- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kenya: Kufundisha Uvumilivu wa Kikabila Kupitia Hadithi za Sayansi

Mada za Habari: Uandishi wa Habari za Kiraia

Watoto wa Kenya wanafundishwa uvumilivu wa kikabila kupitia hadithi za sayansi [1]: “Kushambuliwa kwa akina Shida:Bunduki za AKA Zaokoa Sayariā€¯ ni hadithi inayozungumzia maisha ya jamii tatu zilizoishi katika jangwa katika mji fulani ambazo zilitegemea kisima kupata maji. Lakini wenyeji wanatishika pale wanapogundua kuwa maji wanayoyategemea yanamwagwa kimiujiza usiku.”

“Watoto watatu katika mji huo wanagundua kuwa wanazo nguvu maalumu kwa kuwa waneweza kuwaona na kuwasikia wezi wa maji wasioonekana uwezo unaosababisha matatizo mengine mengi katika jamii hizo tatu. Bado hata hivyo hakuna anayeamini wanachokisema watoto hao, kwa sababu watoto hao watatu pekeyao wanazo nguvu maalumu za usawa na uvumilivu zinaowawezesha kuona kile ambacho jamii zao haziwezi kukiona. Je, watoto hawa wanaweza kuwazuia wavamizi kabla vita haijalipuka mjini?”