Senegali:Rais Wade Aandamwa Hata Baada ya Kukubali Kushindwa Uchaguzi

Wakati ulimwengu wa nje ya Senegali unaonekana kushabihiana katika kumwagia sifa kemkem rais wa Senegali anayeondoka Abdoulaye Wade pamoja na kupongeza demokrasia iliyochukua nafasi baada ya matokeo ya uchaguzi uliojidhihirisha kuwa wa amani mwezi Machi 2012, ulimwengu wa blogu nchini humo umekuwa mkosoaji mkubwa wa rekodi ya Rais Wade. Wanablogu hawaonekani kusahau athari na waathirika wa ghasia za kuelekea uchaguzi, kuingiliwa kwa uhuru wa habari na mifano mingine mingi ya utawala mbovu katika kipindi chote cha urais wa Wade tangu 2000-2012.

Abdoulaye Wade akiongea Mjini New York mwaka 2002. Picha ya Marcel Bieri wa Swiss Image. Iliwekwa kwenye habari za Mkutano wa Uchumi wa Dunia kwenye Flickr (CC-BY-SA-2.0)

Fabienne Fatou Diop anaandika kwamba Wade hakuwa na uchaguzi mwingine isipokuwa kukubali kushindwa na Waziri Mkuu wa zamani na mshindani wake Macky Sall katika posti yake “Senegali, tarehe 25 Machi 2012, Heshima kwa watu wetu!” [fr]:

Non, Abdoulaye Wade n’a pas été démocrate en téléphonant à Macky Sall. Il n’avait plus le choix. Nous lui avons imposé le choix le 23 juin, nous lui avons imposé le choix lors des manifestations contre sa troisième candidature. Il a poussé son mépris à son paroxysme en violant notre Constitution, en toisant notre indignation et en brimant la seule et unique liberté qu’il nous restait, celle de manifester.

Hapana, Abdoulaye Wade hakuwa muumini wa demokrasia wakati alipompigia simu Macky Sall (kumpongeza). Hakuwa amebakiwa na uchaguzi mwingine wowote. Tulimlazimisha afikie uamuzi huo siku ya uchaguzi tarehe 23, tulimlazimisha afikie uamuzi huo pale tulipoandamana kumpinga alipoonyesha nia ya kugombea urais kwa mara ya tatu. Alionyesha upuuzi wa hali ya juu kwa kutokuheshimu Katiba yetu, katika kutokujali hasira yetu na katika kukandamiza haki pekee na uhuru uliobaki, yaani kuandamana.

Katika blogu yake Bw. Boombastic PlO anakumbuka “jinamizi ya utawala” wa Wade [fr]:

L'élection de Macky Sall n'est pas la première alternance au Sénégal qui a toujours été démocratique. Wade serait même une parenthèse malheureuse car sous sa présidence les libertés ont été bafouées par des meurtres … Des journalistes & opposants ont ete emprisonnés (le cas des jeunes socialistes Malick Noel Seck et Barthélémy Diaz) et surtout les morts de la crise pré-électorale.

Kuchaguliwa kwa Macky Sall si makabidhiano ya kwanza ya utawala nchini Senegali, ambayo siku zote yamekuwa ya kidemokrasia. Muda wa Wade madarakani utaendelea kuwa doa kwenye historia ya siasa za Senegali, wakati ambao uhuru ulikandamizwa kwa mauaji…waandishi wa habari na wapinzani wa kisiasa waliwekwa kizuizini (mfano suala la vijana wa wenye mrengo wa kijamaa Malick Noel Seck na Barthélémy Diaz) na zaidi ya yote, utakuwa ni wakati uliotambulishwa kwa mauaji kufuatia ghasia za kuelekea uchaguzi.

Bendera ya Senegali katika eneo liitwalo de l'obélisque. Imewekwa kwenye mtandao wa Flickr na Nd1mbee imetumiwa kwa ruhusa

Katika blogu ya “Adieu Wade,” [fr] Wirriyamuanaandika:

Ces dernières années A. Wade a eu maintes fois l’occasion d’accorder un minimum d’attention aux souhaits de son peuple … Aucune de ces occasions n’a été saisie. Au contraire quand il ne répondait pas par le mépris (« je suis majoritaire » « ce sont des poltrons » « il ne se passera rien ») il répondait par l’agression.

Kwa miaka mingi (aliyokaa madarakani), Abdoulaye Wade alikuwa na fursa ya kujali matakwa ya watu wake…Hakutumia fursa yoyote kati ya hizo. Badala yake, wakati huo wote kama kuna mahali hakuitikia kwa dharau (akitoa kauli kama “nina umma nyuma yangu”, “Watu hawa ni wajinga,” au “hakuna kitakachotokea”), aliitikia kwa hasira.

