GlobalVoices katika

Japani: Tsunami yaathiri eneo la pwani, yaacha kila kitu kimeharibiwa

TafsiriMakala hii inapatikana pia katika:

Français · Japon : le tsunami frappe la côte, rien ne lui résiste
Español · Japón: Un tsunami golpea la costa y lo arrasa todo
Malagasy · Japana: Mamely ny morontsiraka ny tsunami, tsy mamela mahazo
Deutsch · Japan: Tsunami trifft auf Küste mit verheerenden Folgen
Nederlands · Japan: Allesvernietigende tsunami bereikt kust
বাংলা · জাপান: সুনামি আঘাত হেনেছে, কিছুই বাকি রাখেনি
Italiano · Giappone: Tsunami colpisce la costa lasciandosi dietro solo devastazione
Magyar · Japán: Nem maradt semmi a cunami nyomában
繁體中文 · 日本:海嘯來襲、水漫各地
简体中文 · 日本:海啸来袭、水漫各地
polski · Japonia: Tsunami uderza w wybrzeże, zmywając wszystko z powieżchni ziemi
日本語 · 日本:津波が太平洋沖を襲撃、全てを奪う
Português · Japão: Tsunami atinge litoral e arrasta tudo
English · Japan: Tsunami Strikes Coast, Leaves Nothing in Wake

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.

Kufuatia tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini, Japani imekumbwa na tsumani mbaya zaidi iliyowahi kutokea. Watu wengi nchini kote wameganda kwenye luninga zao wakati vipande vya habari vinavyoonesha tsunami lenye urefu wa zaidi ya mita 7 kwenda juu likisomba magari na majengo. Wakati huo huo, maeneo mengine ya dunia yanajiandaa kwa matukio mabaya zaidi, Hawaii imetoa amri ya kuhama kutoka kwenye maeneo ya pwani na tahadhari zimetolewa katika nchi zisizopungua 20. Jarida la The Guardian linatoa habari za mpya kadiri zinavyojitokeza kuhusiana na janga hilo.


http://www.youtube.com/watch?v=lSimeWFiuYc

Picha ya wimbi kubwa la bahari mjini Ibaraki (kupitia @gakuranman):

Baadhi ya ujumbe kwenye twita.

Tinystar323 anaandika:

津波は「波」じゃなくて、「コンクリートの壁が猛スピードで突っ込んでくる物」だと思って下さい。人間にどうにか出来る代物じゃないです。絶対に興味本位で見に行ったりしないで下さい。

Tafadhali usifikirie tsunami kama “mawimbi”, lakini (ifikirie) kama “kuta nzito zinazoporomoka kwa kasi ya ajabu kabisa”. Wanadamu hawezi kupambana nayo. Tafadhali usiende nje kuangaia kukidhi dukuduku.

Taarifa isiyothibitishwa kutoka @nishi_0024 ikidai kwamba kituo cha mkutano cha Pacifico Yokohama hakipokei tena watu:

【緊急拡散】パシフィコ横浜は津波の危険があるため、受け入れ中止だそうです!

Pacifico Yokohama [kituo cha mikutano] kimo kwenye hatari ya kukumbwa na tsunami, wamesitisha kupokea watu!

Kutoka @edamamicky, mwathirika wa tsunami:

津波被害あり。自宅2階にて母と弟と近所の男性一名と救助を待っています。怪我はありません。1階は浸水して自力では外に出れません。電話も繋がりません。

Mwathirika wa tsunami hapa. Nipo eneo la makazi la 2F pamoja na mama yangu, kaka na majirani tukingoja kuokolewa. Hakuna majeruhi. Eneo la makazi la 1F limegharikishwa na maji na hatuwezi kutoka nje wenyewe. Vilevile mawasiliano ya simu yamekatika.

Kwa habari za hadi dakika iliyopita kuhusiana na hali ya mambo baada ya tetemeko, fuatilia chanzo rasmi cha habari cha NHK.

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Taratibu

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.


Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha