Colombia: Mockus na Fajardo Waungana kwa Ajili ya Uchaguzi wa Rais

Mgombea urais wa Kolombia Antanas Mockus, wa Chama cha Kijani [es], ametia muhuri ushirika na aliyekuwa Meya wa Medellín, Sergio Fajardo, ambaye atakuwa mgombea mwenza wake wa nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Uchaguzi wa Tarehe 30 Mei mwaka 2010. Wote wamewahi kuwa mameya wa majiji makubwa ya Kolombia, Bogotá na Medellín. Wakolombia wengi wanaamini kuwa walikuwa na utawala wa uwazi wakati wa enzi zao kama mameya.

Muungano huu umekubalika na Wakolombia wengi, kama ilivyonekana kwenye kura za maoni. Hata hivyo, ulimwengu wa kublogu nao hauko mbali katika hilo. Hapa ni baadi ya maoni yanayoakisi ni kwa jinsi gani muungano huu unaonekana mtandaoni.

Picha ya Antanas Mockus na Gó Me Z na imetumika kwa kibali cha Creative Commons.

Picha ya Antanas Mockus na Gó Me Z na imetumika kwa kibali cha Creative Commons.

Kwa kuanza, Álvaro Ramírez katika gazeti la kidijitali EquinoXio [es] anaandika kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kama timu:

La renuncia que ha hecho Fajardo a su ambición individual de ser presidente ahora, es significativa porque revela con mayor claridad el revolcón que está transformando a estos ex-alcaldes en políticos cada vez más sagaces e inteligentes. Entendieron que sin estructuras sólidas, sin organizar a sus seguidores y sin tomarse el tiempo y el esfuerzo de construir movimientos políticos y partidos con perfiles ideológicos coherentes, no era posible hacer los cambios profundos que Colombia necesita.

Fajardo sasa ameachana na nia yake binafsi ya kuwa rais, ambalo ni jambo muhimu kwa sababu linaonesha wazi zaidi mabadiliko katika matukio ambayo yanawageuza hawa mameya wa zamani kuwa wanasiasa na jinsi wanavyosidi kuwa makini na uelewa zaidi. Wanaelewa kuwa bila ya kuwa na miundo imara, bila kuwapanga wafuasi wao na bila kuchukua muda na kujenga makundi ya umma ya kisiasa pamoja na vyama vyenye itikadi imara, haitawezekana kuleta mabadiliko ya msingi ambayo kolombia inayahitaji.

Juanita León kutoka kwenye La Silla Vacía [es] anatoa mchanganuo wa mabadiliko yatakayo wanufaisha wafuasi katika kampeni za Mockus na anarudia kueleza utambulisho wa pande hizo 2 kwa sababu hakuna tofauti ya maana katika itikadi zao:

Antanas Mockus y Sergio Fajardo tienen muchas afinidades: ambos son matemáticos, fueron alcaldes exitosos, creen en la importancia de la transparencia de los medios para conseguir los fines en la política. Pero tienen menos complementariedades.

Antanas Mockus na Sergio Fajardo wanafanana kwa mengi: wote ni wana hisabati, wote ni mameya waliofanikiwa, wanamini katika uwazi kama njia pekee ya mafanikio katika utwala wa kisiasa. Hata hivyo, wana vichache vya kuongezeana.

Blogu ya pamoja ya Koestler, Reflexiones Desde Lebrija [es] amefurahishwa na muungano huu, lakini wakati huohuo amekosoa mchezo mchafu unaoonekana katika upigaji kura unaoendelea nchini Colombia:

Un claro ejemplo es el de Datexco, que repitió la encuesta… hasta que aparecía ganándola Juan Manuel Santos.

Sí: es que definitivamente hasta en eso se tiene que engañar a la gente. Porque la encuesta de Datexco la ganó Mockus, pero había que ocultarlo al pueblo.

Mfano mzuri ni kuwa Datexco, ambayo ilirudia utafiti… hadi pale ilipoonekana kuwa (mgombea) Juan Manuel Santos anashinda.

Ndio: ni dhahiri kuwa wanafanya hivi ili kuwachanganya watu. Kwa sababu katika utafiti wa Datexco, Mockus alishinda, lakini walitaka kuyaficha matokeo.

