Morocco: Wanafunzi Wadai Marekebisho kwenye Mfumo wa Elimu

 

Mwezi Julai, kundi la wanafunzi wa Morocco lilizindua ukurasa wa Facebook uitwao “Muungano wa Wanafunzi wa Morocco kubadili mfumo wa Elimu” (ufupi kwa Kifaransa: UECSE). Kundi hilo ni mkusanyiko wa vijana wa Morocco ambapo lengo lao ni “kuchukua hatua, na kujadili ufumbuzi madhubuti wa kukuza ubora wa mfumo wa elimu”.

Ndani ya muda usiotimia mwezi mmoja tayari ukurasa huo uliwavutia wanachama zaidi ya 10,000 na kupata uungwaji mkono kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Yaonekana jambo zima lilipata kasi zaidi kufuatia taarifa kwamba serikali ilikuwa na mipango ya kushupaza sera ya masomo katika vyuo vikuu vya umma.

Kikundi kiliitisha [Fr] maandamano ya nchi nzima mnano Jumapili Agosti 6, 2012, na “kuhamasisha asasi za kiraia na wasomi wanasiasa wa Morocco kuanzisha mjadala wa kitaifa juu ya hatua za kurekebisha mfumo.”

Wito huo ulisambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kupitia video ambayo kundi hilo liliituma kwenye YouTube kabla ya maandamano kufanyika, wanafunzi walitoa wito wa kufanyika mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu. “Mfumo mzima wa elimu unahitaji kubadilishwa,” mwanafunzi mmoja anasema mbele ya kamera. “Mfumo unahitaji kuvunjwa kabisa na kuundwa upya kutoka mwanzo,” anasema mwingine. Wengi wa wanafunzi wanaoonekana kwenye video pia wamekemea kile wanachokiona  kuwa “hatua zisizomotisha” zilizowekwa juu mno na Grandes Ecoles, hasa katika viwango vya kushindaniwa kupitia mitihani ya kujiunga na chuo.

Katika siku ya maandamano, mamia ya wanafunzi na wazazi wao waliitikia mwito wa kuandamana kama inavyoonyeshwa kupitia picha na video zilizochukuliwa na kisha kuwekwa mtandaoni.

Picha ya video ifuatayo ni kutoka katika maandamano yaliyofanyika katika jiji kubwa zaidi la nchini Morocco, Casablanca (zilizowekwa na The7Gladiator):

Picha zilizowekwa kwenye  mtandao wa Flickr na Hassan Ouazzani zinaonyesha utofauti mkubwa wa itikadi za kukemea rushwa, upendeleo, miundombinu duni na masharti magumu yanayowekwa dhidi ya wahitimu wa shahada ya kwanza wanaotaka kuendelea na elimu ya juu zaidi:

Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu – Picha  kwa niaba ya Hassan Qazzani – Imetumiwa kwa ruhusa

Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu – Picha imetumiwa kwa idhini kutoka kwa Hassan Quazzani

Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu – Picha imetumiwa kwa idhini kutoka kwa Hassan Quazzani

 

Maandamano yaliendelea kwa amani. Kundi hili liliahidi kuandaa migomo ya chini kwa chini na mikutano zaidi nchini kote.

Kwenye Tumblr, UECSE iliandika:

 

WANAFUNZI vijana wanaomba kuwepo kwa mfumo bora zaidi wa elimu kwa ajili yao wao kama WANAFUNZI WA MOROCCO, kwa kuwa wamechoshwa na hali ya sasa wana nia ya kubadili hali zao za baadaye (e) ili kutimiza ndoto za maishani mwao, wimbi lenye mshawasha motomoto lajionyesha wazi.

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.