Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

Juma lililopita, huko Hammond, Louisiana, Beth Humphrey (ambaye ni mzungu) na Terence McKay (ambaye ni mweusi) walituma maombi ya kupata cheti cha ndoa na walinyimwa kwa misingi ya rangi zao. Afisa wa kutathmini na uandikishaji (Muamuzi wa Amani), Keith Bardwell, alidai kwamba katika uzoefu wake, “ndoa za rangi tofauti hazidumu kwa muda mrefu” na akasema alikuwa “akiamua hivyo kwa ajili ya watoto wa wanandoa hao”.

Sheria za Jim Crow” ambazo ziliwataka Wamerekani weusi na weupe kuwa na huduma tofauti zilikomeshwa mwaka 1965, na sheria zilizozuia ndoa na mahusiano ya kimapenzi kati ya watu wenye rangi tofauti zilikomeshwa katika majimbo yote ya Marekani mwaka 1967.

Lakini ubaguzi wa rangi bado upo. Ingawa muda mwingi huwa upo chini ya ardh, mara nyingine ubaguzi huo hunyanyua kichwa chake kibaya kwa namna ambayo si haiwezekani kutoonekana; habari hii ilitawala vichwa vya habari katika vyombo vya habari nchini kote Marekani, na kusababisha makala za wanablogu kutokea kwenye jamii za sehemu hizo na zaidi.

Katika majibu yaliyotokana na “utetezi” wa Bardwell kwamba huwafungisha ndoa watu weusi mara zote, blogu ya kupinga ubaguzi wa rangi iitwayo Stuff White People Do ilionyesha kuchukizwa kwake, kwa kusema:

Sawa, u mtenda haki na mema wa namna gani, Jaji Bardwell. Bila kutaja, uingiliaji wako (katika maisha ya watu) na ubaba wa kulazimisha.

Nikizungumzia nyumba ya Bardwell, ambayo nina hakika imezidiwa na kundi kubwa lenye furaha la watoto weusi kwa weupe wakicheza pamoja, alikuwa na haya pia ya kusema:

Nina mabiwi na mabiwi ya marafiki weusi. Huja nyumbani kwangu, ninawaoza, wanatumia msala wangu. Ninawafanyia kama ninavyomfanyia yeyote.

Mh ndio, marafiki weusi pia, wengi mno. Pale kwake, hadi bafuni kwake!

Mtoa maoni kwenye blogu hiyo, Siditty (ambaye pia aliandika makala yake hapa), aligusia hali ya kinyume cha hasira ya Bardwell:

Huwa ninajiuliza kuhusu mtu ambaye katokea Louisiana, mwenye historia ndefu ya kujichanganya na watu wa rangi tofauti, kwa kupitia mfumo wa utamaduni wa ukazi kati ya watu weupe na wanawake weusi (placage) kadhalika na utamaduni mchanganyiko wa jamii ya Kispania na Kifaransa nma Weusi (Creole), sasa hivi ghafla tu anaonekana kujali sana watoto. Jamii yake haikuwa inajali hivi kwenye miaka ya 1700, hapaswi kuwa hivyo anavyodai leo.

Blogu ya Racism Review ililichachafya suala la Bardwell “ kujali watoto” kwa ushahidi wa watoto waliotakana na uhusiano wa rangi tofauti:

Na, ili kuutazama zaidi ushahidi, watoto wa ndoa za wenzi wenye tofauti ya rangi huwa hawateseki ukilinganisha na watoto wengine kwa kigezo kwamba wanakulia katika mazingira yanayokubali tofauti za watu na watoto wa ndoa za rangi tofauti. Kama watoto wa namna hii watakutana na ubaguzi wa rangi (na matatizo mengine ya kimfumo), basi wana uwezekano mkubwa wa kukumbana na msongo, matatizo ya kiafya yanayohusiana na msongo wa mawazo, kama vile uvutaji sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Hayo ndiyo matokeo ya ubaguzi wa rangi, na hiyo ni sababu nyingine ya kufanya kazi ili kuukomesha ubaguzi wa rangi. Isitumike – kwa kupindua mantiki juu chini –kama sababu ya kuendeleza ubaguzi.

