Julai, 2012

Habari kutoka Julai, 2012

Angola: Raia Wadai Kampeni za Uchaguzi za Wazi

Asasi za kiraia nchini Angola zinatoa wito wa uwazi zaidi [pt] katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 agosti, 2012. Moja wapo ya miradi iliyozinduliwa hivi karibuni kwa lengo hilo ni maombi ya mtandaoni [pt] ikiwataka viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kushiriki midahalo ya moja kwa moja kupitia...

Ethiopia: Maandamano ya Waislamu Yashika Kasi

Jeshi la Polisi nchini Ethiopia waliamua kutumia nguvu kupambana na wanaharakati wa ki-Islamu, likituhumiwa kufanya vitendo haramu katika maeneo yanayochukuliwa kuwa matakatifu katika misikiti, kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na ukurasa wa kikundi cha waislam katika mtandao wa Facebook uitwao Dimtsachin Yisema (Iache Sauti Yetu Isikike). Tangu mwezi Mei, Wa-Islamu wa ki-Ethiopia wamekuwa wakiandamana kupinga serikali kuingilia mambo yao ya kidini.

Paraguai: Kutoka Kutumikishwa Hadi Kuwa Kiongozi Mzawa.

Sauti Chipukizi  21 Julai 2012

Kutana na Margarita Mbywangi, ambaye katika umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa na kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani. Tangu wakati huo amekuwa kiongozi muhimu wa kabila la Aché na hata kuwa Waziri katika nchi yake. Mbywangi sasa anasimulia maisha yake binafsi kupitia Mradi wa Rising Voices.

Hispania: Maandamano ya Wachimbaji Madini Yaungwa Mkono na Wananchi

  16 Julai 2012

Maelfu ya wananchi wa Uhispania wameungana na maandamano ya wachimbaji wa madini nchini humo, wakati waandamanaji hao walipowasili nchini Madrid baada ya kutembea kilometa 400 wakitokea kaskazini mwa nchi hiyo. Wachimbaji hao walishangazwa na kiwango cha hamasa kilichoonyeshwa, ambacho kiliongeza chachu ya kile ambacho sasa chaitwa 'usiku wa wachimbaji madini'