Habari kutoka 30 Novemba 2012
Mkanganyiko wa Makubaliano ya OIC Kuanzisha Ofisi Nchini Myanmar
Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) limependekeza kuanzisha ofisi nchini Myanmar kwa lengo la kukisaidia kikundi kidogo cha Waislamu nchini humo. Serikali ilishakubaliana na mpango huu lakini ilibadili uamuzi huu mara baada ya kutokea maandamano ya kupinga uamuzi huo katika maeneo mengi ya nchi.
Mwanzilishi wa Kikundi cha Kijeshi Kilichofutwa Nchini Pakistani Ajitolea Kuisaidia Marekani.
Wakati kukiwa na makelele na uharibifu mkubwa huko ukanda wa pwani ya mashariki mwa Marekani unaotokana na kimbunga kikubwa kijulikanacho kwa jina la Sandy, Hafiz Mohammad Saeed, mwanzilishi wa shirika la kijeshi lililofutwa la Lashkar e Taiba (LeT) na kiongozi wa Jaamat ud Dawa (JuD) ajitolea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Marekani ili kufidia uharibifu.