Nepal: Mapinduzi Ya Gesi Inayotokana na Samadi

Kituo cha gesi inayotokana na samadi. Picha na mtumiaji wa Flickr Marufish. Na imetumika chini ya leseni ya hati miliki huru.

Kituo cha gesi inayotokana na samadi. Picha na mtumiaji wa Flickr Marufish. Na imetumika chini ya leseni ya hati miliki huru.


Teknolojia ya gesi inayotokana na samadi inaanzisha mapinduzi ya kijani nchini Nepal. Kwa mujibu wa WWF kuni ni chanzo cha nishati kinachopendwa zaidi nchini kwani takriban ya 87% ya kaya zinategemea chanzo hiki. Hata hivyo, gesi inayotokana na samadi imejitokeza kama mbadala wenye uhakika. Taarifa ya hivi karibuni ya AFP inadokeza kwamba Nepal inatengeneza pesa (karibu dola 600,000 za Kimarekani mwaka 2007) kwa kuuza kaboni kwa msaada wa vituo kadhaa vya gesi inayotokana na samadi nchini kote. Kwa nchi inayohangaika kutafuta chanzo nafuu na endelevu cha nishati, gesi inayotokana na samadi ni habari njema kwa nepal.

Globalwarming Arclein, blogu inayoandika kuhusu jinsi kilimo kinavyoweza kusaidia kupunguza gesi ya ukaa, inasema kwamba teknolojia ya hali ya chini ya gesi inayotokana na samadi inasababisha gesi hiyo kuwafikia Wanepali walio wengi ambao wanaishi vijijini:

“Uzalishaji wa gesi inayotokana na samadi hauna teknolojia ya hali ya juu. Inahitaji mtungi au tanki ambalo linaweza kutengenezwa kwa beleshi nap engine kuweka matofali ya uzio kama inavyofanya kwenye sehemu za kisasa za maji-taka. Kufunika na kunyonya gesi iliyotengenezwa kwenda kwenye mtungi wa kuhifadhia ni rahisi na matumizi baada ya hapo yanahitaji vifaa vichache vya kuokoteza.

Hitaji kubwa ni kufahamu kuwa inawezekana na kwamba itafanya kazi. Upakuzi wa mboji iliyotengenezwa hapo baadaye hakuvutii na hauna tofauti na kazi nyingine za namna hiyo. Siyo njia inayofaa ya kutengeneza gesi ya kutosha ili kupasha moto nyumba, lakini inatosha kabisa kuongezea moto wa kupikia na kuchemsha maji ya moto kwa njia bora.”

Mafinikio ya Nepal katika gesi inayotokana na samadi imewahamasisha majirani zake pia. Mshirika wa karibu wa Nepal, India nayo pia inatarajia kuendeleza vyanzo vya nishati mbadala ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka katika majimbo yake yanayokua kwa haraka katika nyanja ya viwanda. Razib Ahmed kwenye South Asia Blog, blogu yenye kutilia makini biashara na masuala ya jamii katika kanda hiyo, anasema:

“Ninavutiwa sana na gesi inayotokana na samadi kwa sababu ninaamini kuwa ina uwezo mkubwa siyo tu kwa Napal bali hata kwa nchi jirani kama vile India na Bangladeshi. Sekta ya ubia wa gesi inayotokana na Samadi Nchini Nepal (BSP-Nepal) ni Asasi Isyo ya Kiserikali ambayo inafanya kazi kwa ajili ya kuitangaza gesi hiyo nchini. Hadi mwezi Juni 2008, vituo 172,858 vya gesi inayotokana na samadi vimetengenezwa kutokana na msaada wao.

Na matokeo yake, zaidi ya watu milioni 1 wanazipata faida zake. Watu milioni 1 wanaweza kusikika kama vile si wengi sana kwako lakini inakupasa ukumbuke kuwa kwa kiasi kikubwa ni watu masikini wanaoishi sehemu za vijijini ambao wamenufaika na teknolojia hii. Si hivyo tu, lakini pia ningependa kukamata mawazo yako juu ya ukweli kuwa Nepal inaagiza Karibu asilimia 100 ya mafuta yake. Kwa hiyo, kila kituo cha gesi inayotokana na samadi kinachotengenezwa kunamaanisha uokoaji wa fedha za kigeni kwa nchi.”

Na kuvutiwa na gesi inayotokana na samadi si jambo linalopita kwa Nepal. Baada ya miaka mingi ya kazi ngumu na mipango, imeweza kuongeza hali ya kujulikana. Tukirudi nyuma mwaka 2005, Mallika Aryal katika RenewableEnergyAccess alitoa taarifa iliyohusu jitihada za Nepal kuataka kuzalisha uendelevu na faida kupitia gesi inayotokana na samadi.

“Mpango wa kuunga mkono gesi inayotokana na samadi nchini Nepal umeeneza kazi yake kuzifikia wilaya 66 kati ya 75 katika tsaifa hilo na una mpango wa kusimika vituo 200,000 mwaka 2009. Kituo kinachofaa kwa kayta iliyoko vijijini inagharimu dola za Kimarekani 300. Ruzuku za serikali zimefanya vituo hivyo kuwa na gharama nafuu. Mtu binafsi anawekeza dola za Kimarekani 200 tu na kitega uchumi chake hurejea baada ya miaka mitatu. Mpango mzuri sana!

Hivi sasa vituo vya kutengeneza gesi inayotokana na samadi vimo njiani kuwa “mpango mzuri” kwa ajili ya mazingira ulimwenguni. Wakati Itikadi ya Kyoto, mkataba wa hali ya hewa duniani, utaanza kutekelezwa Nepal Disemba mwaka 2005, itakuwa na haki ya kuanza kuuza hewa ya ukaa ambayo haikuzalishwa kwa kutumia gesi inayotokana na samadi na kuweza kupata hadi dola milioni 5 kwa mwaka.”

Ili kujua zaidi kuhusu jinsi gesi inayotokana na samadi inavyoisaidia Nepal, ifuatayo ni video iliyotengenezwa na Mradi wa Nepal katika Chuo Kikuu cha Mji wa Tokyo, Japan.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.