Bolivia: Wanaharakati Washinikiza Upatikanaji Nafuu wa Mtandao wa Intaneti

Wanablogu na wanaharakati wanatetea haki ya kupata “kiwango cha chini kinachokubalika cha kasi” ya kuunganishwa na mtandao wa intaneti nchini Bolivia.
Kama ilivyokuwa imeripotiwa na (tovuti ya) Global Voices , Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Kukuza Uunganishwaji wa Intanenti nchini Bolivia National Meeting to Promote Connectivity in Bolivia [es] ulifanyika mwishoni mwa Januari 2012. Baada ya mkutano huo, kikundi cha wanaharakati kiliendelea kutetea, kama mwanablogu Mario R. Duran kutoka Palabras Libres [es], who met [es] aliyekutana na Rais wa “chemba”, Ms Gabriela Montaño.
Kampeni hiyo ilitafuta pia kujulisha na kukuza uelewa wa masuala na vikwazo vinavyotokana na hali ya sasa ya mtandao.
Kikundi hicho kinakutana kuunga mkono tovuti ya Más y mejor internet para Bolivia [es] (Mtandao zaidi na nafuu kwa ajili ya Bolivia). Tovuti “inatafuta usawa katika upatikanaji wa mtandao wa intanenti kwa wa-Bolivia […] Usiote kupata mtandao wa kasi kubwa ila dai kasi ya kiwango cha kawaida kinachokubaliwa”.

Wahitajika-Upatikanaji Nafuu wa Mtandao kwa wa-Bolivia wote. Picha kwa hisani ya IICD kupitia mtandao wa Flickr, CC BY 2.0

Mchoro wenye taarifa [es] umekuwa ukisambaa katika majukwaa ya vyombo vya habari vya kiraia kuonyesha kwamba Bolivia ni kati ya maeneo ya mwisho kabisa katika sekta ya ubora wa kasi ya mtandao barani Amerika ya Kusini. Mchoro huo unaonyesha pia kwamba nchini Bolivia, Megabaiti moja kwa sekunde inagharimu kati ya mara 6 na 11 zaidi ya inavyokuwa katika nchi nyingine za jirani kama Paraguay, nchi ambayo ina eneo dogo sana la ardhi.
Injia wa Umeme Sergio Toro, ambaye ni mtaalamu wa ki-Bolivia kwenye masuala ya TEKNOHAMA ya maendeleo, alitoa maoni katika posti iliyowekwa kwenye blogu ya post by TIC para el desarrollo‘s [es] blog:

el costo de una banda ancha superior a un megabyte es de 700 bolivianos, eso significa el 98% del salario mínimo, mientras que en Corea del Sur –por ejemplo- el mismo servicio cuesta un 0,2% del salario mínimo

Gharama ya kutumia Megabyte moja ni sarafu za Bolivia 700 (karibu Dola za kimarekani 102), hiyo ikiwa nai karibu ya asilimia 98 ya ujira wa chini kabisa, wakati nchini Korea Kusini kwa mfano, huduma hiyo hiyo inagharimu asilimia 0.2 ya ujira wa chini kabisa nchini humo.

Miongoni mwa wale wanaopigania miunganisho nafuu ya mtandao wa intanenti ni Edgar Yana kutoka Nuestra Cultura Primero. Edgar ni mwanablogu anayeishi katika jamii ya wenyeji wa Chaguaya, umbali wa masaa matatu na nusu kwa basi kutoka jiji la El Altro. Alihudhuria Mkutano wa Kitaifa wa Kukuza Uunganishwaji wa mtandao wa intaneti nchini Bolivia, na taarifa ya kuhitimisha mkutano huo [es] inakazia mazingira ya kazi yake:

Edgar Yana, comunario de Chaguaya menciona que tiene que viajar a El Alto para subir contenidos a su blog y que tener internet en su casa es una necesidad.

Edgar Yana, mwanachama wa jumuiya hii kutoka Chaguaya anasema ilimbidi kusafiri kuja El Alto kuja kupandisha maudhui kwenye blogu yake, kwa hiyo kuwa na mtandao wa intaneti nyumbani ni hitaji la kweli.

Wanaharakati wanakusanywa kwenye ukurasa wa Facebook uitwaoADSL Bolivia [es], ukurasa wa Facebook Más y mejor internet YA [es(Mtandao nafuu wa Intanenti SASA) na pia maoni kwenye mtandao wa twita kwa kutumia alama #mejorinternetYA [es].

Lengo la kampeni hiyo limefanyiwa muhtasari na Mario R. Duran katika posti katika blogu ya El Eco de los Pasos [es]:

la meta es que en el 2014, todos los hogares bolivianos tengan acceso a 1 mbps (como velocidad mínima) a un costo menor a 20 dólares

Lengo ni kwamba mpaka 2012, nyumba zote za wananchi wa Bolivia wawe na angalau MB 1 kwa sekunde (kiwango cha chini kabisa cha kasi ya mtandao) kwa gharma ya chini ya dola 20 za kimarekani.div>

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.