Novemba, 2010

Habari kutoka Novemba, 2010

Haiti: Kuokoa Maisha

  20 Novemba 2010

“Idadi ya wagonjwa waliotibiwa katika siku 10 zilizopita ni 227″: matumaini ya kweli kwa haiti wanaeleza uzoefu wao wakati wanasaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Myanmar: Hatimaye Suu Kyi Amekuwa Huru

  20 Novemba 2010

Amekuwa kifungoni kwa miaka 15 katika miaka 21 iliyopita, lakini hivi sasa hatimaye yuko huru. Kiongozi wa upinzani na alama ya wapenda demokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi aliachiwa huru kutoka kizuizini mchana siku ya Jumamosi na serikali inayoungwa mkono na jeshi la Myanmar

Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon

  11 Novemba 2010

Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.

Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’

  11 Novemba 2010

Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” amefariki kutokana na shambulio la moyo mnamo Oktoba 21 akiwa na umri wa miaka 66. Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa utamaduni wa Uruguay. Mwaka huu alikuwa akifanya kazi na wasanii wengine katika mradi wa Kompyuta Moja ya Mapajani kwa Kila Mtoto nchini Uruguay Uruguay, Mpango wa Ceibal, ili kutumbuiza kwenye maonyesho kwa ajili ya watoto wa shule nchini kote.

Haiti: Video Inayookoa Maisha

  9 Novemba 2010

Mganga nayeishi jijini Fransisco ambaye pia ni mwanablogu Dkt. Jan Gurley amezuru Haiti mara mbili tangu lilipotokea tememeko la ardhi la Januari 12 ili kuwahudumia watu kwa kujitolea. Ziara yake ya pili ilikutana na tukio la maambukizi ya kipindupindu ambalo limetwaa maelfu ya maisha na kusababisha maelfu wengine kulazwa hospitali...