Uganda: Wanablogu wa Uganda Wajadili Muswada Unaopinga Ushoga

Muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda umepelekwa bungeni na sasa unamsubiri Rais Yoweri Museveni kutia saini ili kuufanya ushoga kuwa ni kinyume na sheria. Sheria ya awali haikuwa wazi sana lakini sasa muswada unaoitwa ‘Muswada wa kupinga ushoga wa mwaka 2009’ ulioletwa na mbunge David Bahati unaosema kwamba tendo lolote la ushoga ama tabia za kishoga zinaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo ama kifungo cha jela. The Ugandan anaandika:

Nitakuwa nikiwaleteeni sheria kadhaa mara tu rais atakapoitia saini sheria hii. Naam, wabaya wetu wameshasema tunatakiwa kudhibitiwa kwa sheria ngumu zaidi, lakini hili linaenda mbali zaidi ya hapo. Nikijaribu kufanya kosa…(mungu, mara ambazo nimetongoza na kukataliwa!) Kila moja ya mara hizo inastahili miaka 7 jela. Mbingu nzuri!!!! Kabla, tungeweza kustahili kufungwa kifungo cha maisha. gug anatangaza kwamba, Rais wa Jamhuri atakapoisaini sheria hii, gug atakuwa anastahili adhabu ya kifo…kwa sababu mimi na mpenzi wangu ni wakosaji, tunaivunja sheria hii.

Mswada pia unawazuia mashoga waliooana kuasili watoto; mtu yeyote anayesaidia, anayetetea ktuoa ushauri wa kisheria kwa tendo lolote la kishoga kwa namna yoyote atakabiliwa na adhabu ya kifungo kisichozidi miaka saba, au kutozwa faini ya shilingi milioni 100 za Uganda. Muswada unasema kwamba madhara ya ushoga ni pamoja na:

Utafiti unaonyesha kwamba ushoga una madhara mabaya yafuatayo pamoja na uwezekano wa matumizi zaidi ya nguvu, magonjwa ya zinaa, na matumizi ya madawa ya kulevya. Uwezekano wa kutengana na kuachana katika mahusiano ya kishoga pia yanasababisha mazingira yasiyoaminika kwa watoto wanaolelewa na mashoga kwa kuasili ama vinginevyo, na yanaweza kuwa na matokeo mabaya kisaikolojia kwa watoto hao. Na zaidi ya hayo, kutetea tabia za kishoga kunaharibu maadili yetu ya asili ya kifamilia.

Kwa kuzingatia historia, sheria, utamaduni na maadili ya kidini ambayo yanasema kwamba familia, yenye misingi ya ndoa baina ya mwanaume na mwanamke ni kiini cha jamii. Muswada huu unakusudia kuimarisha uwezo wa nchi wa kupambana na matishio yanayoanza kujitokeza ya ndani na nje dhidi ya familia za kitamaduni baina ya watu wa jinsia tofauti. Matishio haya yanajumuisha: dhana mpya wa haki za binadamu inayozipa nafasi tabia za mahusiano ya jinsia moja na tabia za kujibadilisha jinsia kuwa makundi ya watu yanayolindwa kisheria.
Aidha kuna hitaji la kuwalinda watoto wetu na vijana wanaofanywa kuwa wepesi kudhurika na ukatili wa kingono na kuharibiwa maadili yao kama matokeo ya mabadiliko ya kiutamaduni, teknolojia holela ya habari, ukuaji wa watoto bila wazazi na kuongezeka kwa majaribio ya mashoga kulea watoto katika mahusiano ya jinsia moja kwa njia ya kuasili, malezi ya kambo, ama vinginevyo.

Waandaaji, wachapaji na wasambazaji wa kazi zenye mambo ya kishoga hasa kama ni biashara, asasi hiyo isiyo ya kiserikali (AZISE) itafutiwa leseni ama usajili wake na mkurugenzi wake atakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela. Hii inajumuisha blogu za mashoga nchini Uganda:

Masikini wale wanaowaunga mkono. Hamjakosea kutupenda. Hapana, wapenzi wote wa mashoga, na mashoga wote Uganda watataabika, na kuadhibiwa na sheria hii. Mkutano wowote na waandishi wa habari? Hautaitishwa na mashoga wa Kiganda. Unaona, sisi ni watu waliotengwa ambao hatuwezi kufanana kamwe na Waganda wengine. Ha ha ha ha ha! Oh, blogu ya gayuganda ni mojawapo ya vitu ambavyo ni haramu, kwa mujibu wa muswada huu. Mimi ninautangaza ushoga kwa hasira katika blogu hii, nikilalamikia sheria kama hii. Kwa hiyo, miaka mitano gerezani, na akaunti yangu ya benki (isiyokuwepo) itakwapuliwa shilingi za kiganda milioni 100…! Na watu wanaothubutu kutupatia kondomu na vilainishaji kwa ajili ya ngono…au, kama utathubutu kuwa na mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mashoga nchini Uganda…au hata kujaribu kufundisha ngono salama. Kweli, adhabu ni ngumu. Ngumu mno. Gereza. Jela, na jela na mambo mengine.

