Angola: Kuelekea Uchaguzi Unaosubiriwa Kwa Muda Mrefu

Ni chini ya chini ya mwezi mmoja kwa Angola kabla ya kuingia zoezi linalosubiriwa zaidi katika aya za historia yake. Miaka kumi na sita baada ya uchaguzi wake wa mwisho, Waangola kwa mara nyingine tena watapata fursa ya kutumia haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi wa bunge,utakaofanyika kuanzia tarehe 5 mpaka 9 Septemba.

Hali ni ya ukimya, japokuwa kuna hisia zinazotofautiana katika umma. Watu wanojiweza wanasema watakwenda ughaibuni; wengine wanatabasamu na kujihakikishia kwamba hakuna litakalotokea kwani Waangola hawataki tena vita na mateso; wakati wengine wanakimbilia madukani kunua vyakula, ikiwa muovu atalipa na mambo yataenda vibaya, kama ilivyotokea mwaka 1992. Kama itakumbukwa, wakati ule chama kikubwa cha upinzani, UNITA, kilishindana katika uchaguzi na mapigano yalizuka, yakapelekea kuibuka tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika miaka kumi baadaye, na kifo cha kiongozi mwenye mvuto mkubwa wa chama hicho, Jonas Savimbi.

Inapokuja kwa wafanyabiashara wa nje waishio Angola, wao hawakusudii kurudi kwenye nchi zao. Jumii ya wafanya biashara inaamini kwamba kila kitu kitabaki kama kilivyo baada ya uchaguzi na kwamba hapana ulazima wa kubadilisha majukumu ya kikazi. Jotace Carranca [pt] anatoa tahmini ya hali ilivyo:

Baada ya hatua za kwanza za uchaguzi, ambazo zilikuwa ghafiri na zenye athari mbaya, uchaguzi wa pili wa Bunge nchini Angola unakuja kwa kasi. Kama mchakato huu, kwa wengi, ni sawa na matumaini mapya na kuimarika kwa demokrasia nchini kote, kwa wengine, walio sehemu za mashamba na kwa wale walio mikoani ambao waliteseka na ghasia, na matokeo ya vita vilivyojiri baada ya uchaguzi wa mwa 1992, nadhani bado kuna hisia za woga, kutokuwa na uhakika, mtazamo hasi pamoja na kutokuamini katika faida zitakazofikia maisha ya wananchi kutokana na mchakato huu. Katika maeneo haya kuna haja ya kufanya kazi ya kurahisisha mchakato mzima ili kwenda mbele zaidi ya vishawishi vya kisiasa, vionjo, vya kiutamaduni, vya kidini na vya kifilosofia. Ni lazima tutetee na kuimarisha dhamira za watu na za jamii kwa ujumla.

Rais wa Angola jose Eduardo Dos Santos ameshatoa rai ya kutaka utulivu na mpangilio siku za kupiga kura, alieleza kwamba “ni muhimu kuhakikisha kuwa usalama wa raia na ulinzi wa mali zao, kwa sababu usalama wa umma ni kipaumbele”. Kiongozi huyo aliongeza kwamba ni muhimu “kuheshimu mitazamo na fikra za wengine” bila kutumia ” maneno au vitendo vya vurugu”.

Tunategemea kuwa wapiga kura milioni 8.3 watakuwa na mazingira yenye amani kwa upigaji kura na watafanya hivyo katika njia ya safi na inayoeleweka vyema. Kuna zaidi ya vituo 12 elfu vya kupigia kura katika dola ya kitaifa. Wkati huo huo, Angola tayari imo kwenye vuguvugu la kampeni linaoloendeshwa na vyama tisa vya kisiasa. Kwa taarifa zaidi kuhusu mlengo wa kila chama kati vyama hivyo vya siasa tafadhali tembelea blogu ya Eugenio Costa Almeida. [pt].

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.