Korea: Wajibu wa Kitaifa Wachuana na Dhamiri

Kijana mmoja anayetumikia jeshi kama askari polisi aliamua kutorudi kwenye kikosi alichokuwa akifanya kazi baada ya likizo na alipeleka taarifa kuwa dhamiri yake ilikuwa ikimshtaki. Sababu ilikuwa kwamba dhamiri yake ilimshtaki baada ya kuwa amewanyanyasa raia walioshiriki katika mkesha wa tukio la kuwasha mishumaa. Uamuzi wa kijana huyu umevuta hisia za watu wengi, uamuzi ambao unapingana na serikali na kumaanisha kwamba hawezi kumaliza muda wake wa kulitumikia jeshi.

Netizen anauliza maswali kuhusu suala hili.

Kijana, Lee Kil Joon, aliyekuwa akilitumikia jeshi kama polisi na ambaye alitumwa kwenda kuzuia tukio la mkesha wa kuwasha mishumaa, alitangaza ‘azimio la (kujisikia kushitakiwa na) dhamiri’, tangazo lake hilo limekuwa ni jambo kubwa. Askari Lee Kil Joon ambaye amepangiwa kazi katika kikosi cha kuzuia uhalifu na kuendesha doria katika kituo cha polisi cha Jungrang jijini Seoul alipitisha usiku mzima pasipo kurejea katika kituo chake cha kazi. Baadaye aliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Kanisa Katoliki la Sinwondong jijini humo jioni ya tarehe 27 mwezi Julai na kuanza rasmi mgomo wake mahususi kwa kipindi kisichojulikana baada ya tamko lake la kujisikia kushitakiwa na dhamiri dhidi ya wajibu na mfumo wa polisi wa kutuliza ghasia.

Alisema, “Nilipofanya kazi kama askari polisi, nilihisi kwamba tungweza kutumwa na wakuu wetu kudhibiti tukio ambalo tusingependa kulidhibiti” na “kwa hiyo niliamua kupinga uonevu wa kunilazimisha kutenda nisilopenda kwa sauti yangu mwenyewe …” […] Je, ninyi mnafikiri nini kuhusu uamuzi wake wa kutorejea jeshini kwa sababu ya kutumwa kwenda kudhibiti waandamanaji kwa nguvu kwamba kufanya hivyo ni sawa na ‘kuingilia uhuru wa dhamiri'?

Wanamtandao wa intaneti wengi wameunga mkono uamuzi wa kijasiri wa askari huyu na kueleza kwamba kuna matatizo mengi katika mfumo wa jeshi.

Lee Kil Joon alitangaza kushitakiwa na dhamiri kutoana na kitendo cha kutumia nguvu ili kuzuia tukio la mkesha wa uwashaji mishumaa.Alisema kwamba alijiuliza maswali mengi baada ya kusikia amri kutoka kwa kamanda wake ikisema ‘wapigeni pasipo kuonekana’ wakati wa mkesha wa kuwasha mishumaa katika uzuiaji wa raia na askari kwa kutumia mabavu. Hatimaye alitangaza mgomo wake kwa sababu ya kusukumwa na dhamiri. Hata hivyo, wapo wanaomkosoa.

Baadhi ya wanaotoka katika makundi ya kihafidhina wanamchukulia kama mtu mwenye matatizo ya akili. Hivi, kwa nini analaumiwa kiasi hiki? Je, ni kwa sababu “anagomea wajibu wa kulitumikia jeshi?” Hili ni swali ambalo ningependa kuwauliza watu wa makundi ya kihafidhina. Au, je, wanamchukia kwa sababu amefunua ukweli wa mambo? Kwa sababu ya kutilia shaka na kuwa na hatia kutokana na ukandamizwaji unaofanywa na polisi, kwamba ndiyo aliibuka na tangazo la kushitakiwa na dhamiri. Endapo kama polisi wangekuwa wanaheshimu uhuru wa kuandamana na kama wasingalidhibiti maandamano kwa nguvu, huenda jambo hili lisingetokea.

Licha ya ushawishi wa wazazi wake, alichojaribu kuonyesha ni matumizi mabaya ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya maandamano. Hebu tafakari hili kwa uwazi na ukweli. Hata kama wewe ni askari polisi ambaye huna budi kutawanya maandamano, je, ungejisikia vipi endapo kamanda wako angekuamuru ‘kuwapiga pasipo kuonekana'? Kwa sababu raia wako kwenye maandamano, basi, uwapige katika mahali ambapo hutaonekana. Je, hii si ghasia kwa kisingizio cha kuzuia uvunjaji wa sheria na kuleta utulivu? Kuwapiga raia si haki. Ndiyo sababu alichukua uamuzi huo.Badala ya kumpongeza kwa ujasiri wake, kwa nini tunamtukana?

