- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hali ya Hatari kwa Watoto nchini Syria: Namna Utakavyo Saidia.

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Syria, Haki za Binadamu, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Wakimbizi

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusiana na maandamano nchini Syria 2011/13 [1]

Madhara ya Vita kwa Watoto wa Syria:

Inakadiriwa kuwa, watoto wa Syria 4,355 wamekwishakuuawa (hadi tarehe 15/1/2013) katika mgogoro unaoendelea nchini Syria, hii ni kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na hifadhi ya Mapinduzi ya Syria ya Martyrs [2]. Maelfu ya watoto wameshajeruhiwa, kushikiliwa, au kuachwa bila ya ndugu, au pia kutokupata msaada wa kimatibabu na pia misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi za Umoja wa Mataifa [3] (UNHCR), wakimbizi takribani 650,764 kutoka Syria wanaandikishwa au wanasubiri kuandikishwa ndani na nje ya Syria. Zaidi ya nusu yao (asilimia 52) ni wenye umri chini ya miaka 18. Hata hivyo, idadi kubwa ya watoto nchini wamekuwa wakikabiliana na maumivu makali ya kupoteza makazi yao, mali zao na wazazi wao. Tovuti ya Haki za Binadamu inataarifu [4]:

[5]

watoto wa Syria katika mahangaiko, mbali na vita, pia wanakabiliana na baridi. Chanzo: Wasaidie Watoto [5]

kiuhalisia, katika mazingira haya, mahitaji yote muhimu kwa ukuaji wa watoto yameharibiwa, , and the psychological damages of armed conflicts are incalculable…. waototo hawa, wanaoshindwa kukua katika mazingira mazuri na badala yake wanakabiliana na matukio ya ukatili wakiwa na umri mdogo kabisa, mara nyingi wanajijengeaa dhana ya kwamba vurugu ni njia kama zilivyonjia njia nyingine za kutatua migogoro, na kwa hiyo inakuwa vigumu sana kwao kutuma ujumbe wa amani na ulinzi wa kimataifa kwa vizazi vijavyo.

 

 

Watoto wa Syria wasaidiweje?

Mapema wiki hii, tulitoa taarifa [6] kuhusiana na hali ngumu wanayokabiliana nayo watoto wa Syria kuhusiana na vita hii inayoisambaratisha nchi yao vipande vipande. Leo tunaangalia njia ambazo watu wangeweza kuzitumia ili kuondoa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa Syria.

Kwa namna utakavyofanya, unaweza kuonesha namna unavyoguswa na madhila wanayoyapata watoto wa Syria, na unaweza pia ukapaza sauti yako ili Umoja wa Mataifa utimize wajibu wake katika kulinda haki za watoto wa Syria wanaodhalilishwa nchini mwao. Onesha mshikamano wako pamoja na watoto wa Syria kwa:

Harakati maalum kwa ajili ya kuujulisha umma kuhusiana na makosa dhidi ya ubinadamu ulimwenguni kote pamoja na kusaidia kuyakomesha, kwa kuanzia na matukio ya kikatili yanayowapata watoto nchini Syria.

 

Video inayofuata [Tahadhari: Picha, zinaonesha watoto waliofariki] inawakilisha hali halisi ya Watoto wa Syria iliyoandaliwa na mpango wa Kupinga Unyanyasaji dhidi ya Binadamu, yaani Rise 4 Humanity.

Shirika la “Saidia Watoto (Save the Children) lilizindua kampeni ya kusitisha ukatili dhidi ya watoto nchini Syria. Muitikio ulikuwa wa kiwango kisichoelezeka– uliopelekea ulimwengu wote kutupia macho matukio ya kikatili wanayoyapitia watoto nchini Syria. Hii ilikuwa ni kampeni yetu iliyokuwa na kasi kubwa kabisa kuliko nyingine yoyote ambapo, maelfu ya watu walikuwa wakijiunga kila siku.

[13]

Tangazo la Hali ya Hatari ya baridi kwa Watoto wa Syria liliowekwa na UNICEF mnano mwezi Desemba 2012 katika njia ya treni ya chini kwa chini jijini London. Chanzo: Tafiti ya dunia (Global Research) [13]

Weka Saini katika hati za Malalamiko Dhidi ya Serikali:

Saidia kwa kutuma tovuti hizi pamoja na hati za malalamiko kwa rafiki zako na kwa viongozi wako. Wanaweza kufanya mambo makubwa. Unaweza kufanya mambo makubwa.

[26]

Mgogoro wa Syria unawadhuru watoto milioni 2. Tunahitaji mchango wako ili tumfikie kila mmoja. Chanzo: UNICEF España [26] katika ukurasa wa Twitter.

Jumuia za Ndani Zinazowasaidia Watoto wa Syria:

Video inayofuata, (wakiwa nje kwenye baridi: Familia za wakimbizi wa Syria wakikabiliana na baridi), imetumwa na savethechildrenuk [30] ili kuelezea hitaji la watoto na harambee ya kuwasaidia watoto wa Syria ambao ni waakimbizi:

Watoto wa Syria ni wahanga wasio na hatia wa vita hii na kutoa msisitizo kwa wakati mgumu wanaoupitia na ujaribu kusaidia kuwaepusha na mateso wanayoyapa kwa kadiri ya utakavyoweza.

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusiana na maandamano nchini Syria 2011/13 [1]