Mapema mwaka 2010, Mockus alitangaza kuwa ana ugonjwa wa Parkinson, ugonjwa ambao alisema kuwa anaudhibiti kwa kutumia dawa na ambao upo kwenye hatua za mwanzo. Hata hivyo, baadhi ya wapinzani wamekuwa wakitupia macho zaidi kwenye ugonjwa wake. Víctor Solano katika blogu yake ¿Comunicación? [es] anachanganua habari ambazo wanahabari wa kituo cha Caracol [es] walitaka kuzitumia katika kuiharibu sifa ya Mockus, akikabiliana na mmiminiko wa kundi kubwa la wafuasi wa muungano unaoongozwa na Mockus, na akauliza:

Sinceramente me sentí muy triste, no tanto por la salud del candidato porque sé que Mockus es fuerte, gallardo, honesto y porque con medicación podrá atenuar los efectos de su padecimiento; me sentí triste al ver que tengo colegas en la radio que atentan contra la dignidad de los candidatos, que buscan los presuntos talones de Aquiles en la necesidad de menoscabar a las personas y no a los hechos.

Kwa kweli, nilipatwa na huzuni, sio ktuokana na afya ya mgombea kwa kuwa nilijua kuwa Mockus ni imara, jasiri, mkweli, na kwa sababu matumizi ya dawa yanaweza kupunguza madhara ya ugonjwa; nilijisikia huzuni kwa kujua kuwa nina wenzangu kwenye radio ambao wanadhalilisha heshima ya wagombea kwa kutafuta mambo yatakayowaumiza ili kuwadhalilisha watu badala ya kutafuta ukweli.

Superuser kwenye blogu ya Tu Web Florida [es] anachambua faida na hasara za muungano huu. Hata hivyo, amehitimisha kwa uzuri wake hatimaye:

Hay quienes interpretan eso como una debilidad a la hora de administrar un país, pues las funciones son más complejas. Por ejemplo, la política de relaciones exteriores es de manejo exclusivo del Gobierno central; la actuación del Presidente y del Banco de la República es determinante en la economía; a esto se suma que la seguridad y la defensa de la nación son del fuero del más alto nivel del Ejecutivo. En otras palabras, una cosa es administrar una ciudad y otra un país.

Sin embargo, las ciudades en las que fueron alcaldes Mockus y Fajardo son las más importantes del país, y en buena medida, sus administraciones representan desafíos debido a la complejidad de sus problemas.

Baadhi ya watu hutafsiri hii kama udhaifu wakati wa kuongoza nchi, kwa sababu kazi ni ngumu zaidi. Kwa mfano, siasa za uhusiano wa kimataifa hufanywa zaidi na Serikali kuu; kazi ya Rais na Benki ya Jamhuri ni muhimu katika uchumi, katika hili ongeza ulinzi na na usalama wa taifa zipo chini ya mamlaka ya ngazi ya juu ya utawala. Kwa maneno mengine, kuongoza jiji na kuongoza nchi ni vitu viwili tofauti.

Hatahivyo, majiji ambayo Mockus na Fajardo walikuwa meya, ni majiji makubwa zaidi nchini, na yanawakilisha changamoto kubwa kwenye utawala kutokana na ukubwa wa matatizo yake.

Katika mitandao ya kijamii, muungano huo umekuwa ukipata kuungwa mkono sana na wafuasi wake wanaotengeneza makundi mbalimbali. Kati ya yenye uwakilishi mkubwa zaidi, lipo moja katika Facebook lenye jina “Antanas Mockus na Sergio Fajardo kwa ajili ya Urais wa Jamhuri [es]” lenye wafuatiliaji zaidi ya 65,000. Tovitu hii inaratibiwa na na watu wanaojitolea kusaidia kampeni za kwenye mtandao. Kuna maoni mawili moja yanayoonekana kwenye tovuti hiyo, moja linamuunga mkono Mockus na jingine linampinga:

Juan Daniel Cruz Podríamos ahorrarnos 60.000 millones de pesos: lo que vale la segunda, si elegimos a Antanas en primera vuelta. Pongamos esta información en el estado de Facebook este sábado 17 de Abril, tener el mejor presidente nos sale muy económico, igual que la campaña que manejo durante su candidatura, manifestémonos y apoyemos esta campaña el 17 de abril.

Aragon de gondor. nadie habla del contrato de Mockus, en su primera alcaldía con Ica de México para repavimentar la malla vial de Bogotá. No se ejecutó ni el 40% hoy no se ha recuperado el dinero del distrito, sigue el pleito y el experto estadista, de candidato a la presidencia….ver más ilusos.

Juan Daniel Cruz: Tunaweza kupata pesomilioni 60,000: ambazo ni sawa na gharama za uchaguzi, kama tutamchagua Antanas katika mzunguko wa kwanza. Hebu tuweke taarifa hii kwenye Facebook Tarehe17 Aprili, ili kupata rais bora ni matokeo ya kiuchumi zaidi, kama zilivyo kampeni zilizoratibiwa wakati wa kampeni hebu tutamke na kusaidia kampeni hii Aprili 17.

