Uganda Yaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru

Uganda@50 Logo. Image source: Uganda@50 Facebook page.

Nembo Rasmi ya Sherehe za Uganda kufikisha miaka 50 ikiwa huru. Chanzo cha picha: Ukurasa wa Facebook wa Uganda@50.

Mnamo Jumanne ya Oktoba 9, 1962, Uganda ilijitwalia uhuru wake wakati bendera ya Uingereza iliposhushwa, na bendera ya Uganda kupandishwa wakati huo wa-Ganda wenye furaha na matumaini mapya wakiimba Wimbo wa Taifa la Uganda.

Tarehe 9 Oktoba, 2012, Uganda ilitimiza miaka 50 ya dhahabu ya tukio hilo la kihistoria. Shughuli nyingi zimefanyika katika nchi hiyo kusherehekea siku hii maalumu, ambayo ilianza kwa onyesho la Kampala siku ya Jumapili Oktoba 7. Watu wengi wengi walimiminika katika uwanja wa ndege wa Kololo kusherehekea miaka 50 ya uhuru.

Uganda imewahi kuwa namarais nane tangu uhuru, kwa majina, Mfalme Edward Muteesa II, Apollo Milton Obote, Idi Amin Dada, Yusuf kironde Lule, Godfrey Lukongwa Binayiisa, Paulo Muwanga, Tito Okello Lutwa, na rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni.

Nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto za huduma za afya, elimu, uhuru wa habari na nyinginezo nyingi.

Kwa ujumla hata hivyo, wa-Ganda wanaonekana kuwa na furaha kwa miaka 50 ya uhuru, na wana matarajio makubwa kwa miaka mingine 50, kama wanavyosema
Yoga Yoga Uganda (jina la wimbo rasmi wa sherehe hizo, wenye maana ya hongera sana katika lugha ya Luganda)

Wa-Ganda wengine, hata hivyo, wanadhani maadhimisho hayo ni upotevu wa rasilimali za nchi ambayo mpaka sasa wapo watu wanalala njaa.

Wa-Ganda mtandaoni wamekuwa wakijadili maadhimisho hayo kwenye mitandao ya kijamii kama twita na Facebook.


Twita

Wakati wa tukio lenyewe, kulikuwa na maonyesho ya ndege za kivita za nchi hiyo. NOrman Anguzu alitwiti picha ya ndege hizo zikiwa angani:

@normzo#UgandaAt50 Picha nzuri kutoka kwenye “Kumbukumbu za Mzungu” #Ugandapic.twitter.com/IJ25bPUw

Lucy Smize akitwiti kuhusu rangi za bendera ya Uganda na maana zake:

@Lucy_smize: Nyeusi, Njano, Nyekundu: Watu, Mwanga wa jua, Undungu.#UgandaAt50

Patricia Kahill anawatakia wa-Ganda siku njema ya uhuru, lakini aligusia kero ya mgao wa umeme, unaofanywa na kampuni ya kusambaza umeme wa maji iitwayo Umeme:

@pkahill: Heri ya siku ya uhuru mkiwa gizani  #fumemeug@50 #ILoveUgBecause more

Rosebell Kagumire anasema kwamba pamoja na Uganda kusherekea miaka 50 ya uhuru, nchi hiyo haijaonyesha dalili zozote za kukomaa:

@rosebellk: Unasherehekea miaka 50 ya uhuru na kimsingi hakuna dalili za kukua kwa namna yoyote! Huwezi kusimama mwenyewe, utakuaje? #Ugandaat50

Angelo Izama anaamini Uganda bado ni moja ya nchi nzuri zaidi duniani:

@opiaiya:  Bado ni mojawapo ya nchi nzuri zaidi duniani  #Uganda@50

Vanessa anazo pongezi nyingi kwa sherehe hizo:

@v_sees_you: Hongera sana Uganda! Miaka 50 ya uhuru! Mungu aendelee kulibariki taifa letu!

Timothy Kalyegira anatwiti kuhusu Ukurasa wa nyumbani wa Google:

@timkalyegira: Hata Google inashiriki matangazo ya sherehe za miaka 50, kwa kuwa na maonjo ya ki-Ganda katika ukurasa wake wa kufungulia. (Lakini kiungo cha intanenti kimetowekakatika ofisi ya Google ya Kampeni!)