Haya ni melengo ya huo muswada.

3.1. Malengo ya Mswada ni:

(a) Kuilinda ndoa kuwa ni ile kati ya mwanaume na mwanamke nchini Uganda;

(b) Kuzuia tabia za kishoga na vitendo vinavyohusiana nchini Uganda kwa sababu vinatishia familia za kitamaduni;

(c) Kulinda afya za wananchi wa Uganda dhidi ya madhara mabaya ya ushoga na vitendo vinavyohusiana;

(d) Kuanzisha sheria endelevu zinazolinda familia za kitamaduni ambazo zinaweza kuwa mfano kwa nchi nyingine;

(e) Kuzuia makubaliano ya mkataba wowote wa kimataifa, mikutano na matamko ambayo yanapingana au hayakubaliani na vipengele vya sheria hii;

(f) Kuhakikisha kuwa hakuna vyombo vya kimataifa ambavyo Uganda ni sehemu yao vinaweza kutafsirika ama kutumika nchini Uganda kwa njia ambayo haikukusudiwa wakati ambapo viliundwa;

(e) Kujitoa kwenye makubaliano yoyote ya kimataifa ambayo Uganda tayari ni mwanachama, au kuweka masharti ya kujihadhari, ambayo yanatafsiriwa upya ili kujumuisha kulindwa kwa tabia za kishoga, au kutetea ndoa za jinsia moja, au kutoa wito wa kutangaza au kufundisha kuhusu ushoga kama tabia yenye afya, ya kawaida au uchaguzi unaokubalika wa utaratibu wa maisha, au kutafuta kuanzishwa kwa tabia za kingono, mtazamo wa kingono, au utambilsho wa kijinsia au makundi madogo ya kijinsia kama makundi ya watu yanayolindwa kisheria; na

(f) Kuizuia Uganda kuwa mwanachama wa chombo chochote cha Kimataifa ambacho kinatamka wazi ujumuishaji na kulindwa kwa tabia za kishoga; kushabikia ndoa za jinsia moja; kutoa wito wa kushabikia na kufundisha kuhusu ushoga na mahusiano ya jinsia moja kama yenye kumaanisha afya njema, kawaida, ama uchaguzi wa namna ya maisha unaokubalika; na/au kutafuata kuanzisha tabia za kingono, mtazamo wa kingono, utambulisho wa kijinsia au makundi madogo ya kijinsia kama makundi ya watu yanayolindwa kwa nguvu ya sheria.

Gay Ugandan anakuasa kuchukua hatua hizi pamoja naye na kukuuliza ikiwa anastahili kufa kwa sababu hii:

Kama uko nje ya nchi, kwa nini, hivyo ni vizuri sana. Kusanyiko la watu wako linaweza kujulishwa mazuri yote ambayo baadhi ya Wakristo wa Uganda wanawatakia wenye dhambi waitwao mashoga wa Kiganda. Nina uhakika hasira zako zitasaidia. Barua, maandamano, maswali kwa viongozi wa Uganda, wa kidini na vinginevyo wanosafiri nje ya nchi hii. Hili ni swali la kimaadili, wanawezaje kuhalalisha kuniua mimi kwa sababu ni shoga, ninayeishi katika uhusiano wa kishoga na mtu mwingine ambaye naye ni shoga?

#Sawa, inakuwaje kwa mashoga wa nchi nyingine. Ninyi ni rafiki zetu. Ndio, tunathubutu kuwaomba msaada kaka na dada zetu mashoga, hasa wakati ambapo wananchi wenzetu wanaamini tunapaswa kuwa wazalendo kiasi cha ‘kufa’ kwa jina la uongofu wa kimaadili, kwa mungu na kwa nchi.
Waambie kundi la mashoga wenzio mahali uliko kuhusu suala hili.
Andaeni maandamano, makubwa na madogo. Mwelimishe yeyote asiyejua suala hili. Andikeni barua za kupinga. Kuweni waungwana, (mtayarishaji wa Mswada huu anasema eti sisi mashoga tunataka kumuua. Anasema eti tumeshamwandikia barua ‘za kumtisha’.)

