitry Peskov alijibu kwa haraka habari hizo kutoka Vatican.

Mchekeshaji anayetumia jina la KermlinRussia hakuiiacha fursa hiyo ipite, naye akatwiti [ru]:

П. отрекся от престола.

Putin amegoma.

Wakati utani huu ulisambazwa na watu zaidi ya 146, haukuvunja rekodi ya @fuckdaoutlaws, ambaye ujumbe wake ulitumwa na watu zaidi 254 kusambaza habari hizo na kuifikisha mahali pake twiti [ru] hiyo iliyoweza kugeuka utani wa uzoefu wa kiuongozi wa Waziri wa sasa wa Ulinzi Sergei Shoigu(aliyewahi kushika nyadhifa nyingine jeshini pamoja na kuongoza kamati ya bunge ya Mambo ya Dharura), ambayo ilionyesha wasiwasi kuhusu hatma ya uongozi wa Urusi (Shoigu, mwenye kupenda sifa kwenye vyombo vya habari, mara nyingi hutajwa kama mmoja wapo ya watu wanaoweza kumrithi Putin):

временно исполняющим обязанности Папы Римского назначен Сергей Шойгу

Sergei Shoigu, kwa sasa, amechaguliwa kuwa kaimu Papa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.