Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele

Kama kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?

Ni kwa nini migogoro ya Afrika haitiliwi maanani na vyombo vya habari, hasa lile jinamizi linalendelea katika Kivu, hili ni swali la karne (sambamaba na lile swali linalouliza, kwa nini vyombo vya habari vya kimataifa, ikiwa wataandika habari zinazoihusu Afrika, huandika habari za migogoro tu).

Elia Varela Serra aliandika katika tovuti hii kuhusu swala hili, siku chache tu zilizopita, alitafsiri sehemu ya makala kutoka Rue89 iliyoandikwa na mwanahabari hugues Serraf. Jinsi Hugues Serraf alivyolitizama swala hili kulizaa hali tete kati ya wasomaji wengi wa lugha ya Kifaransa, wote, wasomaji wa Kikongo na wale Wakiislamu.

Wasomaji wengine wa Rue89 wanakubaliana na mtazamo wa Serraf.

Rafa anafafanua ni kwa nini vyombo vya habari vya Ufaransa vinaipa kipaumbele zaidi Palestina ikilinganishwa na Kongo:

Jamii ya Kifaransa imeushupalia mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina kutokana na ukweli kwamba kuna uwepo mkubwa wa watu wa jamii hizo ndani ya Ufaransa, jamii ambayo huyarejea yale yanayotokea huko [mashariki ya kati]. Kwa upande mwingine, nafikiri kwamba kwa kuwa Israeli ni nchi mojawapo ya “magharibi” kwa maana kwamba Israeli ni sehemu ya “dunia huru” (kama anavyosema Livni), watu wa Ufaransa wanajifananisha na Waisraeli, na kutokana na ukweli kwamba [Israeli] inatambulika kama nchi iliyostaarabika, na ina demokrasi sawa na yetu, na yenye watu wenye tabia na taratibu za maisha kama zetu, pamoja na jamii zinazoshabihiana, nchi kama hiyo inapofanya vitendo vya kikatili kama hivi, huwa tunatikisika. Tofauti na mgogoro wa Kongo ambao unaonekana kana kwamba ni moja tu ya madhila mengine yanayotokea kwenye bara lililolaaniwa ambalo watu hawalitilii maanani tena kwa sababu madhila ya namna hii hutokea mara kwa mara.

Msomaji mwingine wa Rue80, Pierre Haski:

Mwezi uliopita niliyaona maandamano ya Wakongo [pale kwenye Kasri ya Jamhuri mjini Paris] kuhusu mgogoro nchini mwao. Walikuwapo watu dazeni kadhaa, waliosindikwa nyuma ya kamba za polisi [wa kuzuia fujo], wapita njia hawakuwajali. Jumamosi, niliona maandamano ya Wapelestina yalipokua tu yakianza, tayari wapiga picha wa televisheni walikuwa wameshafika.

Lakini kuna wengi walioshutumu ujinga wa mwa mwandishi huyo kulihusu bara la Afrika. Katika makala yake Serrif alisema:

Mimi, ni sawa na wewe. Sifahamu sana mambo ya Kongo wala hili Jeshi la Upinzani la Bwana [LRA]… si hivyo tu, kuna Kongo mbili! Isitoshe Afrika ni ngumu kuielewa. Kati ya majanga, magonjwa ya kuambukiza, wakuu wa majeshi pinzani wanaorandaranda ndani ya magari ya Land Cruiser, na hayo yote… ni kina nani tunaowatambua kama kundi “zuri” au kundi “baya”?

Pia aliandika kwamba mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina unaweza ukawa uliandikwa zaidi nchini Ufaransa kwa sababu, kwa mtazamo wa umma, ni rahisi zaidi kutofautisha kati, “wema” na “waovu”.

Bloga Alex Engwete, ambaye amekuwa akiandika habari mpya mpya za mgogoro wa Kivu kwenye blogu yake, ameandika dhidi ya ujinga wa Serrif:

Nilianza kwa kushiriki hasira yako inayotokana na ukimya uliolizunguka balaa la Kongo kabla ya kugundua wapi ulipokuwa unaelekea katika aya zako tatu za mwisho. Nilitaka hata kukudokezea kile ambacho rafiki yangu mmoja mwandishi wa habari wa BBC alichoniambia kule Nairobi, ambacho shirika lake la habari tukuka lilimtaka afanye… kwamba aache kutuma taarifa kutokea Kongo ikiwa idadi ya waliokufa ni pungufu ya 50! Ni watu weusi walio katika kiini cha giza, isitoshe, ni sehemu ambayo “mambo ya kutisha tisha!” ni ya kawaida – kwa mujibu wa Joseph Conrad… Lakini niligundua baadaye, huku nimekata tamaa, kwamba kwako Kongo si kitu kingine zaidi ya mwongozo wako (wenye visingizio) uliotupeleka kwenye risala yako iliyopindapinda! Kama hujui lolote linaloihusu Kongo, waache wafu wapumzike kwa amani!


