Brazil: Ukatili Dhidi ya Wanawake Kila Siku

Mauaji ya hivi karibuni ya mwanamke yaliyofanywa na aliyedaiwa kuwa baba wa mwanae, na kijana golikipa mtarajiwa wa Brazil, yamekuwa kwenye vyombo vya habari, na kuishtua nchi nzima kwa kiasi cah ukatili uliofanywa kwenye ualifu huo. Wakati huohuo, Instituto Sangari [pt], taasisi isiyo ya kibiashara ya kuelimisha jamii juu utamaduni wa kisayansi iliyopo São Paulo, ilichapisha Ramani ya Ukatili Nchini Brazil ya mwaka 2010 [pt] ikieleza kuwa wanawake kumi wanauawa kila siku nchini humo. Bila shaka, uwanja wa blogu wameweka haya mawili pamoja na ulaani wa vitendo hivyo vya kihalifu umeondokea kuwa mada kuu zaidi ya yale yanayotangazwa katika vyombo vikuu vya habari, ambavyo vimejikita katika habari za uhalifu wa mchezaji huyo wa mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa Nilcéa Freire, Waziri wa sera za wanawake, ukatili dhidi ya wanawake kwa hakika unpuuzwa sana na vyombo vya habari [pt]:

“Quando surgem casos, principalmente com pessoas famosas, que chegam aos jornais, é que a sociedade efetivamente se dá conta de que aquilo acontece cotidianamente e não sai nos jornais. As mulheres são violentadas, são subjugadas cotidianamente pela desigualdade”, afirmou ao ministra.

Kunapokuwa na kesi, hasa za watu maarufu ambazo hutokea kwenye habari , jamii hujua kinachotokea kila siku na kile ambacho hawapati kupitia magazeti. Wanawake wanabakwa, wanatawaliwa kwa kupitia ukosefu huu wa usawa.

Huku wakiwa na uelewa huo, makundi ya wanawake, kama vile Pão e Rosas [Mkate na Maua, pt], yanauliza je matukio mangapi zaidi inabidi yatokee ili wanawake wanaokandamizwa waungane mashuleni, mitaanini na katika maeneo ya kazi.

Devemos exigir abrigos para as mulheres vítimas de violência e para seus filhos e filhas subsidiados pelo Estado, mas sob controle das próprias vítimas de violência, das organizações e comissões de mulheres independentes do Estado, da patronal, da polícia e da Igreja.

Ni lazima tudai hifadhi ya makazi kwa wanawake walioathirika na ukatili pamoja na watoto wao, kwa ruzuku ya serikali, lakini chini ya usimamizi wa waathirika wenyewe, na mashirika au umoja wa wanawake bila kutegemea serikali, polisi au makanisa.

Siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, Flickr, maonesho ya Daniela Gama, CC Licensed

Matukio ya ukatili dhidi ya wanawake nchini brazili yamesambaa nchini kote. . Ikiwa kwa upande mmoja wilaya 50 zinazidi kwa idadi ya mauaji 10 kwa kila wakazi 100.000, zaidi ya nusu ya majiji ya Brazili hayakuwa na maujai yaliyoripotiwa. Ukilinganisha majiji ya Brazili utofauti katika idadi unastaajabisha:

Espírito Santo, o primeiro lugar no ranking, tem índices de 10,3 assassinatos de mulheres por 100 mil habitantes. No Maranhão é de 1,9 por 100 mil. “Os resultados mostram que a concentração de homicídios no Brasil é heterogênea. Fica difícil encontrar um padrão que permita explicar as causas”, afirma o pesquisador Julio Jacobo Wiaselfisz, autor do estudo.

Espírito Santo, Sehemu iliyoshika nafasi ya kwanza, ina kiasi cha mauaji ya wanawake 10,3 kwa kila wakazi 100.000. Huko Maranhão ni 1,9 kwa kila 100.000. “Matokeo yanaonesha mauaji haya yana sababu tofauti. Ni vigumu kupata mtiririko unaoonyesha sababu za mauaji hayo.” Alieleza mtafiti Julio Jacobo Wiaselfisz, mwandishi wa utafiti.

Katika miaka 10 iliyopita, zaidi ya wanawake 41.000 wenye umri kati ya 18 na 30 kutoka kwenye matabaka yote ya jamii waliuawa, mara nyingi wakishuhudiwa na watoto wao ambao pia ni waathirika wa vitendo vya ukatili [pt]. Ukosefu wa huduma za kuwasaidia wanawake walio hatarini unatajwa kuwa ni sababu mojawapo ya kutokushughulikiwa kwa wahalifu licha ya sheria ya Maria_da_Penha iliyotungwa mwaka 2006, ambayo iliwapa wanawake kinga baada ya kuwasilisah malalamiko na kuwahakikishia kuwa wahalifu wataadhibiwa. Hata hivyo [pt],

a nova lei não impediu o assassinato da cabeleireira Maria Islaine de Morais, morta em janeiro diante das câmeras pelo ex-marido, alvo de oito denúncias. Nem uma série de outros casos que todos os dias ganham as manchetes dos jornais.

sheria mpya haikuweza kuzuia mauaji ya msusi Maria Islaine de Morais, aliyeuawa mwezi Januari mbele ya kamera na mtaliki wake, ambaye (Maria) alishawasilisha malalamiko 8 juu yake

Ukatili dhidi ya wanawake, hatuwezi kuzuia!, kwa leseni ya CC

Ni kweli, wengi huuwawa na ndugu zao, waume wao, wapenzi wao, au wanaume waliowakataa [pt].

