Sudani: Je, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Itafanya Kazi?

Katika makala ya Global Voices ya Disemba 2009 yenye kicha “ICT4D: Makosa Ya Nyuma, Na Busara za Baadaye” Arpana Ray anaonyesha kuwa miradi mingi ya teknolojia kwa ajili ya maendeleo “ilianza kwa kishindo na baadaye kufariki kwa kilio.” Kwa mujibu wa makala ya hivi karibuni kwenye jarida la the Financial Times, hiyo ndiyo hatima ya mpango wa mamilioni uya dola wa Benki ya Dunia wa kusambaza kompyuta na upatikanaji wa intaneti huko Juba, mji mkuu wa Sudani ya Kusini.

Kwa mujibu wa Lawrence Clarke, ambaye anaongoza programu ya Benki ya Dunia nchini humoambaye alihojiwa kwa ajili ya makala hiyo, kushindwa huko hakukutokana na kukosekana kwa vifaa au vitendea kazi. Badala yake, tatizo ni kukosekana kwa nia:

Lawrence Clarke, kiongozi wa programu ya Benki hiyo huko Sudani ya Kusini, anafafanua kuwa fungu la fedha lilitumika kununulia kompyuta, programu na vifaa vya setilaiti mjini Juba, mji mkuu uliochoka sana wa Kusini. Lakini “kila aina ya matatizo yalianza kujitokeza,” anasema…

“Baadhi ya mawaziri waliamua kuwa walikuwa wazee sana kuanza kujifunza kutumia kompyuta, na hawakuonyesha hamu yoyote.” katika visa vingine hata wasaidizi wenye umri mdogo hawakuwa wanafamu jinsi ya kujiandikisha, “Kwa hiyo kifaa kiko pale… kinakufa,” Anasema Bw. Clarke.

Msukumo wa hivi karibuni wa upatikanaji wa simu za mkononi na upatikanaji wa intaneti umechochea hamu ya kutosha kwenye matumizi ya teknolojia kwa ajili ya kila kitu kuanzia utafutaji masoko na biashara ya kwenye wavuti mpaka ufuatiliaji wa magonjwa ya mazao na kuwakumbusha waathirika wa VVU/UKIMWI na wagonjwa wa kifua kikuu wanywe dawa zao. Lakini taarifa kutoka Sudani ya Kusini zinazua swali: kelele zinazoambatana na teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) zinaweza kuhalalishwa? Na ni kwa vipi akina sisi ambao tunafanya kazi kwenye nyanja hiyo tunaweza kuhakikisha kuwa jitihada zetu hazitaishia katika kifo cha kujiozea chenyewe?

Kama mtafiti wa Mtandao wa Teknolojia ya Uwazi, ninavutiwa hasa katika njia ambazo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano zinaweza kusaidia kuwashirikisha raia katika utawala wan chi yao na kuhamasisha serikali kuwa na uwazi pamoja na uwajibikaji. Miradi mingi imefanikiwa kutumia teknolojia kwa ajili ya uwazi; mapitio ya hivi karibuni ya David Sasaki ya tafiti nane za kwanza za mtandao huo zinaonyesha hivyo. Lakini, kama hali ya mambo huko Juba inavyoonyesha, teknolojia huwa haipelekei utawala bora kimiujiza.

Mwanablogu wa Sudani na mwandishi wa Global Voices Drima anaamini kuwa intaneti na simu za viganjani havitoshi. “Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni teknolojia tu. Manufaa yake ni jambo ambalo linaweza kufikiwa ikiwa watumiaji wake watatumia teknolojia kwa ustadi ili kufikia lengo zuri,” anaandika katika barua pepe.

Ili tekonolojia ilete mafanikio, Drima nasema, miundo mbinu inayosaidia si lazima itoke kwa wafadhili, bali itoke ndani (ya jamii husika):

“Inapofikia suala la tabia na malengo, hilo ni suala ambalo Wasudani ya Kusini inabidi walitafutie ufumbuzi. Na kabla hata ya kuingia kwenye hii dhana ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuwa kana kwamba ni ‘risasi ya fedha’ inatubidi tushughulikie masuala mengine mengi yanzyotuzingira, kuanzia utawala potofu na ukabila angamizi.”

Wakati Sudani inaelekea uchaguzi mwezi Aprili, teknolojia ina uwezo wa kucheza nafasi kubwa katika kuwashirikisha raia na katika kufuatilia mchakato wa kisiasa. Sudani Inapiga Kura, tovuti ya lugha mbili inayodhaminiwa na shirika la Kijerumani Media in Cooperation and Transition pamoja na mashirika ya Sudani Teeba Press pamoja na Jumuiya ya Vyombo vya Habari, vinatarajia “kuboresha viwango vya habari za uchaguzi” na “kuhamasisha uelewano mzuri palipo na vikwazo vya lugha.” Tovuti hiyo ina makala zenye mada tofauti kuanzia siasa mpaka afya na utamaduni, pia Kurasa ya Uchaguzi wa Sudani ili kuwasaidia raia kujifunza zaidi kuhusu vyama vya siasa nchini humo.

Sudani Inapiga Kura

Sudani Inapiga Kura



Tovuti ya Ufuatiliaji Kura Sudani
, inayoongozwa na Taasisi ya Sudani ya Utafiti na Sera, imepanga kutumia Ushahidi ili kuwawezesha raia wake kufuatilia na kuripoti juu ya uchaguzi.

Tovuti ya Ufuatiliaji Kura Sudani

Tovuti ya Ufuatiliaji Kura Sudani

Katika uchaguzi ambao “raia wengi hawana ufahamu wa karibu wa michakato ya msingi ya uchaguzi, wanapinga ushindani wa vyama vingi na wana mashaka kama uchaguzi utakuwa wa haki,” miradi hii inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuwaelimisha watu na kuorodhesha matatizo yanayoweza kujitokeza katika mchakato wa upigaji kura. Ili kuwa na mafanikio, hata hivyo, kwanza ni lazima wapate njia ya kuwashawishi raia juu ya umuhimu wake.

Vyote, Sudani Inapiga Kura na Ufuatiliaji wa Uchaguzi Sudani zinaonekana kuwa na ushiriki wa maana wa Wasudani katika ngazi za chini, ambao unaweza kuwasaidia pale ambapo programu ya Benki ya Dunia imeshindwa. Huku uchaguzi unazidi kukaribia, nitakuwa naangalia kwa Karibu ili kuona jinsi mashirika haya yanavyoendelea. Je watashindwa vibaya, hayatatiliwa maanani na kutotumiwa na Wasudani? Au wataweza kutafsiri tekenolojia kuwa ushirikishwaji wa umma wa kweli?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.