Chile: Tetemeko Kubwa la Ardhi lenye Ukubwa wa 8.8 Laikumba Chile

Saa 9:34 usiku kwa saa za Chile, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.8 liliukumba mwambao wa eneo la Maule nchini Chile. Tetemeko hilo liliutetemesha mji mkuu wa Santiago uliopo Kilomita 325 kutoka katika kiini cha tetemeko hilo. Uharibifu mkubwa umeripotiwa nchin nzima, na idadi ya waliofariki inazidi kwenda juu. Kwa siku nzima, matetemeko madogo madogo yaliyofuatia yalilitetemesha eneo hilo.

Blogu ya Terremoto Chile [es] (Tetemeko la ardhi Chile) iliundwa haraka na Fransisco mara baada yua tetemeko kutokea. Na zaidi ya kuchapisha mapendekezo kuhusi nini raia wanachotakiwa kufanya kufuatia tetemeko la ardhi [es], amekuwa akikusanya na kupanga picha mbalimbali za Twitpic.

Picha ya uharibifu uliolikuta Kanisa la Nuestra Señora de la Divina Providencia mjini Santiago. Iliyopigwa na Julio Costa Zambelli na kutmika kwa leseni ya Creative Commons.

Picha ya uharibifu uliolikuta Kanisa la Nuestra Señora de la Divina Providencia mjini Santiago. Iliyopigwa na Julio Costa Zambelli na kutmika kwa leseni ya Creative Commons.

Karibu na kiini cha tetemeko, Robinson Esparza wa gazeti la kiraia la El aMaule [es], ambalo ni sehemu ya mtandao wa Diarios Ciudadanos [es] amekuwa akiweka habari mpya kadri zinavyotokea kutoka katika habari mpya za kanda na taifa [es]. Maoni mengi yamekuwa ni ya hofu juu ya wanafamilia walio kwenye maeneo ya nje ya mji mkuu, na ukosefu wa mawasiliano umeendelea kuwa suala gumu kwa ndugu wanaojaribu kuwasiliana na familia pamoja na marafiki katika sehemu ambazo nyaya za umeme na simu zimeathirika. Ign. Rodríguez de R. (@micronauta) anaandika kuhusu usumbufu huu:

tratando horas d comunicarme con familia en Valparaíso, la red fija telefónica VTR es desastrosa, no se les debería permitir dar servicio :@

najaribu kwa masaa kuwasiliana na fimilia iliyopo Valparaíso, njia ya simu za kawaida (za shirika la simu) VTR ni janga, wasiwaruhusu kutoa huduma :@

Wale ambao wamekuwa wakiandika makala kwenye blogu ya Terremoto Chile pia wametengeneza akaunti ya Twita inayoitwa Ayuda Chile [es] (Saidia Chile) ambayo kwayo taarifa kutoka kwa watumiaji wengine wa Twita ambao wanatafuta ndugu zao zinazukusanywa na kutumwa trena kwenye twita. Watumiaji wengine wa Twita kama vile Pablo González Carcey wamejitolea kuwapigia simu ndugu [es] wa watu kama Daniela Alvarado ambaye hakuweza kumfikia kaka yake aliye Chile. Anafuata:

@DaniAlvaradoA hice los llamados y tu familia esta bien! Abrazos

@DaniAlvaradoA, Nimepiga sim una familia yako ipo salama! kumbato

Baada ya kukucha, picha nyingine za uharibifu zilianza kutokea kwenye mtandao. Claudio Olivares alikwenda kuvinjari kwa miguu jijini Santiago ili kuangalia uharibifu na kupakia picha kwenye Owly, kama vile alivyofanya Costanza Campos, ambaye alipiga picha kadhaa za uharibifu kwenye makanisa ya Santiago.

Mtumiaji wa YouTube Franciso Vivallo Sainz alichukua video ifuatayo ya kuporomoka kwa ghorofa katika minara ya Bilbao katika kitongoji cha Las Condes jijini Santiago:

Tayari kuna tahadhari kuhusu Tsunami iliyotolewa na Kituo Cha Pasifiki cha Maonyo ya Tsunami kwa ajili ya maeneo yanayopakana na bahari ya Pasifiki.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.