Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia

Santiago baada ya tetemeko la ardhi na pviojo CC-By

Santiago baada ya tetemeko la ardhi na pviojo CC-By

Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.

Kuna video zilizotengenezwa wakati wa tetemeko lenyewe, kama vile video hii ya ridhaa iliyokutwa kwenye YouTube. Inaanza kwa picha ya kompyuta kwenye chumba, na wakati ardhi ilivyokuwa ikisogea mingurumo ya ardhi inaweza kusikika, halafu taa zilizimikana tunaachwa kwenye giza, na kusikia sauti pekee ya mwanamke na mwanaume ambaye tunadhani ndio aliyekuwa amebeba kamera akijaribu kumtuliza.

Inayofuata ilirekodiwa na mtumiaji wa YouTube ikonsento wakati wa moja ya matetemeko yaliyofuatia.

Ikonsento amekuwa akiripoti tangu dakika chache baada ya tetemeko la kwanza, wakati alipopakia video zinazoonyresha jinsi nyumba yake ilivyobaki: jinsi samani zilivyoseleleka kwenye sakafu na kupinduka kama ushahidi wa nguvu za tetemeko hilo:

Video hii ilitengenezwa dakika chache baada ya tetemeko, na hii inayofuata ambamo wanaume wawili ambao ndio kwanza walikuwa wamewasili nchini Chile walivyoshuhudia tetemeko la ardhi na baadaye waliamua kutoka ndani ya jingo lao na kusimama nje kwa muda mfupi. Wakati taa zilipowaka tena katika jingo lao, walirudi tena na wakazi wa jingo hilo wanajumuika barazani, na walivyokuwa wakirejea kwenye jingo, na kukagua uharibifu: mabomba ya maji yaliyovunjika na zege lililopata ufa.

Wakati mwanga wa asubuhi ulipotoka, watu zaidi walielekea mitaani na kurekodi madhara waliyoyaona:

Netprox aliendesha kwenye barabara kuu, na ilimbidi ajipenyeze chini ya darakja lililoporomoka ili aweze kupita.

Rafael Vial pia alikwenda mitaani na kurekodi daraja lililoanguka huko Llaillay, Chile, amblo alilionyesha kwa kupitia simu yake ya mkononi katika Qik.

Mawasiliano katika sehemu nyingi za Chile yako chini na inazidi kuwa vigumu kuwasiliana na wapendwa ili kuhakikisha kuwa wako salama. Wasichana hawa wawili walitumia YouTube na kurekodi video yao, ambayo kwayo wanawaeleza rafiki na ndugu zao kuwa wapo salama, na kueleza kidogo yale waliyoyaona na kusikia kuhusu tetemeko hilo la ardhi:

Na wengine, katika haja yao ya kusaidia wanasambaza habari muhimu zinazohusu nini cha kufanya ili kukuza uwezekano wa kuweza kuendelea kuishi chini ya jingo lililoporomoka. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye video ambayo ilisambazwa baada ya tetemeko. Nadharia ya Pembe Tatu za Maisha inaeleza kimsingi kwamba sehemu nzuri ya kujikinga wakati wa tetemeko siyo chini ya samani, bali pembeni ya samani imara; kwa njia hiyo, ikiwa kipande cha samani kitavunjwa na vitu vinavyoporomoka, hakitamuangukia mtu aliyejikinga chini yake. Na badala yake, mtu huyo atakuwa salama katika nafasi iliyojitengeneza pembeni ya samani. Hii ni video ya matangazo ambayo iliasiliwa na kutafsiriwa kwa Kihispania, inafafanua kwa nini kujikinga chini ya madawati au chini ya milango hakutakunusuru.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.