Na Black Girl in Maine aligusia pia kuhusu swali la “vipi kuhusu watoto?”, kwa kuelezea uzoefu wa mwanae ambaye ni chotara:

Na kwa watoto, vipi kuhusu watoto? Ndio, watoto chotara mara nyingine hupata usumbufu kutoka kwa wengine lakini sio mara zote na nadhani kati ya vijana wa leo inaonekana poa sana kuwa chotara. Kama rafiki yangu alivyoniambia mwanangu hapati matatizo na kupata marafiki wa kiume na wa kike. Nadhani wakati pekee ambapo watoto machotara huweza kupata shida ni pale wanapokosa mtu wa kuongea nao kuhusu asili yao. Nadhani wakati ambapo watoto wameunganishwa na historia ya asili yao na ya jamii yao, hiyo huwatengenezea nafasi salama kwao.

Nchini Marekani, sheria ya kuwazuia watu wa rangi tofauti kuoana ama kuwa na uhusiano wa kimapenzi katika majimbo mengi ilipiga marufuku ndoa za Wamarekani weupe na Wamerekani weusi (na wale wa asili nyinginezo) katika majimbo kadhaa. Wakati katika majimbo mengine, sheria hizi zilibatilishwa mwanzoni mwa miaka ya 1780, katika majimbo 16 sheria hizi hazikuondoshwa mpaka wakati wa kesi ya mwaka 1967 , kati ya Loving na Virginia, ambapo wenzi hawa wa rangi tofauti waliokuwa wameoana mjini Washington, D.C walitiwa chini ya ulinzi kwenye chumba chao cha kulala. Vita yao ya kisheria ilifika mpaka Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo sheria hizi zilifika mahali zikatupiliwa mbali.

Wanablogu kadhaa waligusia mtazamo wa kisheria kwa suala hili. Mwanablogu mmoja, Jay Says, anaandika:

Kama Jaji wa masuala ya Amani, anatakiwa kuelewa kwamba ndoa za rangi tofauti si kinyume cha sheria tena – baada ya kuonekana ni kinyume cha katiba miaka 40 iliyopita. Tukio hili limegusa hisia baada ya Maandamano ya Usawa Kitaifa mwishoni mwa wiki ambapo nilifanya mahojiano mafupi na wanandoa wa rangi tofauti, Bwana na Bibi Newman (pichani) kuhusu kwa nini wanaandamana.

Ubaguzi wa rangi, Uwepo wa matabaka, Ubaguzi wa watu wa jinsia tofauti, Hofu ya Ushoga, Kutovumiliana kidini pamoja na upendeleo wa aina nyingine vinaweza kuwapo na vipo katika jamii yetu, lakini havipaswi kuwepo kisheria. Kumruhusu mwajiriwa wa Serikali anayelipwa kwa kodi za watu “huru” wa Marekani (au katika mukhtadha huu jimbo lililo nchini Marekani) kutumia imani zake binafsi kuamua masuala yanayotawaliwa kwa sheria za kiraia ni kichefuchefu. Kama hakubaliani na ndoa za rangi tofauti, basi anahitaji kutafuta kazi nyingine –labda Mkuu wa Ku Klux Klan?

Mwisho, mwanablogu mmoja amechukua fursa ya kuligeuza suala hili kuwa wakati muafaka wa kujifunza. Yeye, ambaye blogu yake inatwa Ni Nini Ninachojua?, anawasihi wasomaji kufikiri kuhusu hisia zao wenyewe kuhusu mada husika:

Kama una wasi wasi kwamba ubaguzi wa rangi bado unaishi ndani yetu wote, fikiria unavyojisikia unapopata wazo la kuoa au kuolewa nje ya watu wa rangi yako, hasa wewe ukiwa ni mzungu na mwingine ni mweusi. Ndio, ni sawa kwa watu wengine, lakini hivi usingetafuta sababu nzuri zenye hoja zinzoshawishi za kuelezea kwa nini binti yako atayafanya maisha yake yawe magumu sana atakapomleta nyumbani mchumba wake mweusi? Kuwa mkweli. Hata kama ulisema, “Hakuna shida” hivi kweli haukusita hata kidogo kupata jibu? Kama haikuwa hivyo, basi wewe si wa kawaida.

Wakati Bardwell anasema sasa kuwa hatajiuzulu kwa sababu ya suala hili, jambo moja ni la hakika: bila ya shaka kuna habari zaidi zaja.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.