Familia zimeweka makazi katika jengo lililovunjwa baada ya kulazimishwa kuzikimbia nyumba zao kutokana na kupamba moto kwa mapigano katika jimbo la Kivu ya Kaskazini. (Picha na S. Schulman wa UNHCR).

Djé anayeblogu kwenye case en construction anaandika:

Msisimko wa habari ambao umelitilia mkazo suala la Gaza umekuwa na tabia ya kuvigeuza vyombo hivyo vya habari (na hivyo, umma mzima kwa ujumla) kutoka kwenye yale ambayo yanaendelea kujiri huko Kivu. Nina hakika, baadhi ya wanahabari wameweza hata kutengeneza faida kwa kutumia ulegevu wa mkazo kwa upande wa vyombo vya habari unaoendelea huko Mashariki ya Kongo, kwa minajili ya kusambaza propaganda zinazoipendelea Israeli.

Djé ameiita makala ya Serrif kama “jaribio la hovyo la kupotosha habari” na anamuomba aifikirie makala nyingine inayojadili masda hiyo hiyo, iliyoandikwa kwenye kongotimes.info ambayo inadai kwamba, ‘Vita hizi mbili zinabeba mashaka sawa, pamoja na hatari zinazoweza kuyumbisha eneo lote” [Fr].

Watumiaji wa wa mtandao wa Islamie.com kadjhalika walivunjwa moyo na ulinganishaji alioufanya Serrif na udaku uliofanywa na vyombo vya habari kuhusu swala la Gaza, kwa ujumla Abdullah anauliza, kwa kejeli, “Ni maiti ngapi za watu wa Afghanistan zinazopaswa kuwekwa kwenye mnara wa mazishi Gaza?” [Fr].

Katika mwangaza wa hisia kali hivi sasa zinazohusiana na Gaza, nimeghafirika sana tangu niliposoma nukuu ya Abou Ghazi inayosema kwamba kuna mauaji ya kinyama kila wakati yanayotokea huko Afghanistan ambayo hakuna mmoja anayeyajali. Siyo kwamba najihusisha zaidi au la kuhusu mauaji haya au yale. Lakini nukuu kama kama hii, ambayo inaonyesha (katika maana ya kwanza ya neno) mambo mengi.

Ni hali mbaya iliyoje tuliyokuwamo! Tunajiachia wenyewe tulishwe, tupumbazwe, na kuongozwa na vyombo vya habari.

Kwa kweli inanitia kichefuchefu.

Jounaïda:

Nukuu ya Abou Ghazi inashabihi upeo wetu finyu. Pia unaonyesha jambo moja: kwamba sisi ni vikaragosi wa vyombo vya habari, tulio na kiu ya habari za udaku.

Tunahitaji, na siku zote tutahitaji, vitendo madhubuti kwa ajili ya kaka na dada zetu wanaokandamizwa, mpaka hapo neno la Mungu litakapotawala dunia.


Wanaume wa Kipalestina wakiuzika mwili wa mtoto wa miaka 4 Lama Hamdan katika makaburi ya Beit Hanoun Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza tarehe 30 Desemba 2008. Lama na dada yake waliripotiwa kuwa walikuwa wakiendesha mkokoteni uliokuwa ukivutwa na punda siku ya Jumanne karibu na sehemu inayotumika kurusha makombora iliyokuwa ikilengwa na Waisraeli. (Picha na Amir Farshad Ebrahimi)

Souleymene:

… nimekuwa nikijiuliza jambo hili mara nyingi katika siku chache zilizopita. Lakini naweza kusema zaidi, mchakato huu tunaouna ni dalili tu na si gonjwa lenyewe. Wakati zoezi hili litakapofifia (na Allah anajua vyema…) na katika wakati wowote ule uwao, yote yatarudia kwenye “utaratibu”, na nikiangalia viongozi tulio nao, hapatakuwa na hatari ya machafuko. Wana-Jihadi tunaowaona kwenye televisheni huko Jordan na Yemeni kati ya sehemu nyingine, watakuwepo, na ALLAH awazidishie katika malengo yao. Waislamu watarudi kuendelea na shughuli zao za kila siku, Palestina itasahauliwa, na damu iliyomwagika huko Gaza pamoja nayo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.