Ni kweli kwamba kutokamilisha kipindi cha kulitumikia jeshi si jambo linalokubalika vilevile. Hata hivyo, kutatua tatizo la kwanini askari hakukamilisha wajibu wake inapaswa kuwa jambo la kupewa kipaumbele katika kuleta mageuzi.

Hata hivyo, masuala yanayohusiana na wajibu wa kulitumikia jeshi yana nafasi ya pekee nchini Korea. Si wanamtandao wengi wa intaneti wanaotafsiri kitendo cha askari huyo kwamba ni cha kugomea wakuu wake, bali wanaamini kwamba ni kisingizio cha kukwepa wajibu wa kulitumikia jeshi.

[…] unapoona habari hii, unadhani kwamba kuna jambo la maana. Lakini kwa maoni yangu, ni kama simulizi kuhusu mtu anayedeka na asiyetaka kulitumikia jeshi. Hebu sikiliza kile alichosema. “Nilijihisi vibaya kujipokea nafsi yangu, mimi ambaye nilitakiwa kutii amri bila kutia neno hasa pale nilipoamriwa kwenda kudhibiti mgomo na hasa iliponipasa kuvumilia kuzomewa na kugomewa na wananchi. Nilihisi kwamba utu wangu kama binadamu ulikuwa umefutiliwa mbali kabisa.” Hivi sasa kuna vijana wapatao 600,000 walio katika nafasi sawasawa na ile aliyokuwemo. Hawana budi kuishi kwa kutii amri na kufa ikibidi kwa amri. Kama angekuwa raia wa kawaida, ningeelewa uamuzi wake dhidi ya makumpuni au asasi gandamizi ambapo angekuwa akifanyia kazi. Hii ni jamhuri yenye kuheshimu uhuru na demokrasia, na kwa hiyo ni jamii ambapo haki za binadamu hazina budi kuheshimiwa.

Hata hivyo, katika nafasi yake kama askari hana fursa ya kueleza waziwazi vile anavyofikiri. Unapokuwa kijana katika jamhuri ya Korea, jeshini ni mahali ambapo huna budi kwenda kama sehemu ya wajibu kwa watu wa nchi hii. Kuna amri na majukumu ambayo huna budi kuyatunza kama askari jeshi au polisi. Lakini kwa vile alijifikiria nafsi yake tu, basi aliamua kupuuzia kila kitu. Hata kama kuna amri nyingine ambazo ni za kipuuzi, huna budi kuzitii kwa sababu uko katika kundi maalumu. Like Mwenyewe alisisitiza kwamba kwa sababu yeye ni mtu safi basi asingeweza kufuata amri za kipuuzi. Kama tutakubaliana na jambo hili, je, ni nani atakayekuwa tayari kujiunga jeshini, na je, ni nani atakayekuwa askari wa kutuliza ghasia au kufanya kazi kama askari polisi?

Endapo upo vitani, mbele ya kamanda anayekuamuru ‘songa mbele’, wewe unamwambia kwamba hutaki kuua watu. Unadai kwamba dhamiri inakushitaki na kwa hiyo unatelekeza silaha yako.

Je, ni nani atakayeilinda nchi hii? It is not so Hiyo haitofautiani sana na kile ambacho askari wa kutuliza ghasia hufanya. Hapo ni kundi zima linalotakiwa kufuata amri. Endapo kundi hili halitatii amri, basi ni jambo hilo litakalosababisha kusambaratika kwa kundi hilo. Je, ni nani anayependa kufuata amri za wengine bila kujali dhamiri zao zinawaelekeza vipi? Unapokuwa kwenye kundi fulani, basi kuna kanuni kwamba unalazimika kutii mambo ya kundi hilo. Ingawa hiyo ni kanuni isiyo sahihi na haina budi kubadilika,haipaswi kubadilishwa kwa namna ambavyo kijana huyu anataka iwe.

Kwa sababu ya umimi wake, je, askari wengine katika kikosi chake watafikiriaje sasa …

Ikiwa umewahi kupitia jeshini, naamini utaelewa ni nini ninachojaribu kueleza hapa. .[…]

Kumaliza muda wa kutumikia jeshini ni kama kuvuka geti (lango) fulani katika maisha.

