- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mauritania:Ghadhabu Dhidi ya Kauli ya Balozi wa Marekani

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Marekani, Mauritania, Maandamano, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vijana, Vyombo na Uandishi wa Habari

[1]

Picha ya maandamano dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Nouakchott – Iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook ya Vijana wa Kukusanya Nguvu ya Kidemokrasia

Mnamo Januari 23 [1],  kikundi cha upinzani “Vijana wa Kukusanya Nguvu ya Kidemokrasia”  (Jeunesse RFD), kilianzisha maandamano dhidi ya Ubalozi wa Marekeni mjini Nouakchott. Mapema, Oktoba 2012, Jo Ellen Powell, Balozi wa Marekani nchini Mauritania aliyeombea kushindwa [2] kwa upinzani, akiwafananisha wanachama wake na “paka”. Mwanadiplomasia huyo wa kimarekani alionyesha kuwa mkuu wa chama cha RFD Ahmed Ould Daddah anafikiri yeye ni uzao sahihi au mrithi halali baada ya utawala wa kaka yake, rais wa zamani Moktar Ould Daddah [3]. Matamshi hayo yameweka hadharani katika Vuguvugu la tarehe 25 Februari. Ukurasa wa YouTube [4] na ilichochea mtafaruku katika vyombo vya habari vya Mauritania [5] [ar].

Kwenye Ukurasa wa facebook, chama cha RFD kililaani kauli [6] ya Balozi wa Marekani:

اطلعنا في المنظمة الوطنية لشباب تكتل القوى الديمقراطية خلال الأيام الماضية على تسجيل صوتي نشرته حركة 25 فبراير، يحتوي على تصريحات للسفيرة الأمريكية في موريتانيا تساند خلالها النظام العسكري الجاثم على صدور أبناء شعبنا وتسخر فيه من منسقية ومؤسسة المعارضة الديمقراطيتين و تسيء لزعيم المعارضة الرئيس أحمد ولد داداه إساءة صريحة

 

Sisi vijana wa RFD, tumesikia kauli ya Balozi wa Marekani nchini Mauritania, iliyotolewa katika Vuguvugu la Februari 25 ambapo alionekana kuunga mkono Utawala wa Kijeshi unaowanyanyasa watu wetu na kukejeli upinzani huku kumshambulia waziwazi kiongozi wetu Ahmed Ould Dadah.