Afrogay mwanabogu mwingine wa Uganda anaifananisha serikali ya Uganda na kikundi za Nazi, ansema wakati wa kuufutilia mbali muswada huu ni sasa:

Tena, kama nilivyotoa hoja hapa na kwingineko, tunashauriwa vyema kutunza marisawa kwa ya vita halisi kama muswada huu utapitishwa na kutiwa saini kuwa sheria. Kwa hiyo, Mimi sitarajii kusema mengi kuhusu nati na boriti za nini kina makosa katika (muswada) huo. Na sababu ni rahisi: kama tukionyesha nini ni kibaya hivi sasa, wabaya wetu watatumia hayo tunayoyasema ili kuuosha muswada huo. Cha Ni bora kupigia kelele kwa kosa hili la makusudi kwa sauti sana tuwezavyo dhidi ya chembechembe za kibaguzi za muswada huu bila kuwaongoza kuhusu udhaifu wa kiufundi unaojionyesha, kisheria, kikatiba na katika mitego (uwanja wa mabomu) ya haki za binadamu ambayo wanajiingiza wenyewe na muswada huu huku wakiwa wanatembea wakati wamelala usingizi.

Mwanablogu wa Naijeria Anengiyefa anafikiri kwamba muswada huu una makosa na jopo lililoutengeneza halina ufahamu wa kutosha kuhusu ushoga. Anasmea ushoga hauwezi kuwa kosa, huwezi kumwadhibu mtu kwa kuwa na hisia za kimapenzi na mtu mwingine:

Ndugu Bahati anaendelea na kutaka adhabu ya kifo kwa kile anachokiita “ushoga uliovuka mipaka”. Nimesoma na nikajiuliza kama Ndugu Bahati amewahi kuwa na fursa ya kukaa darasani maishani mwake, kwa kuzingatia kwamba isipokuwa awe mjinga aliyekubuhu, anatakiwa ajue kuwa hakuna vitabu vya sheria kwenye hukumu za kawaida za kisheria, (pamoja na Uganda), ambavyo vinarejea kosa linaloitwa ‘ushoga’. Ushoga hauwezi kuwa kosa! Huwezi kulifanya kuwa kosa na kumwadhibu mtu kwa kuwa na tamaa ya kimapenzi na hisia za kuvutiwa na mtu mwingine wa jinsia yake. Huwezi kuuthibitisha ‘ushoga’ kwenye mahakama ya kisheria kwa viwango vya ushahidi vinavyotakiwa kwenye mahakama ya jinai.

Anengiyefa anaona kwamba Uganda imeona unafiki wa wabunge waliungana na wako tayari kupitisha sheria ya kuufanya ushoga kuwa kosa kwa jina la maadili; hii inalishinda kusudi la kwa nini mfumo uko makini kuyafanya mahusiano ya hiari baina ya watu wawili wazima wa jinsia moja yawe jinai na kuacha masuala muhimu kama mapigano ya kikabila, ukabila, UKIMWI, ukabaji wa watotot nk:

Kulipuka kwa ushabiki huu wa hofu ya ushoga ni ushahidi wa unafiki unaotawala maisha ya siasa ya Afrika. Wakati ambapo muda wa gharama za bunge ulitakiwa kutumika kisheria katika mambo ambayo yana tija kwa maisha ya watu wa nchi hii; wakati watunga sheria wa Uganda na serikali ya Uganda ilitakiwa kuguswa na ustawi wa Waganda wanaoteseka, (ikijumisha watu wale wanaowapenda watu wa jinsia yao katika jamii yao, ambao wanahatarishwa kwa matumizi ya nguzu na unyanyapaa); wakati ambapo mamlaka za Uganda zilitakiwa kuangalia namna ya kulinda wale wananchi wa vijijini ambao ustawi wao ni jukumu lao; wakati ambapo changamoto zinazolikabili bara letu katika karne hii ya 21 zinatisha; tunachokisikia badala yake ni Muswada wa kupinga ushoga ukiletwa Bungeni. Muswada huu unaonekana kuwa muhimu kwa mujibu wa Mbunge Davidi Bahati aliyeuleta. Anadai kwamba lengo la muswada huu ni kuwalinda watoto na ‘familia zilizozoeleka kitamaduni’.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.