- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ni Sikukuu ya Kuzaliwa Kristo (Noeli) Mjini Betlehemu

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Palestina, Dini, Uandishi wa Habari za Kiraia

Ni sikukuu ya kuzaliwa Kristo mjini Betlehemu [1], katika ukanda wa Magharibi, Palestina, mahali alipozaliwa Kristo. Ni namna ipi nzuri zaidi ya kusherehekea tukio hili kwa kuwashirikisha picha pamoja na mitazamo ya watumiaji wa intaneti kuhusiana na tukio hili linalosherehekewa na mabilioni ya watu duniani kote.

Mwanahabari wa Israeli Joseph Dana alikuwa Betlehemu kuangalia mwanga wa miti ya Krismasi na alipakia mtandaoni picha ifuatayo:

The lighting of the Xmas tree in Bethlehem [2]

Mwanga wa mti wa Krismasi mjini Betlehemu. Picha iliwekwa na @ibnezra [2] katika mtandao wa Twita

Lauren Bohn aweka picha ya mti wa Krismasi aliyopigwa kwa ukaribu zaidi wakati wa sherehe hizi:

Beautiful Christmas tree lighting in Bethlehem [3]

Mwanga mzuri wa mti wa Krismasi mjini Betlehemu, maoni @LaurenBohn [3] katika Twita, wakati akiweka mtandaoni picha hii

Na Maath Musleh aweka mtandaoni picha zinavyoonesha jinsi mitaa ya Bethlehemu ilivyoangazwa katika maandalizi ya sikuu ya kuzaliwa Kristo:

Bethlehem streets lighting up for Christmas [4]

Mitaa ya Betlehemu inavyoangazwa kwa mwanga wa taa za Krismasi, anatwiti @MaathMusleh [4], ambaye aliweka picha hii katika mtandao wa Twita

Ahmed Aggour, mchana wa leo aliweka picha hii ya mti:

[5]

Mti mzuri wa Krismasi kuliko mwingine wowote ule unaopatikana mjini Betlehemu. Heri ya sikukuu ya kuzaliwa Kristo. #Betlehemu #Palestina, alitwiti @Psypherize [5]

Naye Daniel Aqleh aliweka mtandaoni video hii [6] katika mtandao wa YouTube kuhusiana na sherehe ya kuwasha mti wa Krismasi iliyoambatana na kulipuliwa kwa fataki:

Heri ya Sikukuu ya Noeli kusherehekea Kuzaliwa kwa Kristo!