MENA: Maoni Wakati Wa Kuapishwa Obama

Tukio la kihistoria limetokea Marekani leo wakati Barack Obama alipoapishwa kuwa rais wa 44. Wakati kuungwa mkono kwa Obama kati ya Waarabu kumekuwa kukipungua katika miezi michache iliyopita kufuatia uteuzi wake wa baraza la mawaziri na ukimya wake kuhusu mashambulio ya Israeli huko Gaza, wanablogu wa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini wanayo mengi ya kusema.

Bloga A Syrian in London anaorodhesha matukio ya wiki chache zilizopita wakati wa mashambulizi ya Israeli, halafu anaeleza:

Hapajatokea mwingine tangu Kennedy, na wengine wanasema hakuna rais mwingine wa Marekani aliyewahi kuwa na mvuto pamoja na matumaini makubwa, kutoka duniani kote, kwenye mabega yake. Katika hotuba yake ya kuapishwa, Rais obama alisema:

“tumechagua matumaini dhidi ya hofu, umoja wa nia dhidi ya migogoro na kutoelewana”

“tumetoa tamko la kumaliza manung'uniko yasiyo na maana na ahadi za uongo, visingizio na imani zilizopitwa na wakati, ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikinyonga siasa yetu.”

“Katika kutilia mkazo ukuu wa taifa letu, tunaelewa kwamba ukuu si haki yetu ya kupewa hivi hivi tu. Ni lazima tuupiganie.”

” chaguo ama la usalama wetu au maadili yetu, ni la uongo na tunalikataa”

“Je tunathubutu kuomboleza wafu?

“Je tunaweza kuwa na matumaini kwa wale wanaoishi?

Bloga Jar of Justice aliyeko Dubai, anadhani kwamba hotuba ya Obama ilikuwa na mapungufu:

Pamoja na kufikiri kwamba hotuba ya Obama ilikuwa nzuri – hakusita pale aliposema ‘Waislamu” lakini alijitahidi sana kuonekana mkweli pale “alipomshukuru” yule mpumbavu ambaye hatutamzungumzia tena baada ya leo – nafikiri kulikuwa na jambo muhimu lililokosekana kwenye htukio hili…

… lakini ninahisi kuwa Obama hatajishusha na kumhusisha yule mjinga zaidi ya ishara tu ya kidplomasia kwenye hotuba yake.

Bloga wa Kimoroko Laila Lalami, ambaye ni mkazi wa marekani ambye anakiri kumpigia kura Obama, kidogo ana matumaini zaidi na kuridhika kuwa siku ya Obama imewadia:

Nimeridhika kwamba siku ya Obama imewadia.

Miaka minane iliyopita, nilimpigia kura Ralph Nader kwa sababu nilifikiri kuwa hapakuwa na tofauti kubwa kati ya vyama vya Democrat an Republicanm kwenye masuala muhimu. Lakini baada ya upuuzi uliotokea Florida, maamuzi ya Mahakama ya Rufaa, na urais dhaifu uliofuatia, nilijifunza somo moja: Si kweli kuwa wanasiasa wote wako sawa. Kuna wengine ambao hawana vipaji, hawaguswi na busara zilizo wazi, ambao hawana huruma kiasi kwamba wanaifanya ofisi ya rais kuwa ni kitu cha mzaha. Nadhani hivi sasa situmaini kama kutakuwa na tofauti kubwa katika sera za serikali, hata hivyo bado ninajawa na shauku kwenye haya mabadiliko, kwa Barack obama, na kwa kuondoka kwa George W. Bush.

Washabiki wa Kimoroko wa Obama bado wanaendelea kupiga kampeni ya kumtaka rais Obama atoe hotuba yake ya kwanza nje ya nchi nchini Moroko.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.