- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Bulgaria: Gharama Kubwa za Nishati Zasababisha Maandamano

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Bulgaria, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara, Utawala

Siku ya Jumapili, Februari 17, makumi ya maelfu ya ya watu katika mji mkuu wa Sofia pamoja na majiji mengine nchini Bulgaria waliendelea kuandamana ili kupinga gharama kubwa za umeme pamoja na za joto pamoja na kupinga ukiritimba wa makampuni ya usambazaji wa nishati [1]ChCEZ [2], EVN [3],naEnergo-Pro [4]. Waandamanaji wanataka makampuni matatu nchini Bulgaria ambayo ni CEZ, EVN na Energo-Pro yataifishwe na shirika la Shirika la Taifa la Umeme. NEK [5].

Zaidi ya watu 20,000 walijitokeza huko Varna kwa ajili ya kuandamana, watu 10,000 huko Plovdiv, 6,000 huko Sofia na watu 5,000 huko Blagoevgrad. Watu wanne walishikiliwa pale waandamanaji katikati ya jiji la Sofia walipokabiliana na polisi walipofurika jijini Sofia kujaribu kuzuia waandamanaji waliokuwa wanaelekea makao makuu ya Shirika la Nishati la Umma la CEZ.

Waandamanaji wanataka wiki ijayo madai yao yawe yameshasikilizwa- na kama haitakuwa hivyo, wanamtaka Waziri Mkuu na Rais wajiuzulu. Pamoja na kuwa vyama vya kizalendo vinajaribu kupata faida ya kisiasa, waandamanaji wamepinga vikali dhidi ya upotoshaji huo kwa kusema kwa sauti kuu, “Hakuna vyama!”

Mtumiaji wa YouTube, Iasssen alipakia video hii [6] ya maandamano ya Sofia (iliyochukuliwa na SkyMedia-bg.com kutokea angani kwa kutumia helikopta, sauti ikiwa imenaswa tofauti kutokea ardhini). Video nyingine ya ubora wa hali ya juu (HD) iliyochukuliwa wakati wa maandamano ya Sofia ilipakiwa na mtumiaji wa Youtube MickeyMouseFrance:

Mwanablogu wa Bulgaria Kostadin Kostadinov alipakia taarifa iliyokuwa na kichwa cha habariposted an entry titled “Uelekeo utakuwa upi mara baada ya uasi?” [7][bg]:

Takribani watu100,000 waliandamana leo katika maeneo mbalimbali ya nchi. Maandamano hayo, yaliyoanzaThe protests, which began as a reaction against the pompous arrogant and brusque bills, yalibadilika na kuwa ya kijamii na kisiasa zaidi. Watu waliimba kwa kurudiarudia “Boyko [Boyko Borisov [8], Waziri Mkuu wa Bulgaria] atoke” na “pamoja na [GERB [9], chama tawala],” na waone ni nani ambaye angewafuata. […] Watu 100,000, wengi wao wakiwa ni vijana wadogo, wangefanya nini kwenye chaguzi katika kipindi hiki cha kiangazi ni jambo la msingi sana. Bila mashaka yoyote, wana wajibu mkubwa wa kuiamsha Bulgaria iliyolala na kuwafanya watu wa Bulgaria wajiamini na kuibadilisha nchi yao. Kwa upande mwingine, hawamuamini mtu yeyote, na wana sababu maalum.

Mwanablogu wa Bulgaria, Sabina Panayotova alionesha kukosa tumaini kabisa [10] kuhusiana na maandamano ya Februari 17 [bg]:

Watu hawa si watu wale.
– Watu wa wakati wa[majira ya joto mwaka 2012 [11] wealioandamana huko Eagle Bridge [12]] siyo hawa wa leo. Watu wa leo wamekuwa na huzuni, waliokata tamaa na wanyonge.
– Maandamano ya leo yamekuwa kama [maandamano ya mwaka 1989 ya kupinga ukomunisti], tofauti ni kuwa, baadae inaonekana kutakuwa na uwezekano wa kuwarudisha wakomunisti madarakani.
– Matokeo ya maandamano haya hayatakuwa mazuri. Kwa kufafanua vizuri zaidi, hali itaendelea kuwa kama awali.

Blogu ya Taralezh (“Nungunungu”) ilitoa maoni [13] kuhusiana na chama tawala na wizara kushindwa kutoa matamko yoyote:

Wakubwa wa nchi wanayakwepa maandamano pamoja na kutokuwajali watu. Wakati mamia ya maelfu ya watu wakipita katika mitaa ya majiji 35 nchini kote huku wakiimba kwa sauti kubwa, haluna hata kiongozi mmoja anayefikiria kurudi Sofia na kusimama mbele ya wananchi kama viongozi halisi.

Blogu ya D-r Beloliki ilipakia mkusanyiko wa picha [14] za maandamano ya tarehe 17 Februari yaliyofanyika karibu nchini kote Bulgaria. Dimi Lazhov alipakia picha [15] kutoka jiji la kaskazinimagharibi la Vratza lililopo kaskazinimagharibi ambapo watu wanaandamana kupinga ukiritimba pamoja na from the northwestern city of where people protesting against the monopoly and the new “rain tax.” Ukurasa wa Facebook wenye jina Saprotiva (“Ukinzani”) umekusanya picha za maandamano ya nchi nzima [16] na pia, kuna mkusanyiko wa habari na maoni here [17].

Mwandishi wa habari wa Bulgaria, Adelina Martini alitwiti [18]:

Maelfu ya maandamano katika majiji mbalimbali nchini Bulgaria kupinga bei kubwa za nishati ya umeme, watamka kwa sauti kubwa, “mafia” na “kujiuzulu” vyombo vya habari nchini Bulgsria vinataarifu.

Mwandishi mwingije wa habari wa Bulgaria, Mariya Petkova, ambaye makazi yake ni Cairo, alitwiti [19] pia kuhusiana na maandamano haya:

Mamia ya maelfu ya watu wanaandamana nchini kote Bulgaria kupinga ukiritimba wa makampuni binafsi kuhusiana na huduma muhimu za jamii pamoja na hali ngumu ya kiuchumi!!!