Aragon de Gondor: Hakuna anayezungumzia mkataba wa Mockus na Ica wa Mexico wakati wa kipindi chake cha kwanza kama Meya. Mkataba ulikuwa wakukarabati mtandao wa barabara wa Bogota. Hata asilimia 40% za malengo hazikufikiwa na pesa za kutoka wilayani hazijarudishwa, na ugomvi bado unaendelea na na mwanasiasa huyo, kutoka kuwa mgombea hadi urais…. Ona maajabu zaidi

Japo kuwa wanablogu wengi wa Kolombia wanaupenda muungano huu, wapo baadhi walio tofauti kama vile Saúl Hernández, ambaye amechapisha katika blogu yake Opinet [es], na ambayo ilitokea pia kwenye El Tiempo. Katika blogu yake binafsi, ilimbidi kufunga sehemu ya maoni kwa sababu wafuasi wa muungano wa Mockus na Fajardo wanaandika kwa wingi kujibu ukosoaji mkali wa Hernández kuhusu vijana wa Kolombia wanaounga mkono kampeni, na kuwaita kama watoto wasiopevuka:

Esos inconformes, entre ellos muchos jóvenes con su típica inmadurez política, buscan algo peor que el mesianismo y el caudillismo que tanto critican, como son las salidas utópicas. Buscan el Obama colombiano que acabe con la corrupción, la pobreza, la violencia, el desempleo y la ignorancia; que legalice las drogas, que haga las paces con Chávez, que haga el intercambio humanitario, firme la paz con las guerrillas y logre otras enormidades de ese calibre.

Wale wasiokubaliana na utaratibu wa jamii, kati yao wapo vijana wengi ambao hawajakomaa kisiasa, wanatafuta kitu kibaya zaidi ya umasiha au utawala wa kiimla wa kijeshi (caudillism), kiasi kwamba wanakosoa, sawa na mwenendo wao wa kufikirika. Wanatarajia kupata Obama wa Colombia ambaye atamaliza rushwa, umasikini, fujo, kukosekana kwa ajira na ujinga. Wanataka utumiaji wa madawa ya kulevya uwe halali, waweze kuelewana (Hugo) Chávez, kuweka mkataba wa amani na waasi wa msituni na kufikia malengo mengine kadhaa ya aina hiyo.

Jorge Luis Rocha, mwenye umri wa miaka 19, ana ari kubwa, kitu kunachoonekana kwa vijana wengi Wakolombia kuhusu muungano huu. Anaandika katika blogu yake CP ¡Cuántas Palabras! [es]:

Por estas pocas razones (comentemos muchas más!) la unión Fajardo-Mockus da aires de esperanza para vivir en otra Colombia y sentirse (personalmente, por primera vez) orgulloso de esta tierra. No sería raro que, como Barack Obama, Mockus gane inesperadamente la presidencia en Colombia. Tenemos con qué ganar. Tenemos monopolizados las redes sociales, trabajamos con bajo perfil, le hacemos ver otras cosas a la gente… somos activos. Somos activos en medio de otros políticos que se dedican a darle largas a peleas mediáticas infantiles. Sé, y tengo la ilusión, de que a partir del segundo semestre de 2010 habrá un presidente no conservador, no Uribista, sino independiente.

Kwa hizi sababu chache (na tuzihesabu nyingine nyingi!) umoja huu wa Fajardo na Mockus unatupa matumaini ya kuishi kwenye Kolumbia tofauti na kujisikia (binafsi kwa mara ya kwanza) majivuno kwa nchi yangu. Haitakuwa ajabu, kama vile Barack Obama, Mockus akishinda urais Kolombia bila kutarajiwa. Tuna uwezo wa kushinda. Ni lazima tuutawale mtandao wakijamii, tufanye kazi kimya kimya, tuwafanye watu wauone upande mwingine… tupo hai. Tupo hai kati ya wanasiasa wengine waliojiingiza kwenye michezo ya kitoto ya kupambana katika vyombo vya habari. Najua na nina matumaini kwamba kuanzia nusu ya pili ya mwaka 2010 kutakuwa na rais asiyekuwa mhafidhina, asiye wa mlengo wa Uribe, bali anayejitegemea.

Mwisho, wagombea hao wawili hawajajikita sana kwenye kampeni, na wamejaribu kutumia vyombo vya habari kama hivi. Waratibu wakujitolea wamekuwa wakituma barua pepe zenye ujumbe , “kaulimbiu – umoja ni nguvu, waliokuwa meya wametangaza jambo la muhimu katika kampeni nalo ni utamaduni wa raia, elimu na utu”

Kampeni za Uchaguzi wa rais utakuwa wa ushindani na wakuvutia, na lipo tumaini kwamba raia wengi watashiriki ili kutimiza haki yao ya kupiga kura Tarehe 30 Mei.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.