- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, Kameruni, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari, Matangazo
Highway Africa Award for Global Voices

Washindi: Dorothee Danedjo kutoka Kameruni akiwa na Ndesanjo Macha wa Global Voices. Picha ya Ettione Ferreira [1] (imetumiwa kwa ruhusa)


Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara [2] imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa [3] katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha [4] alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba, 2012 kwa niaba ya timu nzima. Mwanablogu na mwandishi wa habari Dorothy Dandejo [5] kutoka Kameruni alikuwa mshindani wa karibu aliyeibuka mshindi wa pili katika kundi hilo hilo.