Mexico: Mwanamke wa Miaka 20 ni Mkuu Mpya wa Polisi katika Mji wa Kaskazini mwa Mexico

Jina lake ni Marisol Valles García na amepewa jina la mwanamke jasiri kuliko wote nchini Mexico” [es].

Valles García ni mwanamke aliyeolewa mwenye umri wa miaka 20 ambaye anasoma mwaka wa mwisho wa masomo ya makosa ya jinai na uhalifu; vile vile ni mkuu mpya wa polisi wa Práxedis, Chihuahua. Práxedis ipo umbali wa kilometa 100 (maili 62) kutoka Ciudad Juárez, mji wenye uhalifu zaidi nchini Mexico.

Lakini, Kwa nini alipewa kazi muhimu kama hii? Richard Grabman alieleza hali ilivyo katika blogu yake The Mex Files:

Mgombea pekee aliyejitokeza kuliongoza jeshi la ulinzi wa jamii alikuwa Marisol Valles García, mwanafunzi wa miaka 20 anayesomea elimu ya makosa ya jinai na uhalifu. Mkuu wa polisi mpya (na mwenye uri mdogo kuliko wote nchini Mexico) anayesimamia kitengo ambacho kinaweza kutoa zamu mbili za askari wa kulinda doria katika kila jamii.

Cristhian García, mwanablogu wa Mexico mwenye umri wa miaka 21 ametoa maoni yake [es] juu ya suala hilo:

El alcalde de ese municipio, buscaba un Jefe de Policía, y después de repasar a todos los hombres que tenia dentro de la corporación, Marisol se levanto y dijo: “Aquí toda la gente tiene miedo, todos tenemos miedo, pero vamos a cambiar ese miedo por seguridad”

Y para demostrar su valor, ayer Marisol se dejo fotografiar con la cara descubierta, mostrando así que en Mexico aun hay personas valientes que están dispuestas a luchar contra el narcotráfico y el crimen organizado.

Meya wa mji huu alikuwa akitafuta mkuu wa polisi, na baada ya kuwaangalia wanaume wote waliopo jeshini, Marisol alisimama na kusema: “Hapa kila mmoja anaogopa, wote tunahofu, lakini basi hebu tubadili hofu hiyo kwa ajili ya usalama”

Na katika kuthibitisha ujasiri wake, Jana Marisol alipigwa picha akiwa hajafunika uso wake, akionesha kuwa nchini Mexico bado wapo watu jasiri wenye nia ya kupiga vita biashara ya madawa ya kulevya na uhalifu.

Makala katika wavuti ya habari ya La Polaka [es] inaafiki kuwa, “hakuna mwanaume hata mmoja anayetaka kuwa polisi na zaidi kuwa mkuu wa polisi, kwa sababu ya hofu ya kuuawa kama ilivyowatokea polisi wengine wengi.”

Kwa sasa, raia wa Mexico na watu wengine kote ulimwenguni waliopata kusikia juu ya ujasiri wa Valles García wamekuwa wakiandika twita kuhusu habari hiyo: Mtumiaji Adam D. Prince (@rabbitcincouno) kutoka Ohio alituma twita hii:

#HerooftheWeek tuzo iende kwa binti wa miaka 20 Marisol Valles Garcia, Mwanafunzi wa Kriminolojia ambaye ni mkuu wa polisi wa Guadalupe, nchini Mexico…

Laura Ruíz (@YoSoyBereNice), fwa Veracruz, México alichangia kwa maoni haya:

Marisol Valles García de 20 años encabeza policía en Chihuahua.-Para que vean quien lleva los pantalones por allá.

Marisol Valles Garcia mwenye umri wa miaka 20-year, amekuwa mkuu wa polisi huko Chihuahua. – Unaweza kutambua “nani anavaa suruali” huko Chihuahua.

Mada hii ilijadiliwa pia kwenye akaunti ya mcheza filamu Tom Cruise, (@TomCruise):

Marisol Valles Garcia mwenye umri wa miaka 20 ni shujaa wa kweli akiwa kama mkuu wa polisi kwenye mji wenye uhalifu wa hali ya juu sana nchini Mexico. Tumuunge mkono: http://bit.ly/ata0wm

Mwisho, katika blogu ya Hermosillo kupitia Periodista Digital [es], tukio hili limeandikwa na Valles García ametajwa kuwa ni mtu wa kujivunia sana katika eneo lake:

Sin duda alguna una vez más la enaguas de la bella y valiente mujer de Chihuahua pone en alto a su región.

De todas maneras bienvenidos los comentarios ya que ELLA, MARISOL VALLES GARCÍA, así con mayúsculas, fue única que aceptó el cargo.

Bila shaka, Kwa mara nyingine tena “Sketi” ya mwanamke mzuri na jasiri kutoka Chihuahua imeipa mkoa huo jina na sifa nzuri.

Pamoja na hivyo, tunakaribisha maoni kwa kuwa Mwanadada, MARISOL VALLES GARCÍA, kwa herufi kubwa, ndiye pekee aliyekubali kufanya kazi hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.