Haby Ba, katika posti yenye kicha cha habari “Président Macky Sall”, [fr] anaeleza kwamba mkanganyiko wa uamuzi wake wa kugombea urais kwa mara ya tatu kwa hakika uliinyima nchi kampeni za kweli za uchaguzi:

Nous aurions dû avoir cette année une campagne qui porte sur les choix de société. Comment faisons-nous pour reconstruire l’école sénégalaise qui est clairement à la dérive? Comment organiser la solidarité nationale pour que les plus démunis soit non seulement scolarisés mais également suivis sur le plan médical? Ces questions-là n’ont pas du tout été abordées parce que nous étions focalisés sur la nécessité de veiller à la transparence du processus électoral.

Mwaka huu, tungekuwa na kampeni za uchaguzi ambazo zingejikita kwenye masuala ya msingi ya kijamii; (kama vile) tufanye nini kuujenga upya mfumo wa elimu ya Senegali, ambao ni bayana unadidimia? Tunawezaje kujenga umoja wa kitaifa ili raia maskini kuliko wote si tu wapate elimu, bali pia wapate huduma za afya? Maswali haya hayakushughulikiwa kabisa kwa sababu tulimezwa na hitaji la kuhakikisha uwazi unakuwepo katika mfumo wa uchaguzi.

Wirriyamu [fr] anasema:

Au final, en maintenant sa candidature, Wade a peut-être troublé le cours de l’histoire au Sénégal. Il a empêché la juste confrontation des idées qu’est une élection digne de ce nom. L’opposition s’est retrouvée à se structurer autour d’un seul projet : faire partir Wade. Ce faisant le Sénégal ne sait pas grand-chose des projets et ne sait pas ce qu’elle aura sauf qu’elle sait que ce ne sera pas avec Wade …

Mwisho, kwa kung’ang’ania kugombea urais, wade ameharibu mwenendo wa historia ya Senegali. Hakuruhusu ushindani wa haki wa mawazo, ambayo ni msingi wa uchaguzi wowote wenye hadhi ya kuitwa uchaguzi. Upinzani uliishia kujikita kwenye mradi mmoja: kumng’oa Wade. Katika kufanya hivyo, Senegali imeonyesha kwamba inajua kidogo mno mambo ya mipango na kwamba haijui majaliwa yake, isipokuwa (labda moja tu) kwamba mustakabali wa nchi hiyo hautafungamana na Wade…

Wanablogu wanakubaliana katika mahitimisho yao na katika namna yao ya kudai haki itendeke. Kwa mujibu wa Fabienne Fatou Diop [fr]:

Nous n’aimerions pas que les décès et les blessés lors des manifestations contre la troisième candidature d’Abdoulaye Wade soient vains. Nous exigeons que les auteurs et les commanditaires de ces crimes soient traduits devant la justice.

Hatutaki majeraha na maisha yaliyopotea wakati wa maandamano dhidi ya hatua ya Abdoulaye Wade kugombea urais kwa muhula wa tatu yawe ni bure. Tunadai kwamba wale waliohusika na ghasia hizo na wale walioamuru uhalifu huu ufanyike wafikishwe kwenye mikono ya sheria.

Haby Ba anasema [fr]:

Tant que les politiciens ne seront pas conscients que leurs actes ont des conséquences -y compris pénales- ils continueront à piller ce pays. Seule la justice peut nous éviter de retomber dans la même spirale.

Wanasiasa hawatambui ukweli kwamba matendo yao yana matokeo, hii ikiwa ni pamoja na adhabu kwa mujibu wa sheria, kwamba wanaendela kuifilisi nchi hii. Ni mfumo wa sheria tu unaweza kutulinda kurudi kwenye mzunguko wa zamani.

Bw. BoOmbastic PlO anaandika [fr]:

Ces parents de victimes estiment que Wade et ses hommes ne doivent pas emporter avec eux «cette injustice et que toute la lumière doit être faite sur ces meurtres.»

Familia za waathirika zinaamini kwamba Wade na wafuasi wake hawapaswi kukwepa uvunjifu mkubwa wa haki na kwamba wanapaswa kujiandaa kwa vifo vyao”.

Kwenye mtandao wa twita, @astouka ameanza kutafuta uungwaji mkono kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu za serikali inayoondoka madarakani nchini Senegali, pamoja na kufumuliwa kwa mfumo wa sheria wa nchi hiyo. [fr].

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.