São casos como negativas de fazer sexo ou de manter a relação. Em 50% das ocorrências, o motivo foi qualificado como fútil, como casos de discussões domésticas. Houve 10% de mortes por motivos passionais, ligados a ciúmes, por exemplo, e 10% relacionado ao uso ou à venda de drogas.

Kukataa kufanya mapenzi au kutaka kuvunja mahusiano husababisah matukio haya. Katika 50% ya matukio sababu zilizopelekea zilionekana kuwa hazina maana, kama vile matukio yaliyotokana ugomvi wa ndani ya nyumba. 10% yalitokana na msongo wa hisia, uanohusiana na wivu, kwa mfano, na 10% yanahusiana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Mizizi ya ukatili inalaumiwa [pt] kwa kuwa sehemu ya utamaduni wa kuwachukia na kuwadharau wanawake ambao umo katika utakia utamaduni wa Brazil:

Essas novelas de violência contra a mulher estão tirando do baú toda a brutalidade contra a mulher brasileira. Expôs as vísceras dessa cultura brasileira tão machista; colocou do avesso o iceberg de uma realidade que costumamos empurrar para debaixo do tapete. Os números dessa violência são tão grande que nos assustam e nos levam a pergunta, se essas ações são de seres humanos!

Hii michezo ya sinema ya matukio ya uhalifu dhidi ya wanawake inadhihirisha kiasi cha ukatili kilichopo dhidi ya wanawake wa Kibrazil. Undani wa utamaduni wa chuki dhidi ya wanawake nchini Brazil unaonyeshwa; barafu ya ukweli tunayoificha chini ya zulia inaonyeshwa. Idadi ya matukio ya kihalifu iko juu kiasi kwamba tunaogopa na kujiuliza hivi matendo haya hufanywa na binadamu kweli!

Kwa mwanablogu Flávia D. [pt] wanawake wenyewe ni sehemu ya tatizo hili. Wamekuwa wakikubali kupewa nafasi finyu na kukandamizwa na wanaume, na mara nyingi huwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wale wanaotenda kinyume na hivyo walivyozoea, ambao wangeweza kupunguza kutokea kwa mtendo haya ya kikatili japo wakati mwingine bila hata kujua. KwaBarbarelas [pt], blogu inayomakinikia kupigana kikamilifu dhidi ya uhalifu wa aina zote, na muhimu jamii yote ikaungana katika vita hivi dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake.

A violência contra mulheres e meninas é algo intolerável, inaceitável, fere a consciência da humanidade, é uma violação aos direitos humanos. Afeta a saúde, reduz anos e qualidade de vida das mulheres. O Brasil, como signatário dos documentos internacionais de direitos humanos das mulheres, e tendo uma legislação nacional a ser cumprida, não pode calar-se e omitir-se. Espera-se de cada autoridade que faça sua parte. E da sociedade, do movimento de mulheres e de homens pela equidade de gênero, que protestem contra estas manifestações do atraso cultural, do machismo e da omissão.

Uhalifu dhidi ya wanawake na wasichana hauvumiliki, haukubaliki, na una haribu utu, pia ni kinyume cha haki za binadamu. Unaathiri afya, unapunguza siku za kuishi na viwango vya maisha ya wanawake nchini Brazil. Brazil, kama nchi iliyotia saini mikataba ya kimataifa ya haki za wanawake, na yenye bunge la kutunga sheria, haiwezi kukaa kimya na kuliacha jambo hili kuendelea. Tuanatarajia kila mamlaka ichukue hatua. Na kwa jamiii, kuwe na harakati za wanaume na wanawake kwa ajili ya usawa wa kijinsia, kupinga ukandamizaji na chuki dhidi ya wanawake.

Wanawake wanaohitaji msaada nchini Brazil wanaweza kupiga simu bure kwenda namba 180 ili kutoa taarifa ya ukatili au uhalifu dhidi yao au kupuuziwa kokote na mamalaka kwa malalamiko yao. Habari hizi zimepatikana kwenye blogu ya Contra Machismo ambaye alikuwa akiwakumbusah wasomaji kuhusu makala yake yenye kichwa Ukatili dhidi ya wanawake nchini Brazil bado unatokea kila siku..

Soma habari za kufanana nayo Brazil: mdahalo wa ukatili dhidi iliyoandikwa na Diego Casaes katika mtiririko wa makala maalumu katika kukuza uelewa juu ya siku ya kimataifa ya kutokomeza uhalifu dhidi ya wanawake (Novemba 2009).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.