Myanmar: Hatimaye Suu Kyi Amekuwa Huru

Amekuwa kifungoni kwa miaka 15 katika miaka 21 iliyopita, lakini hivi sasa hatimaye yuko huru. Kiongozi wa upinzani na alama ya wapenda demokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi aliachiwa huru kutoka kizuizini mchana siku ya Jumamosi na serikali inayoungwa mkono na jeshi la Myanmar baada ya kuendeshwa kwa uchaguzi wa taifa ambao ulitawaliwa na wagombea wanaoungwa mkono na serikali.

Tovuti ya The Democratic Voice of Burma iliweza kufuatilia na kurekodi dakika chache za kwanza za kuachiwa kwake. Video hii inawaonyesha mashabiki wa Suu Kyi waliokuwa wakipunga mikono mbele ya nyumba yake iliyoko kando ya ziwa.

AUNG SAN SUU KYI AACHIWA kutoka DVBTV English kupitia Vimeo.

Habari zilisambaa Alhamisi iliyopita kwamba Suu Kyi angeachiwa mwishoni mwa juma mnamo tarehe ambayo kifungo chake cha nyumbani kingeisha. Ilitaarifiwa kwamba alikuwa ametia saini makaratasi ya kuachiwa mnamo majira ya saa 6 mchana siku hiyo Hata wanachama wa chama cha National League for Democracy, ambacho ni chama cha Suu Kyi, walianza kusafisha ofisi za makao makuu ya kamati kuu huku wakiwa na matarajio ya kuachiwa kwa Suu Kyi. Siku ya Ijumaa, kulikuwa na umati wa watu 500 au zaidi waliokusanyika mbele ya ofisi za NLD mjini Yangon, wote wakiwa wanasubiri kuachiwa kwa Suu Kyi. Bango lililokuwa mbele ya makao makuu hayo lilisomeka “ Leo ni Siku ya Kuachiwa Kwake “.

Kadhalika, zaidi ya wanachama 100 wa NLD na mashabiki wa NLD walijitolea damu katika hospitali ya eneo hilo ili kuvutia watu waelewe juu ya kuachiwa kwa Suu Kyi.

Mategemo ya uhuru wa Suu Kyi yalitiliwa mashaka baada ya mahakama ya juu nchini Burma kukataa rufaa yake ya mwisho dhidi ya kifungo cha nyumbani Ijumaa, na kuwafanya watu wawe na wasiwasi kuwa angeachiwa au la.

Wakati huo huo, inasemekana kuwa viza ya Kim Aris, mwanawe Aung San Suu Kyi iliidhinishwa ili aweze kuzuru Myanmar.

Kwamba hivi sasa hatimaye Suu Kyi yuko huru, tovuti huru ya habari The Irrawaddy inawataka wasomaji wake kuwasilisha mapendekezo na mawazo mbalimbali kwa Suu Kyi

Dunia ilifurahi wakati Suu Kyi, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Nobeli, alipoachiwa huru kutoka kifungo cha nyumbani. Watumiaji wa Twita walitumia alama ya #aungsansuukyi wakati walipojiunga na mazungumzo ya ulimwengu mzima uliokuwa ukisherehekea uhuru wa Suu Kyi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.