Agosti, 2012

Habari kutoka Agosti, 2012

Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook

  30 Agosti 2012

Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa ni “kuonyesha ukweli kuhusu shule za umma”, Isadora anaweka picha zinazoonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika shule yake pamoja na...

Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM

Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.

Ufilipino: Mafuriko Yaathiri Vitongoji vya Jiji la Manila na Mikoa ya Karibu

  27 Agosti 2012

Mvua kubwa ilisababisha mafuriko katika vitongoji vingi ya jiji la Manila pamoja na majimbo ya jirani katika Kisiwa cha Luzon nchini Ufilipino. Mhariri wa Global Voices aliye huko Manila, Mong Palatino, anakusanya picha kutoka katika majukwaa mbalimbali ya habari za kiraia yanayoonyesha athari kubwa ya mafuriko hayo katika mji huo mkuu wa nchi.