Google Uganda Homepage

Ukurasa wa nyumbani wa Google Uganda

Maxentia anatoa maoni kuhusu rangi alizovaa leo:

@maxen1987: ilivyo, nilivaa rangi za bendera ya taifa; nyeusi, njano nyekundu kuithamini siku hii ya #Ugandakufikia miaka 50. Inanifanya nijisikie vizuri

Happy Betty anaamini amebarikiwa kuishuhudia Uganda ikitimiza miaka 50 ya uhuru:

Happy Betty: Najisikia kubarikiwa kuwa hai wakati huu Uganda inapotimiza miaka 50 sina hakika kama nitaendelea kuwepo wakati huo itakapofikia miaka 100 bali kwa kizazi changu… wazee wetu wametufikisha hapa tulipo leo, ni zamu yetu kuipeleka Uganda kuelekea miaka mingine 50 tukijua vyema tunakoelekea -Mungu yu pamoja!

Facebook

Edwinsmith Kigozi anasema:

anajisikia vizuri sana kuwaona wa-Ganda wakija pamoja kusherekea miaka 50 ya kuwa wa-Ganda wasiotafuta chama tofauti cha siasa bali kama wa-Ganda. Tusonge mbele wa-Ganda. Kwa Mungu na nchi yangu.

Akampa Ivan anajisikia maonyesho ya ndege za kivita haikuwa chaguo zuri ambalo wa-Ganda wangelihitaji:

Mtu angenipa jiwe zuri niitungue moja ya zile ndege ambazo zimekuwa zikiharibu hali ya hewa ya Kampala kwa makelele na moshi. Ninajiuliza ikiwa Serikali inakosa kitengo bora za manunuzi kununua ndege za kisasa kiteknolojia na sio haya madege ya kizamani au ndio kusema Uganda inakosa watu waliobobea katika masuala ya ndege za aina hii. Nimekatishwa tamaa sana. Hata baiskeli ikiendeshwa vizuri ingeenda kasi kuliko madege haya. Haidhuru ni sherehe za Uganda kutimiza miaka 50, na ninajivunia kuwa m-Ganda. Heri ya kutimiza miaka 50 ya Dhahabu!!! Tusherehekee.

Shy V Okecho anabainisha kwamba wakati Uganda inaendelea kukua, kila kitu kinaendelea kuzeeka sambamba nayo, akirejea barabara mbovu zisizofanyiwa marekebisho, shule na mahospitali:

Naye Uganda@50 ga ekuuze eguudo zikuuze,amaddwaliro gakuuze amadagala tegalimu, ba M.P's bafuuna eguuzi ya 200,000 okuyeesa budget. Naye UGANDA ensi yenge!!

Lakini katika miaka 50 ya uhuru kadri tunavyokua, barabara nazo zimekua na kuzeeka, Hospitali zimekua bila dawa. Wabunge wanapata rushwa ya USH 200,000 kupitisha bujeti. Lakini pamoja nahayo yote, Uganda ni nchi yangu.

Evelyn Mirembe Nkuyahaga anasema:

Ohooo! Hii ni ajabu! Uganda imefikisha miaka 50! Ninaipenda nchi yangu na Rais wangu! Ululululu… Asante Yesu kwa Uganda!

2 maoni

  • Sherehe hizi za miaka 50 za uhuru wa Uganda zinafanyika wakati kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akiwa katika kifungo cha nyumbani na kuzuiwa kuhudhuria. Serikali imedai kwamba huenda kiongozi huyo akavuruga amani katika maadhimisho hayo. Hata hivyo awali Besigye alinukuliwa akisema kuwa kamwe hawezi kuhudhuria sherehe hizo kwa kuwa hakuna chochote alichokiona katika miaka hayo hamsini ila ni mateso na ukandamizaji wa upinzani unaofanywa na serikali ya Museveni.

  • It’s genuinely very difficult in this full of activity life to listen news on TV, thus I simply use internet
    for that reason, and obtain the latest information.

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> mercadeo internet

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.