Mexico: Wanafunzi Wawili Wauawa Kwenye Maandamano Huko Ayotzinapa

Wanafunzi wawili, Jorge Alexis Herrera Pino na Gabriel Echeverría de Jesús, waliuwawatarehe 12 Desemba 2011, wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya vijijini ya Raúl Isidro huko Ayotzinapa, mji mkuu wa Guerrero, Chilpancingo, nchini Mexico.

Maandamano yaliifunga barabara kuu ya “Autopista del Sol” inayoelekea kwenye eneo la kitalii Acapulco. Mitazamo yenye utata kuhusu yalioyotokea imechapishwa mtandaoni, ukiwemo ule uliotolewa na mamlaka za Guerrero iliyosema kuwa maandamano haya “si ya kwaida” na kuwa kuna “watu wengine” wasiohusiana na wanafunzi ambo walishiriki katika maandalizi ya maandamano.

La Jornada de Guerrero [es] ilichapisha mtiririko wa matukio:

Mambo yote yalianza na pazia la moshi, lilisababishwa na mabomu ya machozi ambayo yalitokea mikononi mwa polisi (wa serikali kuu). [..] Baada ya hapo ukafuata mfumuko wa kwanza wa risasi kutoka kwa polisi ambao walipewa kibali kupitia redio. Mfumuko wa pili ambao ulikuwa mrefu zaidi, ulitokea kwenye mikono tofauti: polisi wa wizara waliwafytulia risasi wanafunzi kutokea upande wa kulia (wa barabara kuu kutokea kaskazini kwenda kusini) […] haikuwachukua muda mrefu polisi wa serikali kuu kulenga shabaha ile ile. […] Upande mwingine, upande wa Ayotzinapa, wanafunzi wa vijijini wenye bajeti ya chakula ya dola 3.5 kwa siku, walijibu kwa mawe na magongo. Mabomu ya kujitengenezea hayakutumiwa kwa kuwa hawakupata muda wa kununua mafuta kutoka kwenye vituo vya mfuta viwili vilivyo kandokando ya barabara hiyo. Baadhi, katika harakati za kujitetea, waliwasha mitungi waliyopata kwenye vituo vya mafuta. Ndipo polisi wakawatupia wanafunzi mabomu ya kusambaratisha ya mkono, ambao kwa wakati huo walikuwa wakijitahidi kujiokoa kwa kujificha kwenye nafasi katikati ya misururu ya magari na ukuta uanotenganisha barabara hiyo kuu. Kwa ujumla kulikuwa na mabomu ya kutupa kwa mkono matano ambayo hayakulipuka lakini yalileta mtafaruku kwa wanafunzi hao. […]. Ni wanafunzi wawili tu ambao hawakukimbia, wote walikuwa na umri wa miaka 22.

Shule ya normalista iliyoshiriki katika maandamano ina historia ya kuwa na upinzani katika utamaduni wa kizamani wa ‘escuelas normalistas rurales’, ni shule ambazo zinatengeneza walimu wa kutoka kwenye jamii maskini na zenye duni. Shule hii inamilikiwa na Federación de Estudiantes Campesinos Socialistas de México (Shirikisho la Jamii ya Wanafunzi wa Kisoshalsti wa vijijini nchini Mexico). Mwanahabari Diego Osorno, ambaye amejikita zaidi katika kuandikia migogoro ya jamii, aliandika habari kwenye blogu ya Nuesta Aparente Rendición kuhusu mgogoro wa normalistas huko normalistas huko Guerrero [es], hasa wa shule ya Ayotzinapa.

Shule hiyo ilitoa tangazo [es] ambalo lilikanusha kuwa na silaha zozote na kudai haki katika mauaji hayo, ambayo waliyaita kuwa ni “mauaji nje ya utaratibu wa mahakama”. Maandishi (ya tangazo hilo maalum) pia yanaelezea kusitishwa mara kwa mara kwa mikutano iliyopangwa ya kukutana na Waziri wa Elimu wa Guerrero na kumtaka gavana kujiuzulu.

Ukuta wa shule ya Normalistas ya “Isidro Burgos” huko Ayotzinapa. Picha na @kradprro

Mnamo Desemba 13, Mkuu wa Sheria Alberto López Rosas, wakati wa mahojiano ya redio Carmen Aristegui [es], alitangaza kuwa mmoja wa waliowekwa kizuizini – ambaye ana umri wa miaka 19 alikuwa na bunduki aina ya AK-47, lakini bado hawajajua kama risasi zinawiana na zile zilizowauwa wanafunzi wawili. Hata hivyo alisema kuwa bunduki hiyo haifanani na zile zinazotumiwa na polisi, na aliweka wazi kuwa matendo ya polisi hayakuwa ya kikandamizaji na kuwa walitaka kuleta utulivu tu. Kuhusiana na hili,La Jornada [es] imechapisha taarifa kuhusu matumizi mateso makali ili “kutengeneza” ushahidi kuhusu silaha hiyo ya AK-47.

Baadaye siku hiyo, López Rosas alipinga [es] tamko lile la mwanzo, aliposema kuwa risasi zinaweza kuwa zilifyatuliwa na polisi.

