Costa Rica: Video za Mtandaoni Zaongeza Vichekesho Katika Uchaguzi wa Rais

(makala hii iliandikwa kwanza tarehe 03-02-2010)

Picha imepigwa na thombo2 na fick wameitumia kwa mujibu wa lesini ya CC

Picha imepigwa na thombo2 na fick wameitumia kwa mujibu wa lesini ya CC


Uchaguzi wa Rais wa Costa Rica unafanyika Jumapili hii na kwa kupitia video, wananchi wengi wa Costa Rica wanatoa hisia zao kuhusu wagombea na mustakabali wa nchi yao kupitia vichekesho na utani.

Kwanza, tuna video ya mtandaoni iliyopandishwa na El Basureo, ambamo wanapendekeza utatuzi wa maana kwa tatizo kongwe la muda mrefu la kutokujua nani wa kumpigia kura. Katika uchaguzi huu wa Costa Rica, kati ya wagombea 6 wanaokilimbia ikulu, wanne wao wako mbele: Laura Chinchilla wa Chama cha NL, Otto Guevara wa chama Liberty, Otton Solis wa chama cha Socialdemocrat na Luis Fishman wa Social Christian. El Basero amapendekeza mashine mpya ambayo itachanganya na kuoanisha sifa za wagombea, na majina yatakayotoka baada ya mchanganyiko huo yatakuwa sawia kwa hali ya kisiasa ya Costa Rica.

Video za mtandaoni zinajinadi kama njia ya kutangaza habari na propaganda za kusikiliza na kuona ambazo mara nyingine huondolewa kwenye runinga baada ya muda mfupi. Mfano wa hayo ni suala la kampeni za mgombea Finshman zilizohusisha watu waizma waliovaa kama watoto waliovaa nepi huku wakicheza na kupiga kinanda, wakina mama wajawazito na ala inayofahamiaka sana ya kaulimbiu ‘Fishman, zimwi likujualo.’ Imekuwa kawaida kuona madudu haya, kama hii hapa inayofuata. Kitu pekee ambacho kimebadilika ilikuwa ni sauti na vichwa vya habari, yaliyobaki yote yaliachwa yalivyo:

LaErre.tv pia walikuja na mtazamo wao wa uchaguzi: nyenzo yenye maelezo yote ya Mgombea Urais,ina kila kitu ambacho unaweza kukihitaji ili kujiingiza kwenye siasa. Wakiwa na sentesi za mwanzo zinazosema: Kama umechoka ahadi za wagombea wengine, na kule kupelekwa jela unapoiba, kwanini usiwe mgombea wewe mwenyewe na kushughulikia matatizo yako mwenyewe? Inaendelea kueleza mbinu zinazotakikana, maneno unayohitaji faraja utakayokuwa nayo mara unapopata vifaa vyao na kufuatilia hatua za maelekezo.

Elchamukocr vilevile anaweka video akimtania Otton Solis, ambaye wakati wa kampeni ilibidi asitishe kwa muda ili kuomba michango ili kuendelea na kampeni zake za kwenye runinga kwani mfuko wake ulikuwa umekauka. Katika video, Otton anaratibu kile kinachoitwa teleotton yaani ‘mtangaze otton kwenye runinga’ ili kutunisha mfuko:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.