Kuna kundi la raia wa Cape Verde ambalo huandaa mikutano mjini Lisbon ili kujadili uhusiano kati ya vijana na siasa, kama anavyoeleza Suzano Costa katika video [pt] kama ilivyowekwa tena na Amilcar Tavares. Katika blogu yao – Tertúlia Crioula [pt] – unaweza kusoma maelezo yaliyochukuliwa kutoka “Cape Verde katika Mdahalo” kadhalika unaweza kusoma majadiliano mengine kuhusu masuala muhimu.