Misri: Sisi Ni Washindi

Timu ya kandanda ya Misri iliifunga Ghana katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na ikapata ushindi wake kwa mara ya tatu mfululizo. Huu pia ni ushindi wa saba tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo kwenye miaka ya hamsini. Wanablogu wanaungana na wananchi wa nchi hiyo kusherehekea mafanikio hayo.

Zeinobia aliandika hapa kuhusu ushindi huo kwa Misri akisema:

Tulicheza mchezo mzuri dhidi ya Ghana, na mwishowe Gedo akawa sababu ya kuwafanya karibu ya Wamisri milioni 80 kufurahi duniani kote, akawaunganisha pamoja katika wakati huo adimu bila kujali maana yake ya kisaikolojia au maana ya kisiasa au vyovyote. Kocha Hassan Shehata anasisitiza kuwa mmoja wa Makocha wazuri zaidi sio tu kwenye historia ya kandanda la Misri, lakini pia katika historia ya Afrika. Mtu huyu ameweza kufanya jambo kubwa kutokana na timu yetu kwa hakika. Kumgundua yeye Mohamedi Nagi ama kwa jina jingine Gedo Ahmed Hassan ilikuwa ni ajabu sana. Wachezaji wote walikuwa vizuri sana.

Ushindi haukusherehekewa tu hapa Misri. Huko Qatar, Qatar Living aliandika hapa kuhusu ushindi huo, na akategemea watu kukesha usiku kucha huko Doha:

Misri imeichapa Ghana 1-0 kujivika taji la Kombe la Afrika…
Mod anaandika: Itakuwa ni usiku wa kelele nyingi mjini Doha! Hongera kwa Wamisri wote waishio Qatar!

Mwanablogu wa Misri aishiye Marekani, Egyptian Wish, aliandika kwenye posti yake mpya hapa akisema:

Wapendwa Wamisri,
Hongereni sana kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2010!
Mmisri aliye Marekani

Pia nchini Palestina, Hamas hawakuiacha fursa hiyo ipite, na kuwapongeza Wamisri kwa Ushindi wao huo wa saba. Kelmety aliandika kuhusu hilo hapa:

قدمت حركة حماس التهنئة لمصر رئيسًا وحكومة وشعبًا لحصولها على لقب “بطولة كأس الأمم الأفريقية” السابعة والعشرين للمرة السابعة فى تاريخها والثالثة على التوالى

Hamas imempongeza rais wa Misri, serikali na watu kwa kushinda kwa mara ya saba Kombe la Mataifa ya Afrika, na ushindi wao huo wa tatu mfululizo.


Zeinobia
aliandika posti nyingine hapa, kuhusu wana wa Rais wa Misri, ambao walikwenda Angola kuishangilia timu yao ya soka ya Misri:

Ninaamini kwamba picha za vijana wa Mubarak inabidi ziwe na posti yake ya kujitegemea. Kama nilivyogusia hapo awali, hawa vijana walienda Angola kutazama mechi ya Fainali kati ya Misri na Ghana. Watu wengine wanaweza kulichukulia hili kama suala la kisiasa la kutafuta umaarufu, wengine wakijua jinsi vijana hawa walivyo na ‘ulevi’ wa mpira.

Mwanablogu mwingine, My Oblivia, alikuwa na mtazamo tofauti hapa:

Kwa hiyo, je kuna mtu atakayeweza kujisumbua tafadhali kueleza ni namna gani shindano moja la kizembe linatufanya kuishangilia nchi hiyo hiyo ambako haya yaafanyika…

Katika nchi hii watu wanakufa kwa njaa, wanakufa kwa kuteswa, wanakufa tu kwa sababu hawana hata nusu ya mahitaji ya misingi kwa ajili ya kuishi na hawana huduma za matibabu, acha ile tu kujua kama wanahitaji…

Kwa Mungu hakutaka sisi tushinde vita vyetu vya kila siku vya kule tu kubaki hai, badala yake, Ametupangia kushinda mpambano wa kandanda, ana mashindano yote, haleluya, tumeokolewa!
Kwa hivyo, huu ni ushindi wetu tuliopangiwa, kwenye kandanda…
Na sasa, matatizo tyote mengine yametatuliwa na tumebarikiwa milele!

Na hatimaye, timu ya kandanda ya Wamisri mara nyingi humwongeza nyota mwingine kwenye jezi zao kila mara wanaposhinda Kombe la Mataifa Ya Afrika. Lakini Adel Ghaly alikuwa akijiuliza hapa kama tuna nafasi imebaki kwa ajili ya nyota mwingine:

بينما كنت أعدد المكاسب التى خرج بها المنتخب المصرى من مشاركتة هذا العام بأمم افريقيا التى اقيمت فى انجولا وجدتها لاتعد ولا تحصى بالنسبة للاعبين والجهاز الفنى وتاريخ الكرة المصرية ………..
ولكن وجدت مشكلة عويصة ستقابل المنتخب بعد هذا الفوز وهى ان المنتخب الان اصبح يمتلك 7 نجوم يرمزون الى 7 بطولات افريقية أين سيضع كل هذة النجوم على فانلة المنتخب المليئة بالنجوم ؟!

Nilipokuwa nikihesabu faida za kushiriki masnindano ya mwaka huu, nikakuta kwamba wachezaji, kocha, na historia ypote ya kandanda imefanikiwa kwa mafanikio yasiyolinganishwa. Lakini kuna tatizo moja hapa: tunawaweka wapi nyota wote hao wa jezi za timu yetu ya taifa sasa ambapo tumetwaa ubingwa huu wa saba.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.