Lakini wakati wa tukio, Roberto Ramirez (@robertoramirezb),mkuu wa habari wa jarida La Jornada Guerrero, aliandika kupitia twita:

#Ayotzinapa Eso no es enfrentamiento, eso es un crimen

#Ayotzinapa haya si mapambano (ya kawaida), ni jinai

Akitaarifu kupitia twita alisema kuwa alikamatwa na kushikiliwa kwa kuwa alionekana kama mwanafunzi na alikuwa amepigwa sana [es] [es] kabla ya kuachiwa. Ramírez pia alieleza kupitia twita kuwa baadhi mabomu ya kutupwa kwa mkono yaliyookotwa kwenye eneo la tukio yalitengenezwa nchini Uingereza[es].

Kupitia twita, watumiaji wamekumekuwa wakichangia kwa uchache, picha zinazojieleza vilivyo za wanafunzi hao waliofariki ([1] [2]); moja ya picha hizo inaonyesha mwanafunzi mwenye alama za kuteswa.Reforma, moja ya vyombo vya habari vikuu nchini mexico imeweka video ambayo inaonyesha mtu mwenye mavazi ya kawaida akifyatua risasi. Pia wameweka mtiririko wa picha [es] za mmoja wa wanafunzi akikimbia kabla ya kupigwa risasi.

Wakati huo huo, El Universalilitaarifu [es] kuwa [es] risasi zilizowauwa wanafunzi ziliwalenga vichwani, na Revista Proceso [es] imeongeza kuwa mashahidi wamesema kuwa polisi wakiwauwa wanafunzi hao. Kwenye mkutano na waandishi wa habari tarehe 13 Desemba, wanafunzi wa Ayotzinapa walisema polisi walipiga simu na wakapewa ruksa au ‘taa ya kijani” iliyowaruhusu kufanya lolote walilotaka – na ndipo walipoanza kufyatua risasi, Contralínea inataarifu [es].

Kwa mujibu wa La Jornada [es], watu wane walijeruhiwa kwa risasi, na mwanfunzi Édgar David Espíritu amepoteza fahamu hadi sasa. Watu ishirini na watatu waliachiwa mchana wa tarehe 13 Desemba, lakini 15 hawajulikani walipo na ripoti hiyo pia inasema kuwa mmoja bado anashikiliwa na polisi.

Baadaye siku ya Desemba 13,Mkuu na Mkuu Msaidizi wa Ulinzi , pamoja na na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Chilpancingo, waliachishwa [es] kazi na gavana wa Guerrero.

Watumiaji wa twita walionyesha hasira zao kwa kutumia alama ya #Ayotzinapa [es]:

@roblesmaloof: Culpar a quienes son asesinados de sus propias muertes, es tan viejo como las dictaduras y no se los vamos a creer. #Ayotzinapa.

@roblesmaloof: kuwalaumu waliouwawa kwa vifo vyao, ni tabia ya kizamani kama ulivyo udikteta na kamwe hatutaamini.. #Ayotzinapa.

@danischmidt: Yo aquí desayunamdome el asesinato de 2 estudiantes normalistas por el abuso de las fuerzas policiacas #Ayotzinapa

@danischmidt: Napata kifungua kinywa [na ninajifahamisha kuhusu] mauaji ya wa-normalistas wawili kutokana na ukandmizaji wa polisi #Ayotzinapa.

@VinitoPereda: No dudo que la #PF actuó en consecuencia a la psicosis que les ha producido la guerra de Calderón. Eran ESTUDIANTES no Narcos. #Ayotzinapa

@VinitoPereda: Sina shaka kuwa #PF (polisi wa serikali kuu) walifanya hivyo kutokana na matatizo ya kiakili yaliyosababishwa na vita ya Calderon. Walikuwa ni WANAFUNZI na sio wauza madawa ya kulevya #Ayotzinapa.

@Morf0: Primero les matan el derecho a la educación y luego los matan a ellos. #Ayotzinapa

@Morf0: Kwanza waliua haki ya kupata elimu halafu wakawauwa [wanafunzi] #Ayotzinapa

@blanchepetrich: ¿Qué son muy “radicales” los estudiantes campesinos de #Ayotzinapa? Denles razones, argumentos, respuestas ¡no balazos!

@blanchepetrich: Kwa hiyo wanafunzi wa bara #Ayotzinapa ni “wenye siasa kali” sana? Wapeni sababu, majibu na hoja sio risasi!

@roblesmaloof: Qué difícil es para los medios convencionales decir que los estudiantes de #Ayotzinapa fueron asesinados.

@roblesmaloof: Ni ngumu kwa vyombo vya habari vya zamani kusema kuwa wanafunzi wa Ayotzinapa waliuawa.

@Asteris: Je Mexico sasa iaaonekana machoni mwa vyombo vya habari vya kimataifa kama Iraq nyingine? Kumekuwa na matukio mengi ya kihalifu kiasi cha kushindwa kuyaficha#Ayotzinapa #Chilpancingo

Hamlet García Almaguer (@hamletgar) ameandika katika blogu ya LetraJoven [es]:

Y ahí está el problema, por que quienes han vivido en Guerrero saben que Guerrero es bronco y que en cualquier momento puede levantarse; y saben que los homicidios desde el poder son intolerables.

Hilo ndilo tatizo, wale walioishi Guerrero wanajua kuwa Guerrero ni pabaya na wakati wowote watu wanaweza kuja juu; na wanajua kuwa mauaji yanayofanywa wenye nguvu hayavumiliki.

Tume ya Haki za Binadamu ya Mexico imeanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.