[…] Kwa vyovyote vile Lee Kil Joon atakuwa na wakati mgumu sana kujaribu kuhimili uchungu alio nao hivi sasa kwenye dhamiri yake. Hata hivyo, natoa wito kwake kuendelea kuvumilia zaidi kidogo. […] hapa tunazungumzia maisha ya mtu mmoja. Je, tunaweza kukisia uchungu walio nao wazazi wake hivi sasa? Nafikiri jambo la maana hapa ni kwamba aweke wazi mambo yote ya kishenzi na kisha arejee kwenye kikosi chake cha jeshi. […] Kwa uzoefu wangu, askari polisi wengi ni watu wa kawaida tu. Ukiachilia mbali watu wenye malengo ya kisiasa, walio wengi hawaingilii tukio la kuwasha mishumaa kwa sababu wanamwunga mkono Lee Myung Bak. Hiyo ndiyo kazi yao. Kwa maneno mengine, wanafanya kile ambacho wakuu wao wanawaamuru. Wanafanya hivyo kwa sababu hicho ndicho wanachotegemea kuendesha maisha yao.

Hata kwa kubaki jeshini, bado ana fursa nyingi ambamo anaweza kujikagua na kutafakari maisha yake. Anaweza kuwa na maisha motomoto hata kwa kubaki jeshini.

Jamani, hebu tusaidi kumrejesha jeshini, hebu tuokoe maisha ya mtu huyu mmoja![…]

Wako watu wengine wanaochukulia hii kama fursa ya kipekee ya kukomesha mfumo wa kuwa na askari wa kutuliza ghasia, ambao huwa una kawaida ya kupelekea vijana katika utumishi wa jeshi.

[…] Kwa nini hatuna budi kumlinda Lee Kil Joon
Katika tukio la kuwasha mishumaa jana katika Kanisa Katoliki, mwakilishi wa Chama kipya cha Jinbo, Lee Duk Woo alieleza waziwazi kwa nini hatuna budi kumlinda. Sheria ya askari polisi wapiganaji, usuli, na tatizo tulilo nalo hivi sasa – nchi inayopoteza ziada na kutuma askari huku na huko bila mpangilio maalumu. It Hii ni kinyume cha Katiba ibara za 24 – 25. Kwa lugha nyepesi, askari wa kutuliza ghasia ni askari na kwa hiyo hakuna msingi wa kisheria kwamba askari wanaweza kuwazuia raia kama si katika hali ya sheria za kijeshi. Katika kipindi cha miaka 17, ni mara ya kwanza tunapata fursa ya kupigania haki hii kwa sababu kuna mtu mwenye kuguswa na jambo hili na ambaye amejitokeza. Ndiyo kusema
kuwa uamuzi wa Lee Kil Joon ni muhimu. Ikiwa yeye hatunaye basi ni vigumu kuendeleza ombi la namna hiyo.

Mnamo mwaka 1991, askari mmoja wa kutuliza ghasia alitangaza kujisikia kushitakiwa na dhamiri na sisi tulipeleka ombi la kufutiliwa kwa mbali mfumo wa kuwa na askari wa kutuliza ghasia. Lakini wakati ule wa serikali ya Roh Tae Woo, tulishindwa kwa uamuzi wa uwiano wa 5:4. Hivi sasa, miaka 17 baadaye, uelewa kuhusu haki za binadamu na mambo ya ulimwengu umekua anayeguswa na mfumo huu sasa ametangaza kujisikia kushitakiwa na dhamiri, sasa tunayo fursa nyingine ya kuomba kufutiliwa mbali kwa mfumo huu. Tumepata fursa nyingine baada ya miaka 17. Ndiyo sababu hatuna budi kumlinda Lee Kil Joon.[…]

Je, unajua? Endapo askari wa kutuliza ghasia anapuuza amri ya mkubwa wake na kuondoka kikosini anaweza kutupwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka kati ya 3 hadi 10? Ni wazi kwamba Lee Kil Joon amechukua uamuzi mgumu katika maisha yake. Atafuatiliwa na kusukwasukwa na maadui na kupitia wakati mgumu sana katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo ya ombi letu. Ni kwa sababu hii kwamba si askari wachache wa kutuliza ghasia walijisikia kushitakiwa na dhamiri lakini wakashindwa kufanya tamko. Kabla ombi hili halifafikishwa kunakohusika, ikiwa atakabidhiwa upande mwingine wa wasiopenda ombi hili,basi atapitia wakati mgumu sana – je, hili si jambo gumu kwa mtu kulivumilia peke yake?

—[…]

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.