Wafalme Watatu Watembelea New York

Wafalme watatu walikuja na kuondoka, lakini siyo kabla ya kupita katika jiji la New York ili kusherehekea na mamia ya watoto waliojitokeza kwa ajili ya gwaride lililoandaliwa na Museo del Barrio siku ya tarehe 4 Januari, Ijumaa ya kipekee yenye jua kali katika mwezi huu. Shamra shamra hizi za Noeli, ambazo historia na chimbuko lake bado ni utata mkubwa (kama tu ilivyo kwa Ukristo), kwa karne nyingi, zimekuwa ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Amerika wenye asili ya Karibeani na Walatini.

Kwa mfano, nchini Puerto Rico, katika mkesha kuamkia siku ya ziara ya Wafalme Watatu, watoto huacha bilauri katika kisanduku kidogo kwa ajili ya farasi wa Melchor, Gaspar, na Baltasar, wakiwashukuru kwa ajili ya zawadi watakazozipokea siku inayofuata. Kiuhalisia ni kuwa, kwa miaka sasa, utamaduni huu umebadilishwa kwa namna ya ubunifu wa kipekee kabisa. Ilivyo sasa, wafalme wanawasili wakiwa wamepanda farasi na sio ngamia na wakisherehekewa kwa promises [es] zilizochongwa na santeros (wataalamu wa kuandaa sanamu za kidini) ambazo ni chanzo cha mvuto wa pekee na furaha.

Bila ya mashaka, jamii ya watu wa Amerika ya Puerto Rico na Walatini halisi walio na msisimko katika mji huo mkuu, ambao ni New York, hawajawahi kuacha kusherehekea siku hii kwa mshawasha mkubwa, na hususani kwa watoto. Miji ya Harlem ya Mashariki iligubikwa na hamasa kubwa ya kuona gari la matairi manne linalokokotwa na farasi likipita, mamajusi watatu wakiwa juu ya magongo, ngoma za watu wa Peru, capoeira, vikaragosi vikubwa mithili ya watu, na pia ngamia wawili wanaofugwa katika sehemu maalumu ya kufugia wanyama wasiohitajika tena huko New Jersey.

Tumeweka mfululizo wa picha zilizopigwa na msanii wa Puerto Rico Josué Guarionex zinazoonesha baadhi ya nyuso alizoweza kuzipata wakati wa shamra shamra hizo zilizokuwa na kelele nyingi.

Jesús "Papoleto" Melendez, poeta nacido y criado en El Barrio, fue elegido como rey emerito de la parada.

Jesús “Papoleto” Melendez, mshairi aliyezaliwa na kukulia Harlem ya Mashariki alichaguliwa kuwa mfalme wa heshima katika matembezi hayo.

Los danzantes de música tradicional peruana.

wacheza ngoma wakicheza muziki wa kijadi wa Peru.

Osvaldo Gómez nos deleitó con su hermosa presencia.

Osvaldo Gómez alitufurahisha sana kwa muonekano wake wa kuvutia sana.

Casi podemos sentir la energía de esta banda en esta foto.

Kwa hakika, kwa kuitazama picha hii, tunaweza kuhisi hamasa iliyopo katika kundi hili la waimbaji.

Cientos de niñas y niños desfilaron con sus coronas de papel desde la calle 106 hasta la calle 116 y la avenida Park.

Mamia ya wavulana kwa wasichana wakiwa na mataji yao ya makaratasi kuanzia mtaa wa 106 hadi 116 pamoja na mtaa wa Park.

La destacada reportera María Hinojosa, así como la activista Angie Rivera, fueron elegidas como las reinas magas para esta ocasión.

Mwandishi wa habari maarufu, María Hinojosa, na mwanaharakati, Angie Rivera, waliteuliwa kuwa kama Malkia katika tukio hili.

Fátima Shama, comisionada de la Oficina de Asuntos del Inmigrante de la ciudad de Nueva York, fue elegida como una de las reinas magas.

Fátima Shama, ambaye ni Kamishna wa Ofisi ya Mambo ya Uhamiaji jiji New York, pia alichaguliwa kuwa miongoni mwa Malkia.

anya Torres, artista puertorriqueña radicada en El Barrio, fue una de las madrinas de la parada junto a Nadema Agard, Cecilia Gastón, Christine Licata y Sandra Morales-De León.

Tanya Torres, ambaye ni msanii wa Puerto Rico aishiye Harlem ya Mashariki alikuwa ni miongoni mwa mama wa ubatizo katika kusanyiko hilo, Nadema Agard, Cecilia Gastón, Christine Licata and Sandra Morales-De León.

Caminar en las calles de Nueva York junto a tantos niños es un tremendo regalo.

Kutembea na idadi kubwa ya watu katika mitaa ya New York ni zawadi kubwa sana.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.