Ivory Coast: Je, nani anadhibiti televisheni ya taifa ya RTI?

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast.

Bado kuna mkanganyiko kuhusu swali la nani hivi sasa ndiye mwenye udhibiti wa Radio Télévision Ivoirienne (RTI), ambacho ni kituo cha televisheni ya taifa.

Mnamo tarehe 31 Machi, Vikosi vya majeshi ya FRCI, ambao ni waasi wanaomuunga mkono rais anayetambuliwa na jumuiya ya kimataifa, Alassane Ouattara, viliingia jijini Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast. Vikosi hivyo vilipofika kwenye makao makuu ya RTI vilikabiliana na upinzani mkali kutoka Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya FDS vinavyomuunga mkono Gbagbo. Televisheni hiyo ya taifa hujulikana kwa jina la kebehi la “TV ya Propaganda” au “TV ya LMP” kwa sababu ya kile kinachochukuliwa kwamba inamwunga mkono Rais Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kukiri kwamba alishindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2010 na amekataa kuachia madaraka. RTI imegeuzwa kuwa uwanja wa kuwania udhibiti kamili wa vita.

Kwanza matangazo yalikatwa kwa saa 24, na mnamo tarehe 1 Aprili, 2011 Directscoop, ambayo ni blogu ya habari za kiraia za kutoka Afrika, ilitangaza [fr] kwamba mawimbi ya kituo hicho yalikuwa yameanza kupatikana tena:

La Radiodiffusion télévision ivoirienne ( Rti) a recommencé à diffuser son signal vendredi peu après 19 heures

RTI ilianza tena kurusha matangazo mara tu baada ya saa 1 jioni siku ya Ijumaa

MsomajiWanyu, aliotoa maoni haya:

Un long metrage de Damon : « LA VENGEANCE DANS LA PEAU » est diffusé en ce moment sur la RTI.

Filamu ndefu ya hadithi inayomjumuisha Matt Damon: “The Bourne Ultimatum” inaendelea kurushwa hewani kupitia RTI

Infodabidjan.net [fr], a ambayo ni tovuti ya habari, iliingiza kwenye YouTube video hii ya kiraia iliyopigwa tarehe 1 Aprili, 2011:

Maelezo chini ya video yanaeleza:

Premieres images de la RTI après sa liberation

Picha za mwanzo baada ya RTI kukombolewa

Kundi kubwa la Facebook linalojiita “The Comittee for the struggle against French interference in Côte d'Ivoire” (yaani Kamati ya mapambano dhidi ya uingiliaji wa Ufaransa kwenye mambo ya ndani ya Ivory Coast) [fr] ambalo lina kiasi cha wanachama 6720 wanaomwunga mkono Gbagbo, ilituma kwenye ukurasa wake video ya RTI ya matangazo ya tarehe 2 Aprili, Upande wa Habari za Televisheni : Wanajeshi wa FDS walionyeshwa wakisoma taarifa kwa vyombo vya habari, ikieleza jinsi walivyoshambuliwa na vikosi vya Ouattara, vikiungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast (ONUCI). Walieleza pia kwamba hali katika vituo vya RTI – na hata Abidjan – kwa ujumla ilikuwa shwari na kwenye udhibiti , na kwamba watu waendelee na harakati za maisha yao kama kawaida.

Kupitia Twita, raia walitoa miitiko kuhusiana na uingiliaji kati huu mara moja:

@Gare_au_gorille alikasirishwa mno:

@Gare_au_gorille: la RTI veut 1 bouclier humain en ne relayant pas couvre feu #civ2010 > RESTEZ CHEZ VOUS et faites passer le mot !!!

RTI inataka kujenga ngao ya binadamu kwa kutotangaza amri ya kutotembea hadharani #civ2010. BAKINI NYUMBANI na msambaze ujumbe huu!!!

@JusticeJFK naye:

@JusticeJFK: Intervenant FDS sur la RTI: “nous appelons les populations à vaquer normalement à leurs occupations”. Quelle irresponsabilité!!!

Msemaji wa FDS kupitia RTI: “Tunawatangazia watu kuendelea na shughuli zao kama kawaida” Huku ni kukosa uwajibikaji!!!

“The committee for the struggle against French interference in Côte d'Ivoire” (yaani Kamati ya mapambano dhidi ya uingiliaji wa Ufaransa kwenye mambo ya ndani ya Ivory Coast) ilituma video nyingine iliyopigwa tarehe 2 Aprili katika ofisi za RTI, na kama ushahidi kwamba sasa televisheni ya taifa ilikuwa mikononi mwa FDS inayomwunga mkono Gbagbo. Video hiyo ilitumwa tena kwenye Youtube na AfricaWeWish:

Stéphane Kassi, ambaye ni mwajiriwa wa RTI anaeleza kuhusu kile kilichotokea tarehe 31 Machi, 2011:

Le jeudi (…) Suite à l'alerte de l'attaque de la rébellion, nous avons essayés de faire un repli, au niveau de la cité qui est en face se trouve à côté (…) Nous ne sommes pas agents de la régie, mais nous avons fait de notre mieux. (…) Les combats ont eu lieu , et nous avons réussi à nous terrer quelque part jusqu'à ce qu'on ait pu nous exfiltrer. Ce matin nous sommes là, comme le pays nous le demande, Nous sommes là pour défendre notre patrie.”

Baada ya tahadhari kuhusu shambulio litakalofanywa na waasi, tulijaribu kujiondoa na kujikusanya katika eneo la karibu kabisa. Sisi sio mawakala wa watu wenye wanaodhibiti utengenezaji wa matangazo, lakini tulijaribu vile tulivyoweza. (…) Mapigano yalitokea, na tulifaulu kujificha mahali mpaka tulipookolewa. Asubuhi ya leo tupo hapa, kama vile nchi inavyotaka; tupo hapa ili kulinda utaifa wetu.

Makala hii ni sehemu ya Makala zetu maalumu kuhusu Machafuko ya mwaka 2011 nchini Ivory Coast..

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.