Paraguai: Rais Lugo Akiri Kuzaa Mtoto Wakati Bado Akiwa Askofu

Hivi karibuni rais wa Paraguai Fernando Lugo alikiri kuwa yeye ni baba mzazi wa mtoto wa Viviana Carillo, mtoto ambaye alitungwa wakati Lugo akiwa bado ni askofu wa Kanisa Katoliki la Roma. Pia alikiri uhusiano wa muda mrefu na Carillo. Habari hii inazua utata hivi sasa baina ya wanasiasa, vyombo vya habari, na wanablogu ambao wanaandika kusikitishwa kwao na kiongozi huyo, na ukweli kwamba kuna matatizo mengine makubwa yanayopaswa kuangaliwa ikilinganishwa na vitendo vinavyofanywa na wanasiasa.

Picha kwa hisani ya akaunti ya APC Flickr ya Fernando Lugo. Chini ya Hati Miliki Huria.

Picha kwa hisani ya akaunti ya APC Flickr ya Fernando Lugo. Chini ya Hati Miliki Huria.

Carlos Rodríguez wa Rescatar [es] analinganisha (mkasa huu) na yale yaliyotokea miaka iliyopita nchini Marekani, wakati aliyekuwa rais wakati huo – rais Bill Clinton alipokuwa na mahusiano yasiyofaa, nje ya ndoa na Monica Lewinski. Kuna wale wanaosema kuwa mahusiano hayo yalikuwa ni ya faragha na ya kibinafsi na kwamba hayakuathiri maslahi ya nchi aidha hayakuwa na athari yoyote kwa maisha ya wananchi wa Wamarekani. Na sasa Lugo amejitokeza na amekubali wajibu, anaandika kwamba suala hilo limefikia tamati kwa wananchi wa Paraguai [es]. Anaongeza kwamba kuna vitendo nyeti ambavyo vinatendwa na wanasiasa wengine ambavyo vinapaswa kusakamwa na wananchi wa Paraguai, na kwamba vyombo vya habari virejee na kumakinikia yaliyomo kwenye “ajenda ya taifa”

Hata hivyo, kwa kuwa Paraguai ni nchi ya Kikatoliki (Wnanchi wake wengi ni Wakatoliki) , wengi wamesikitishwa na ukweli kwamba Lugo alikiuka ahadi ya kanisa ya kujitenga na ngono, lakini kwa baadhi ya wanojiita wasiokuwa na dini kama vile Liam wa Políticamente Incorrecto [es], hilo si suala. Pia anaangalia maoni ya sekta tofauti kuhusiana na habari hii [es] ndani ya nchi na pia kimataifa:

Kuna shutuma zisizothibitishwa kutoka pande na sekta tofauti, wanawake waliokerwa, wanaume waliofurahi, wanachama wa chama cha Colorado wanaovuja furaha na wanachama wa chama cha Liberal wanaotamani mashitaka ya kisiasa, kuna wanahabari wanaolipwa kumlinda na wengine wanaomuandama kwa kadiri wanavyoweza. Watu wanaongelea mahusiano ya kimapenzi ya Lugo na nini kinachotokea katika wakati uliopo? Hakuna chochote, kama kawaida, nchi inasambaratika vipande vipande.

Jorge Torres Romero anaandika kwenye blogu yake Detrás del Papel [es], kwamba Lugo aliuhadaa umma:

Lugo aliuhadaa umma. Alijikweza kana kwamba ni mgombea tofauti, mgombea wa mabadiliko, wa maadili na ukweli. Lakini mwishowe, hana lolote bali ni muongo mkubwa. Alituuzia (aliwauzia, kwa sababu sikumpigia kura) sura ya utakatifu na hivi leo amepoteza mtaji huo pekee ambao alitegemeza ugombea wake: ukweli.

Ukweli ni kwamba japokuwa habari hizi zilitikisa na kuwashtua watu wote, wengi wanandhani kuwa suala hili halipaswi kuyaondoa macho kutoka kwenye yale yanayowagusa watu wa Paraguai.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.