Habari kutoka 28 Agosti 2012
Serikali ya Kolumbia Yapanga Kufanya Mazungumzo na Waasi wa FARC
Katika blogu ya Crónicas, Santos García Zapata anaeleza muktadha [es] kuhusu uamuzi wa Rais wa kuanzisha mazungumzo ya amani na makundi ya waasi. Kongresi ya ‘Kamisheni ya Amani’ imetangaza kwamba Rais Santos “hayupo peke yake” katika dhamira yake ya kupatikana kwa amani.
Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru
'Nilitishiwa kufanyiwa vitendo vya ngono na kutendewa vibaya mara kadhaa katika siku ile. Wakati mmoja hata na ofisa wa ngazi za juu wa #NISS.' Mwezi Juni, Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudani liliwakamata maelfu ikiwa ni pamoja na mwanaharakati anayetumia Twita Usamah Mohamed Ali.
Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM
Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.