Februari, 2013

Habari kutoka Februari, 2013

Vurugu Zinazofadhiliwa na Serikali Nchini Angola

Mwanablogu Claudio Silva anaandika kwenye makala yake Africa Ni Nchi kwamba mtazamo wa kina juu ya vurugu zinazofadhiliwa na serikali (kufukuzwa watu mijini na kupigwa kwa waandamanaji) unahitajika ili kuelewa video mbili zilizosambaa sana mtandaoni na kuleta sintofahamu kubwa nchini (tazama habari maalumu za Global Voices). Anaandika “vurugu za Angola...

Udhaifu wa Watawala wa Afrika unajionesha Mali?

Ousmane Gueye katika tovuti ya Mondoblog anaandika [fr] kuhusu kuchelewa kupeleka vikosi vya kijeshi kasikazini mwa Mali: Kama tungekuwa tunasaiili matokeo ya watu wenye amani na huru kuingilia kati hali ya mambo nchini Mali, basi ni wazi kuwa kwa kuchelewa kupeleka vikosi vya ulinzi, nchi za Afrika zimewakosea wananchi wa Mali...

PICHA: Maandamano ya Pamoja ya Watu wa Shia Nchini kote Pakistan Yamalizika Kwa Amani.

  12 Februari 2013

Baada ya milipuko ya mabomu huko Quetta kuua zaidi ya watu 100, maanadamano ya watu wa jamii ya Hazara ya Shia yalisambaa kama moto katika maeneo mbalimbali ya Pakistani. Watu kutoka katika makundi makuu ya dini na makabila mbalimbali waliungana kwa pamoja na watu wa Hazara wakiimba kwa kurudiarudia#Sisi sote ni watu wa Hazara. Maandamano ya kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao yalianzishwa katika zaidi ya majiji 100 na miji.

Blogu 10 Bora za Mapishi ya ki-Afrika

  11 Februari 2013

MyWeku anatengeneza orodha ya Blogu 10 bora za Mapishiya ki- Afrika kwa mwaka 2013: “Inaonekana kuna blogu milioni moja zinazozungumzia mapishi, lakini ni chache sana zinazoonyesha vyakula vya Kiafrika. Pamoja na hayo imekuwa kazi ngumu kuchagua 10 kati ya nyingi nzuri kwa mwaka huu 2013.”