Uganda: Rais Kuzuia Muswada Unaopinga Ushoga

Muswada Unaopinga Ushoga wa 2009 uliopendekezwa nchini Uganda bado unasubiri uamuzi wa mwisho utakaotolewa na bunge la nchi hiyo, lakini gazeti la Daily Monitor lilitaarifu Jumatano kuwa Rais Yoweri Museveni “ameihakikishia Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani nia yake ya kuukwamisha muswada huo”:

Imetaarifiwa kuwa Rais Museveni amehakikishia mamlaka ya Marekani kuwa atapiga turufu muswada uliopendekezwa na mbuge wa Ndorwa David Bahati dhidi ya ushoga, msimamo ambao unavunja msimamo wake wa hivi karibuni na matamko ya maofisa walio katika serikali yake.

Wanaharakati waliokusanyika nje ya ubalozi wa Uganda katika umoja wa Mataifa mjini New york mwezi Novemba ili kuupinga muswada.Picha kwa hisani ya riekhavoc riekhavoc kwenye Flickr

Wanaharakati waliokusanyika nje ya ubalozi wa Uganda katika umoja wa Mataifa mjini New york mwezi Novemba ili kuupinga muswada.Picha kwa hisani ya riekhavoc riekhavoc kwenye Flickr

Mwanablogu Gay Uganda anaonyesha utata katika matamko ya serikali ya Uganda kwa nchi za Magharibi na kwa Waganda wenyewe:

Unakumbuka makala inayohusu Rais alipothibitisha kwa Idara ya Nchi ya Marekani kuwa muswada huu hautakuwa sheria?

Naam, anasema hivyo kwa Wamarekani. Na hivi ndivyo serikali inavyosema kwa Waganda.

Msimamo wa serikali dhidi ya ushoga bado unasimama, anasema waziri
Katika tamko lililotolewa jana, Waziri wa mambo ya Nje Sam Kutesa alisema serikali haiungi mkono utetezi wa ushoga “sawa tu na vile tusivyoweza kutetea biashara ya ngono.”

Mwanablogu AfroGay anadhani kuwa serikali ya Uganda iliamini kuwa ingeweza kupitisha muswada huo kwa kuwa viongozi wa dunia wana mambo mengine katika akili zao:

Kama ilivyokuwa mwaka 1999 ambapo Museveni mwenyewe aliamuru kuwa mashoga wote wakamatwe na kufungwa jela katika kile ambacho ni wazi kilikuwa ni jambo lililowazwa hovyo [ kwa mara nyingine wafadhili waliingilia kati na Museveni akarudisha uamuzi wake nyuma], MU7 alifikiri kuwa muswada wa Bahati ungekuwa ni suala la pembeni katika nyakati hizi ambamo Obama amezama kwa Taliban, Gordon Brown ni bata mjinga na hakuna mwingine yeyote anayeitilia maananni Afrika zaidi Mchina anayefanana na samaki mla nyama. Lakini ukweli ni kwamba Obama na Ulaya watafurahi kuikabili Uganda kwa sababu ni shabaha rahisi ukilinganisha na, tuseme, China. Hillary Clinton alisema siku ile kuwa hukabiliani na China kwa njia ambayo unakabiliana na nchi ya dunia tat una hiyo ilikuwa ndiyo njia yake ya kuashiria kwa mzunguko mahali ambapo aniweka Uganda katika orodha ya ukubwa (wa mataifa).

Katika posti nyingine, AfroGay anajadili kile ambacho kinaweza kikawa kinatokea nyuma ya pazia:

Kwa hiyo, hata kama kwa makusudi hawawi wawazi hivi sasa, serikali ina mtazamo fulani juu ya muswada huu. Na mtazamo wao nim baya kwa nafasi yao kimataifa na kiufadhili. Mitetemo bado haijakwisha. Bahati amepanda kichwa kutokana na jinsi watu wengi walivyomtupia macho, na ni wazi kuwa bado anasherehekea dakika zake kumi na tano za umaarufu. Hivyo basi, ianaelekea hatakubali kirahisi. Lakini serikali itampinda mkono wake. Tazamia zahanati mpya kwenye jimbo la Bahati, na ahadi za hiki na kile kwa watu wa Ndorwa na naweza hata kuahidiwa ufadhili wa moja kwa moja kwa ajili ya kampeni yake ya kuchaguliwa tena. Anachokitaka Museveni nchini Uganda, Museveni hukipata na ninatabiri kuwa muswada huu utakuwa kivuli cha nafsi yake ya zamani wakati utakapofika Bungeni – kama utafika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.